johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Taarifa za sasa zinasema Muuaji wa Watu waliokutwa kwenye viroba huko Kware amepatikana na anahojiwa na Polisi kujua asili yake na sababu za kufanya Mauaji hayo.
Source: Citizen TV
====
DCI nchini Kenya, Mohamed Amin amesema mtuhumiwa aliyekamatwa ,auaji ya Kware, Collins Khalisia mwenye umri wa miaka 33 kutoka Vihiga amekiri kuua wanawake wasiopungua 42 ikiwemo mkewe kati ya mwaka 2022 na Julai 11, 2024.
Amekutwa na simu na laini za simu wakati anakamatwa Kayole leo.
====
Jomaisi Khalisi (33) amekiri kuwaua wanawake 42, ikiwa ni pamoja na mke wake mwaka 2022 kisha kwenda kuitupa miili hiyo kwenye dampo la Kware- Mukuru jijini Nairobi.
Julai 13, 2024 ilipatikana miili 9 ya wanawake kati ya umumri 18-30 waliokuwa wameuliwa kwa kukatwa vipande na kisha uwekwa kwenye magunia katika dampo hilo
Baadhi ya vitu vilivyosemekana kupatikana nyumbani kwa mtuhumiwa ni pamoja na simu 10, line 24 za simu, vitambulisho 8 na nguo za wanawake. Pamoja na panga na magunia kadhaa ambayo linashukiwa kutumika kwa ajili ya mauaji hayo
Tukio hili limegundulika baada ya Polisi nchini Kenya kuanza uchunguzi wa watu waliotekwa na kuuliwa wakati wa maandamano yaliyokuwa yakiendelea nchini humo Julai 2024
UPDATE
- Collins Jumaisi Khalusha, akana kufanya mauaji ya Wanawake 42