BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Raia wa Marekani, Brandon Summerlin (31) ameieleza Mahakama kuwa anakusudia kumwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) ya kukiri na kuomba kupunguziwa adhabu ili aweze kulimaliza shauri lake.
Summerlin ambaye ni mwalimu wa mafunzo kwa njia ya mtandao, anakabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mescaline zenye uzito wa gramu 56.04, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach, ametoa maelezo yake leo Februari 21, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, muda mchache kabla ya Serikali kumsomea hoja za awali (PH).
“Mheshimiwa hakimu mimi nakusudia kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ili niweze kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi yangu na hapa tayari nimeshaandika barua,” amedai Summerlin na kisha kuchana karatasi iliyokuwa kwenye daftari lake kwa lengo la kuiwasilisha mahakamani hapo.
Hata hivyo, wakili wa Serikali, Tumaini Maingu alimpa utaratibu kuwa anatakiwa kuandika barua kwenye karatasi zuri na kisha kuiwasilisha kwa mkuu wa gereza husika ambaye ataiwasilisha kwa DPP.
Awali, Wakili Maingu alidai kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja za awali na upande wa mashitaka wako tayari.
Baada ya kueleza hayo, wakili Maingu alimkumbushwa shtaka lake kwa kumsomea hati ya mashtaka.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Hakimu Huruma alimuuliza kama yuko tayari kusomewa hoja za awali
Mshitakiwa alidai kuwa ana nia ya kuandika barua kwenda ofisi ya DPP kwa ajili ya kuingia makubaliano.
Kutokana na hali hiyo, hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 6, 2023 itakapotajwa.
Mshtakiwa alirudishwa rumande kwa sababu shtaka linalomkabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.
Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 11/2022. Anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 12, 2022, jijini hapa ambapo alikutwa na dawa za kulevya aina ya Mescaline zenye uzito wa gramu 56.04, kinyume cha sheria.
MWANANCHI