Mtuhumiwa wa mauaji ya Kware akamatwa, akiri kuua wanawake wasiopungua 42 ikiwemo mkewe

Mtuhumiwa wa mauaji ya Kware akamatwa, akiri kuua wanawake wasiopungua 42 ikiwemo mkewe

Ngoja nitunge story
Utakuta alikuwa jela kwa mauwaji ila katolewa ajifanye ndio muuwaji ili kutuliza vurugu

Ndio maana zikaitwa SiriKali
 
Kwa kiSwahili

15 July 2024
Nairobi, Kenya

Jinsi jeshi la Polisi Kenya lilivyofanikiwa kumkamata mtuhumiwa akitoka kuangalia fainali ya Eufa Euro 2024 katika vibanda umiza

View attachment 3043055
Collins Jumaisi Khalusha, mshukiwa mkuu wa msururu wa mauaji yaliyopelekea miili ya wanawake kugunduliwa katika jalala la Kware kwa, Mukuru Njenga jijini Nairobi. Picha: Mwananchi Digital

Collins Jumaisi Khalusha ametambuliwa kama mshukiwa mkuu wa msururu (serial killings) wa mauaji yaliyosababisha miili ya wanawake kugunduliwa katika eneo la taka la Kware, mtaa wa mabanda wa Mukuru Kwa Njenga.

Siku ya Alhamisi, wakaazi waligundua miili katika eneo hilo la kutupia taka, na kusababisha zoezi ambalo kufikia sasa limeshuhudia takriban miili 8 iliyoagwa ikitolewa.

Katika maelezo zaidi leo Jumatatu, Mohamed Amin, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai alifichua kuwa polisi walimvamia Khalusha huko Soweto Jumatatu asubuhi.

Khalusha alikamatwa nje ya klabu (Vibanda Umiza) alikokuwa ameenda kutazama Fainali za Euro 2024 kati ya Uhispania na Uingereza.

"Msako wake na matokeo yake kukamatwa kulifuatia uchunguzi wa kina wa simu ya mkononi iliyokuwa ya mmoja wa waathiriwa ambaye ni Josephine Mulongo Owino, ambapo baadhi ya miamala ya pesa kwa njia ya mtandao wa simu zilifanyika siku ambayo Josephine alipotea.

Amin alieleza zaidi kuwa mshukiwa huyo aliwaongoza polisi hadi nyumbani kwake Kware, iliyoko umbali wa mita 100 kutoka eneo la kutupia taka ambapo miili imeopolewa.

Vitu vilivyookotwa nyumbani kwa Khalusha ni pamoja na;
• sim kadi 24
• Simu 10 (simu janja 8)
• Laptop yangu
• Hard drive (Hifadhi kuu ya data)
• Viendeshi vya flash mbili na kadi ya kumbukumbu
• panga moja (machete)
• viroba (mifuko) 12 sawa na yale yanayotumika kujaza miili kwenye bwawa la Kware
• jozi 1 ya Glovu ya kazi ngumu
• 8 Kadi za Utambulisho wa Taifa
• Mkoba wa rangi ya waridi
• chupi mbili za kike rangi ya waridi
• Misokoto 5 ya bangi
• Tepu 4 kubwa
• Jaketi 1 la kiakisi
• hati mbili 2 (Title Deeds)
• Vitabu 2 vya kuandika kumbukumbu na hati nyinginezo mbalimbali.

Katika ungamo kwa maafisa wa polisi, Khalusha alisema ametupa miili ya wanawake 42 katika jalala la Kware.

Mwathiriwa wake wa kwanza alikuwa mke wake Imelda Judith Khalenya, ambaye alimuua mwaka wa 2022.

"Baada ya kuhojiwa, mshukiwa alikiri kuwarubuni, kuwaua na kutupa miili ya wanawake 42 kwenye eneo la kutupia taka zote zilizouawa kati ya 2022 na hivi majuzi Julai 11, 2024," alibainisha Amin.

Kufikia Jumatatu asubuhi, jumla ya maiti 9 zimeopolewa kutoka kwenye jalala linalosubiri upasuaji wa kufanyiwa upasuaji (postmortem) wa kiuchunguzi kuanza leo katika Nyumba ya Kuhidhia Maiti ya Nairobi, ambayo zamani yalikuwa Hifadhi ya Maiti ya Jiji.
NAWAPA PONGEZI POLISI INTELEGENT KENYA KWA KUMPATA MUHALIFU WITHIN SHORT TIME, NA VITIBITISHO LUKUKI VYA UTHIBITISHO USIO NA SHAKA, HONGERA!
 
Taarifa za sasa zinasema Muuaji wa Watu waliokutwa kwenye viroba huko Kware amepatikana na anahojiwa na Polisi kujua asili yake na sababu za kufanya Mauaji hayo.

Source: Citizen TV

====

DCI nchini Kenya, Mohamed Amin amesema mtuhumiwa aliyekamatwa ,auaji ya Kware, Collins Khalisia mwenye umri wa miaka 33 kutoka Vihiga amekiri kuua wanawake wasiopungua 42 ikiwemo mkewe kati ya mwaka 2022 na Julai 11, 2024.

Amekutwa na simu na laini za simu wakati anakamatwa Kayole leo.

Abra kadabra.
 
Kwani wale
Wanajeshi ambao walimwagwa mtaani waliondolewa na polisi kurejeshwa?
 
1721111692496.png

Jomaisi Khalisi (33) amekiri kuwaua wanawake 42, ikiwa ni pamoja na mke wake mwaka 2022 kisha kwenda kuitupa miili hiyo kwenye dampo la Kware- Mukuru jijini Nairobi.​

Julai 13, 2024 ilipatikana miili 9 ya wanawake kati ya umumri 18-30 waliokuwa wameuliwa kwa kukatwa vipande na kisha uwekwa kwenye magunia katika dampo hilo

Baadhi ya vitu vilivyosemekana kupatikana nyumbani kwa mtuhumiwa ni pamoja na simu 10, line 24 za simu, vitambulisho 8 na nguo za wanawake. Pamoja na panga na magunia kadhaa ambayo linashukiwa kutumika kwa ajili ya mauaji hayo

Tukio hili limegundulika baada ya Polisi nchini Kenya kuanza uchunguzi wa watu waliotekwa na kuuliwa wakati wa maandamano yaliyokuwa yakiendelea nchini humo Julai 2024
 
Taarifa za sasa zinasema Muuaji wa Watu waliokutwa kwenye viroba huko Kware amepatikana na anahojiwa na Polisi kujua asili yake na sababu za kufanya Mauaji hayo.

Source: Citizen TV

====

DCI nchini Kenya, Mohamed Amin amesema mtuhumiwa aliyekamatwa ,auaji ya Kware, Collins Khalisia mwenye umri wa miaka 33 kutoka Vihiga amekiri kuua wanawake wasiopungua 42 ikiwemo mkewe kati ya mwaka 2022 na Julai 11, 2024.

Amekutwa na simu na laini za simu wakati anakamatwa Kayole leo.

====
Uyo jamaa amekaa kama mtu ambaye yupo kwenye protocol serikalini 😁
 
Back
Top Bottom