Tulia Padri kama uko chumbani kwa askofu wako, daawa ikuingie usirushe vichwa
Kuabudu Sanamu
Hii pia ni ibada ya msingi katika dini ya Kikristo ambapo sala za waumini wake (Wakristo) huwa hazitimii bila ya kuomba na kuabudu sanamu. Masanamu yanayohusishwa zaidi katika ibada hizo ni pamoja na sanamu la mungu-mtu Yesu wa Kikristo akiwa amebebwa na mama yake na kwenye sanamu lingine akiwa amekufa msalabani, sanamu la "Bikira Maria", sanamu la malaika na masanamu mengine mengi ya watakatifu wa Kikristo waliokufa!
Kama maandiko ya Biblia tukufu yafundishavyo, ibada hii (ya sanamu) ifanywayo na Wakristo, kiasili imetokana na watu wa mataifa (wapagani). Uthibitisho wa hilo tunaupata katika maandiko yafuatayo:
"Bali walijichanganya na mataifa, wakajifunza matendo yao. Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao". (Zaburi 106:35-36).
Kwa uchache, maandiko hayo juu yanathibitisha wazi kuwa waasisi na wahusika wakuu wa ibada hiyo (ya sanamu) ni watu wa mataifa, yaani wapagani.
Sambamba na ukweli huo, Biblia haikuacha pia kubainisha jinsi Yehova alivyowakemea wanadamu tangu mapema kujaribu kuchonga (kufanya) na kuabudu sanamu, kama ifuatavyo:
"Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao". (Kumbukumbu la Torati 5:8-9).
Katika maandiko hayo juu, tunaona wazi jinsi Yehova anavyowakataza wanadamu kuchonga na kuabudu sanamu ya aina yoyote. Makemeo hayo juu ya Yehova ndio yanayosimamisha amri yake kuu ya pili kati ya amri zake zile kuu kumi ndani ya Biblia tukufu alizowapa wanadamu.
Ingawa alidhamiria kumhubiri Mungu mtu wa dini yake ya Kikristo mwenye desturi na sifa za miungu-watu ya wapagani, lakini Bwana Paulo hakuikubali ibada ya sanamu (tazama Wagalatia 5:19).
Hata hivyo, kwa kule kuwawekea Wakristo msingi wa kuzipenda na kuzifuata kwa moyo mkunjufu, imani na ibada za kipagani kamwe hawezi kukwepa dhima kutokana na leo ibada hiyo (ya sanamu) kujaa tele na kujizika mizizi katika dini yake ya Kikristo.
Kwa ujumla, ibada hiyo (sanamu) iliyomo katika dini ya Kikristo ni ibada inayotokana na dini ya kipagani ambayo (kama tulivyoona hapo awali) Yehova amewakataza vikali wanadamu kuitenda.
Kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa Wakristo kutenda ibada hiyo ni uthibitisho wa wazi kwamba hawamwabudu Yehova, Mungu wa Nabii Ibrahimu, Ismaili, Isaka, Yakobo, Musa, Yesu, Muhammad na Mitume na Manabii wake wengine wote aliowatuma duniani (a.s.), kwa kuwa ibada hiyo haitokani na yeye (Yehova).