Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Akibaka wake za watu anasingizia Mungu alimtokea na kumwambia afanye hivyo. Hivi kweli Mungu anaweza mwambie mtu eti baka tu ni haki yako?
Leta andiko amebaka wacha kelele nenda kamsome DAUDI wa kwenye biblia yako alimpataje mama yake mfalme selemani uje utoe majibu humu
 
Kurani nzima imesomwa na kila aya itatikiswa ili watu wajionee ukweli wa mambo.

Kwa mfano kuna tukio mke wake Muhammad,Aisha, alisemekena kuchepuka.Jambo hilo likashikiwa bango na baadhi ya walioamini mpaka kufikia hatua ya kumueleza Muhammad kwa nini anaendelea kubembelezana na Aisha wakati wanawake wamejaa?Kwa nini asiachane na aoe mke mwongine?

Kelele na zomeazomea zilipozidi, katika hali ya Kushangaza,Muhammad akaingia ndani kwa mkewe Aisha na alipotoka nje akasema ameshaongea na Mungu na Mungu kamdhihirishia kuwa hilo suala la Ugoni, Aisha anasingiziwa tu na hapo hapo Aya ikashuka juu ya masuala ya Ugoni kwamba ili ugoni uthibitike ni lazima kuwepo mashahidi.Na baada ya aya hiyo kushuka, ile timu iliyokuwa inasambaza ubuyu ule wa Aisha kuchepuka au kukamatwa ugoni wakaadhibiwa vibaya sana kwa kuchapwa mijeledi! Ni Mungu gani anafanya kazi namna hiyo?
Mkuu upo vizuri sana, kama hawakuelewi basi tena.
 
Tunaendelea kuhakiki au kutikisa aya zinazozitangulia aya za Jua kuzama katika Bwawa la matope ili kujiridhisha kama ni kweli ni Mungu alikuwa anaongea katika Sura hiyo au ni kitu kingine tu. Katika sura hiyo hiyo ya 18(Al-Kahf ),aya ya 50 inaonekana Shetani anao madhuria:

"
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu."

Kwa mjibu wa Kamusi ya Kiswahili,Dhuria ni ndugu katika ukoo.Je,shetani naye anao ndugu?
Utakaa sawa shetani tafsiri yake ni Mpingaji anaweza kuwa katika watu au katika majini kwa lugha nyepesi shetani ni sifa
Mkuu upo vizuri sana, kama hawakuelewi basi tena.
kisa cha DAUDI unakifahamu cha kuzini na mke wa uria mhiti?
 
Juzi na jana mumetueleza kuwa habari za Dhul-Qarnaini zilikuwa ni simulizi za Mungu kwa Muhammad.Sasa tunaanza kuchambua sura nzima ya Al-Kahf (sura ya 18) inakokutwa hiyo habari ya Jua kuzama katika matope.Nifuatilie:

1. Aya ya 1-6 inaongelea ukuu wa Kurani:

"1 - Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo.2 - Kimenyooka sawa, ili kitoe onyo kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri.3 - Wakae humo milele.4 - Na kiwaonye wanao nena: Mwenyezi Mungu ana mwana.5 - Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu. 6 - Huenda ukajihiliki nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya!"

Na kuanzia aya ya 7-8 kunaongelewa uweza wa Mungu na mifano ya uweza huo ikiwa ni viumbe vinavyoonekana kwa macho:

"7 - Kwa hakika tumevifanya vilioko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao wenye vitendo vizuri zaidi. 8 - Na hakika Sisi tutavifanya vyote vilio juu ya ardhi kuwa kama nchi ilio pigwa na ukame. 9 - Bali unadhani ya kwamba wale Watu wa Pangoni na Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu?"


Na kuanzia aya ya 10-26 ndio zinaongelewa habari za hao vijana wawili waliozimia pangoni kwa miaka mia tatu:

"8:10 - Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu.

18:11 - Tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa wa kadhaa.

18:12 - Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili lilio hisabu sawa muda walio kaa.

18:13 - Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu.

18:14 - Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.


18:15 - Hawa watu wetu wameshika miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhaahiri? Na nani aliye dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu?

18:16 - Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu.

18:17 - Na unaliona jua linapo chomoza linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni; na linapo kuchwa linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa basi huyo ni mwenye kuongoka. Na anaye muacha kupotea basi hutampatia mlinzi wala mwongozi.

18:18 - Nawe utawadhania wamacho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeli watokea hapana shaka ungeli geuka kuwakimbia, nawe umejaa khofu.

18:19 - Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi anajua zaidi muda mlio kaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa akuleteeni cha kukila. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala asikutajeni kabisa kwa yeyote.


18:20 - Kwani wao wakikutambueni watakupigeni mawe, au watakurudisheni katika dini yao; na hapo hamtafanikiwa kabisa!


18:21 - Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipo kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao.


18:22 - Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao. Wanavurumisha ovyo. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua sawa sawa hisabu yao. Hawawajui ila wachache tu. Basi usibishane juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize khabari zao kwa yeyote yule.

18:23 - Wala usisema kamwe kwa jambo lolote lile: Hakika nitalifanya hilo kesho -

18:24 - Isipo kuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unapo sahau, na sema: Asaa Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.

18:25 - Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu, na wakazidisha tisa.

18:26 - Sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi muda walio kaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona kulioje na kusikia kwake! Hawana mlinzi isipo kuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake."



Aya ya 6-82 inaongea juu ya Musa na kijana wake walivyokuwa katika safari na wakajikuta Kijana wake amemsahau samaki aliyechoropokea baharini:

"60 - Na pale Musa alipo mwambia kijana wake: Sitoacha kuendelea mpaka nifike zinapo kutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu.


18:61 - Basi wawili hao walipo fika zinapo kutana hizo bahari mbili walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kaporonyokea baharini.

18:62 - Walipo kwisha pita alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machofu kweli kwa hii safari yetu.

18:63 - Akasema (kijana): Waona! Pale tulipo pumzika penye jabali basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hapana aliye nisahaulisha nisimkumbuke ila Shet'ani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.

18:64 - (Musa) akasema: Hayo ndiyo tuliyo kuwa tunayataka. Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyo jia.


18:65 - Basi wakamkuta mja katika waja wangu tuliye mpa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyo toka kwetu.


18:66 - Musa akamwambia: Nikufuate ili unifunze katika ule uwongofu ulio funzwa wewe?

18:67 - Akasema: Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami.


18:68 - Na utawezaje kuvumilia yale usiyo yajua vilivyo undani wake?

18:69 - Akasema: Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, utaniona mvumilivu, wala sitoasi amri yako.


18:70 - Akasema: Basi ukinifuata usiniulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia.


18:71 - Basi wawili hao wakatoka, hata walipo panda jahazi (yule mtu) akaitoboa. (Musa) akasema: Unaitoboa uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya.


18:72 - Akasema: Sikukwambia hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?


18:73 - (Musa) akasema: Usinichukulie kwa niliyo sahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu.


18:74 - Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuuwa. (Musa) akasema: Ala! Umemuuwa mtu asiye na kosa, na wala hakuuwa! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa!

18:75 - AKASEMA: Je! Sikukwambia kwamba hakika wewe huwezi kuvumilia kuwa pamoja nami?

18:76 - Akasema: Nikikuuliza kitu chochote baada ya haya usifuatane nami, kwani umekwisha pata udhuru kwangu.

18:77 - Basi wakatoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa kuwakaribisha. Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka, (yule mja mwema) akausimamisha. (Musa) akasema: Ungeli taka ungeli chukua ujira kwa haya.

18:78 - (Yule mtu) akasema: Huku ndio kufarikiana baina yangu na wewe. Sasa nitakueleza maana ya yale uliyo kuwa huwezi kuyastahamilia.

18:79 - Ama ile jahazi ilikuwa ya masikini za Mungu wafanyao kazi baharini. Nilitaka kuiharibu, kwani nyuma yao alikuwako mfalme anaghusubu majahazi yote.


18:80 - Na ama yule kijana, wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukakhofu asije watia mashakani kwa uasi na ukafiri.


18:81 - Basi tulitaka Mola wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika, na aliye karibu zaidi kwa huruma.


18:82 - Na ama ukuta, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako khazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria."

Aya ya 65 inadokeza mtu mmoja ambaye alikutana na Musa na Kijana wake, wakiwa njiani wanarudi kumtafuta yule samaki ambaye alisahaulika.Ni mtu huyu huyu anaendelea kuwa na Musa katika maongezi hadi aya ya 82:

"65 - Basi wakamkuta mja katika waja wangu tuliye mpa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyo toka kwetu."


Na kuanzia aya ya 83,ndipo kunaanza ufafanuzi wa habari za Dhul-Qarnaini:

"83 - Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.


18:84 - Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.

18:85 - Basi akaifuata njia.

18:86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema."

SASA UTATA UKO HAPA:

1.Ni nani huyu Mja "Basi wakamkuta mja katika waja wangu tuliye mpa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyo toka kwetu" ambaye anaongea na Musa na kumufafanulia habari mbalimbali kama anavyotajwa katika aya ya 65? Je,Muhammad au ni nani?

2. Kama ni Muhammad ina maana Muhammad alikwisha kuzaliwa wakati huo hadi aweze kuongozana na Musa katika safari hiyo?Katika Imani ya Kiyahudi kunasadikiwa Musa aliishi kati ya mwaka 1391-1271KK.Mkatoliki Jerome anakisia kuwa Musa alizaliwa mwaka 1592KK na James Ussher anakisia kuwa Musa alizaliwa mwaka 1571Kk.Sasa,je,muda huo Muhammad alikuwa ameshazaliwa hadi aweze kuongozana na Musa?


3. Kama sio Muhammad ni Mja gani mwingine wa mwenyezi Mungu anayetajwa na aya hiyo?

4. Aya ya 83 inapoanza kwa uyakini ni mwendelezo wa muongeaji yule yule aliyekuwa anaongea na Musa kuanzia aya 65-82.Je,munaposema aya hiyo inamuhusisha Muhammad na Mungu(Mungu akiwa anamsimulia Muhammd habari za Dhul-Qarnaini), ina maana kwa kadri ya aya zinazoitangulia aya hiyo ya 83, Mungu munayemsema kuongea na Muhammad katika aya ya 83-86, ndiye huyo huyo "mja wa Mungu" ambaye Musa alionana naye njiani katika aya ya 65?

Tatizo lako ni hili, huwa unaharibu mambo. Qur'an haisomwi kama unavyosoma makala ya gazeti kisha unaiona umeielewa, la hasha! Haisomwi hivyo na hapa ndipo wengi mnapochanganya habari na mnaharibu mambo.

Aya ya 10 kuhusu ahlul kahfi idadi uliyoitaja ya hao vijana siyo sahihi na mtirirko wa hizo aya Qur'an ipo wazi kabisa kwamba wapo waliyosema idadi yao ni 2 na wa 3 wao ni mbwa idadi ikaendelea mpaka wapo waliyosema idadi yao ni 6 na wa 7 wao ni mbwa. Na hayo yote yalikuwa yanasemwa na watu ambao walitofautiana idadi halisi ya hao watu wa mapangoni. Lakini mwisho kabisa Qur'an ikamalizia idadi kamili anayoijua ni Mungu pekee.

Kuhusu aya ya 60 inazungumza kuhusu habari za Musa a.s na kijana wake walifunga safari ya kwenda kukutana na MTU na Mungu akampa ishara nabii wake Musa a.s akiona mabadiliko Fulani ambayo yalikuwa ni ya samaki basi ndipo hapo wamefika kwa huyo mtu.

Huyo mtu hakuwa Muhammad s.a.w kama wewe unavyoandika bali huyo mtu alikuwa ni Hidhri. Na unafahamu ni kwa nini Musa a.s alipelekwa kwa hidhri? Unajua Hidhri ni nani? Na ni wapi uliona tafasiri inasema huyo ni Muhammad? Mkuu haya mambo yapo juu ya uwezo wako. Kusafu kwenye mitandao au kusoma Qur'an au ahadithi kutoka lugha mama ( kiarabu) kwenda kwenye lugha ya mhusika na kumfanya atambue kilichoelezewa, hakumfanyi kujua mantiki nzima ya kilichokusudiwa. Ukitaka kuyajua haya mambo ni sharti ukae chini ufundishwe. Kupekua kwenye mitandao au kusikiliza jambo kuhusu uislam kwenye memory card au kuangilia kwa video au kusoma makala yanayohusu uislam kama haujakaa chini ufundishwe, miaka 100 haya mambo hautayaelewa. Mtaishia kujichanganya na mwisho wa siku mnaharibu mambo.
 
Utakaa sawa shetani tafsiri yake ni Mpingaji anaweza kuwa katika watu au katika majini kwa lugha nyepesi shetani ni sifa

kisa cha DAUDI unakifahamu cha kuzini na mke wa uria mhiti?
Nakijua sana, Daudi alipata taabu sana baada ya kufanya hila na kumchukua mke wa mtu . Biblia ipo wazi kabisa.
 
Tatizo lako kubwa hujui kutofautisha nafsi ya kwanza,pili na tatu katika umoja na wingi na hii ni kutokana na uwezo wako wa kufikiri kuwa mdogo sana.Tatizo lako hili umelionyesha pia katika kisa cha watu wa pangoni,katika kisa hiki kuna makundi mawili la kwanza ni la watu wa pangoni na la pili ni la watu wa mji ambao yule mmoja wa pangoni alienda kununua vitu kwa hela ya miaka mingi iliyopita.
Kwahiyo ALLAH anazungumza mambo ya panda zote ambazo kuzungumziwa kwao kuna jambo ambalo watu wa ulimwengu wote wanapaswa kujifunza.Kwahiyo maongezi ambayo we umeyatolea mfano katika kisa cha watu wa pangoni ni mazungumzo kati ya yule mtu aliyetumwa na wenzake miongoni mwa watu wa pangoni pamoja na watu ambao yeye alienda kununua vitu kwakutumia ile hela ya zamani.
Kwahiyo kuna mazungumzo ya watu wa pangoni wenyewe kwa wenyewe,pili kuna mazungumzo kati ya mtu mmoja wa pangoni na wauzaji wa vitu katika mji ambao alienda kununua vitu
 
Ni wazo zuri mkuu lakini kwa suala la Uislamu,document pekee ambayo ina uvuvio ni Kurani tu na ni kwa sababu ndiyo iliandikwa na Mungu na kisha ikashushwa hivyo hivyo kwa Muhammad kupitia kwa malaika Jibrili.Kwa hiyo,ningetaka kusindikiza hoja yangu na maelezo ya wanazuoni wa Kiisalmu lazima tungedanganywa kwa namna fulani.Na wewe umejionea jinsi ambavyo wametuletea stori tofauti tofauti na kile kilichoko katika Kurani.mintarafu suala la Jua kuzama katika dimbwi la matope.Kile walichotueleza, sio hicho ambacho kiko katika Kurani.
Mkuu unajua hata hayo maandiko uliyoweka ni tafsiri tu ya Qur'an kwa kiswahili,na hata waliyotafsiri ni hao hao wanachuoni,Sasa ukisema wanachuoni watakudanganya basi hata hayo maandiko uliyoleta hapa pia yawezakuwa wamedanganya.
 
Nakijua sana, Daudi alipata taabu sana baada ya kufanya hila na kumchukua mke watu. Biblia ipo wazi kabisa.
sasa mbona wamtolea povu mtume kumsingizia kubaka kumbe huko kwako mbakaji unae tena wamjua DAUDI na unakubali tena sio kubaka na mume wa huyo mwanamke alimuua
 
Mkuu unajua hata hayo maandiko uliyoweka ni tafsiri tu ya Qur'an kwa kiswahili,na hata waliyotafsiri ni hao hao wanachuoni,Sasa ukisema wanachuoni watakudanganya basi hata hayo maandiko uliyoleta hapa pia yawezakuwa wamedanganya.
kama khadir(hidhiri) amjui huyo awezi ielewe hiyo sura maisha yake yote hadithi za mtume zimekuja wazi kuhusu khadir na sababu za kuitwa ilo jina khadir na sababu ya nabii musa kwenda kumtafuta huko kwenye maji mm namuangalia najua hoja zake ni nyepesi
 
(

Mkuu:

Wanazuoni wa Kiislamu toka uzi ulipobandikwa walituambia kuwa suala la Jua kuzama katika matope ilikuwa ni maongezi kati ya Muhammad na Mungu.Ndio kusema Mungu alikuwa akimpatia Muhammad simulizi jinsi Dhul-Qarnaini alivyoliona Jua likizama mbele ya upeo wa macho yake.Tuliosoma aya hiyo ya 18(Al-Kahf ) kwa kina tuliona ngoja tuwakubalie hivyo wanavyosema ili wafunge milango na madirisha kabisa ili washindwe namna ya kutoka mbele ya safari.Sasa tunawauliza:

1.
Je,Ni Muhammad ndiye anatajwa na aya ya 65 kama mja wa Mungu?

2. Je,kama Muhammad ndiye Mja ambaye alikutana na Musa na Kijana wake wakiwa wanamtafuta samaki aliyesahauliwa na kijana wake,ina maana Muhammad wakati wa uhai wa Musa naye alikwisha kuzaliwa?

3.Kama Kurani haisemi uongo,hivi inaingiaje akilini kwa samaki ambaye Musa na Kijana wake walikuwa wakisafiri naye na kisha kusahaulika,kuweza kuchoropoka na kisha kuingia baharini tena? Huyo samaki alimudu vipi kuwa hai nje ya maji kwa safari ile kiasi kwamba aliweza kuchoropokea tena majini?

"18:60 - Na pale Musa alipo mwambia kijana wake: Sitoacha kuendelea mpaka nifike zinapo kutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu.

18:61 - Basi wawili hao walipo fika zinapo kutana hizo bahari mbili walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kaporonyokea baharini.


18:62 - Walipo kwisha pita alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machofu kweli kwa hii safari yetu.

18:63 - Akasema (kijana): Waona! Pale tulipo pumzika penye jabali basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hapana aliye nisahaulisha nisimkumbuke ila Shet'ani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.

18:64 - (Musa) akasema: Hayo ndiyo tuliyo kuwa tunayataka. Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyo jia.

4.
Aya zilizotangulia ile ya 62,kunaonekana ni simulizi la safari ya Musa na Kijana wake tu lakini ghafla katika aya ya 62 kunaonekana kuna watu zaidi ya watu wawili, ambao wanamuomba Kijana wa Musa chakula wale.Je,hao watu wengine ni akina nani?

5.Ghafla kuanzia ya 65 anaongezeka mtu mwingine safarini ambaye ndiye Musa anamuomba aambatane naye safarini.Ni mtu huyu anayejiunga katika safari ya Musa katika ya 65 ndiye anaendelea hadi aya ya 83 anapoanza kumuhadithia Musa habari za Dhul-Qarnaini.SASA.tuwaulize wanazuoni wa Kiislamu,ni Musa ndiye aligeuka akawa Muhammad na kisha kusimuliwa habari za Dhul-Qarnaini?
Wewe jamaa ni kufanya makusudi au ni kweli hauelewi?!. Wapi Hidhri huyo mtu aliyekutana na Musa a.s ndiye aliyemuhadithia habari za Dhul Qarnayn? Habari za Dhul Qarnayn + watu wa mapangoni asili ya haya maswali ni Wayahudi wa Madinnah, waliwatuma waarabu waende kwa Muhammad s.a.w wakaamulize hayo maswali na la tatu yake swali walilouliza wayahudi kwa Muhammad s.a.w ni nini roho. Lengo lilikuwa kujua kama kweli ni mtume au laa. Kwa sababu wayahudi na waisrael haya mambo wanayajua kwao imetoka mitume mingi, wanafahamu kuna mambo hayafahamiki isipokuwa kwa mitume tu ndiyo yanafahamika. Na ndiyo chanzo cha kushuka suratul Kahfi.

Hiyo sura ndiyo iliyobeba majibu ya maswali yao.
 
Hata kama wamegundua kwamba Mungu hakuwahi kusema hivyo kwamba Jua linachwea katika matope meusi,ni suala la kukiri tu hadharani na kufuta hiyo aya na kisha maisha yanaendelea.Kwani kuna shida gani kufuta hiyo aya katika Kurani na kubakisha yale yaliyo ya kweli?
Wakiamua kufuta aya moja ina maana zote zilizobaki zinakosa hadhi ya kuwa kweli.
 
Neno "SEMA" ni fupi sana lakini kuonyesha kwamba ni muhimu sana na hata mtume alikuwa anasoma Quran hakuliondoa kwani linanyesha uhalisia kwamba aliyekuwa anaambia atamke hayò maneno ni mtu asiyejua chochote juu ya anachoambiwa.
Picha za Haa Mym zimetoa jibu sahihi na jibu linalotosha na huu mjadala huu kuisha.Kisa kinachozungumziwa cha jua kuzama kwenye matope anaambiwa mtu jinsi ambavyo mtu anayezungumziwa aliona jua kutokana na upeo wake kuwa mdogo kama wewe mtoa mada.Kwahiyo kutokana na uwezo wa ALLAH kuona yaliyomo vifuani mwa viumbe wake alikuwa anamwelezea habari ya mambo ya Ghaibu ambayo binadamu hana uwezo wa kuyajua kirahisi.Kwamfano Surat Jinn mtume hakuwepo wa hakuyasikia lakini ALLAH alimuelezea.Mfano wa kitu ambacho umekianzishia uzi kinafanana sana na kitu ambacho kimezungumziwa kwenye Surat Jinn.Soma aya ya kwanza ya Surat jinn halafu uniambie hayo maneno kazungumza nani?
 
Mi wasiwasi wangu sio kwa Muhamad wala simlaumu. Mimi wasiwasi wangu ni kwa yule GABRIEL.wake. ndio nina wasiwasi nae[emoji63]
 
Hayo yote tutayaleta humu hadi yapatiwe majibu.Sasa wameanza kuhamisha magoli kwa kusema kwamba Kurani haisomwi kama vitabu anavyoandika Shigongo.Sawa, lakini mbona hawatuonyeshi hivyo vitabu vya kufafanulia hayo ambayo yameandikwa kwa mafumbo na Mungu?
Hadithi zao wenyewe hawaziamini. Shia watakwambia hizi ni za suni za uongo na suni nao watakwambia hizi za shia ni za uongo. Sasa haijulikani zipi hadithi sahihi.
 
Duuuh ww jamaa kichwa kizito kwelikweli al khadr ndio alikutana na musa kwenye maji ww uwe unasoma aisee unanchosha

Hatujakaa kwamba ni al khadr ndiye alikutana na Musa.Sasa tueleze mambo yafuatayo:

!. Uislamu umeanza miaka 500BK na Musa alizaliwa miaka ya 1500KK hivi.Je,huyo Al khadr anakuwaje Mja wake Mungu wakati uislamu haujakuwapo muda huo?

2.Ukisoma Vizuri sura ya 18, kuanzia ya 65 hadi 82, utaona ni mazungumzo kati ya Al khadr(kwa maelezo yako) na Musa juu ya mambo mbalimbali na kuanzia aya 83-86 ndio hizo habari za Dhul- Qarnaini zinajitokeza.SASA,hebu tuambie hapo Muhammad yuko wapi anapoelezewa na Mungu juu ya Dhul- Qarnaini.?
 
Kweli kabisa, yapo mengi yana changanya sana Mud anasema shetani ni mbaya ila jini kiumbe mzuri hana shida anaweza kushirikiana na binadam bila shida.
Sio hilo tu alimtolea mfano "MTUMWA" wake ambaye alikuwa ni mtu mweusi kuwa ndio shetani anafanania hivyo.
Supriseeeee:: Mohamed alikuwa na watumwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom