Kumbe hata nilivyo iweka kislam silamu napo huelewi; nikuulize Adam alikuwa tunda Akiwa duniani au sardaus [emoji47] [emoji53] utaelewa kwa lazima tu kama unavyo kula roasted farja
View attachment 873175 [emoji117]
View attachment 873178 [emoji39] [emoji39]
Sasa twageukia yaliyofanyika katika muda aliokaa Yesu Msalabani. Hata katika dakika ya mwisho Yesu alikuwa imara kudakuliza:
Eloi, Eloi, lama sabachtani? (Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?)
Huzuni kubwa iliyoje hiyo, na yenye kuumiza mno iliyoje hali hiyo ya kukata kwake tamaa! Kilio chake hicho chaashiria kwa uwazi kwenye ahadi ya zamani na matumaini ambayo pengine Mungu alikwisha mpa. La sivyo, kilio chake hicho hakina maana asilani.
Hicho kinakataa katakata nia yake na upendo wake wa kujitwisha kwa hiyari mzigo wa dhambi za watu wengine, na kinakanusha moja kwa moja wazo hili ya kwamba yeye alitazamia kufikiwa na saa ya mauti wakati huo.
Kwa nini kilio hicho cha maumivu ikiwa yeye mwenyewe alidai kuadhibiwa hivyo? Kwa nini kumlaumu Mungu ama kumwomba
aokolewe? Maneno ya Yesu yanapaswa kuzingatiwa kutokana na yaliyofanyika hapo kabla.
Yeye alikuwa akimwomba Mungu wakati wote kwamba kikombe kichungu kimwepuke.
Sisi Waislamu twaamini ya kuwa Yesu alivyokuwa mwema na mtukufu akamfanya Mungu asikatae maombi yake.
Bila shaka alikwisha ambiwa ya kuwa dua yake imepokelewa tayari.
Siamini katu ya kwamba yeye alitoa roho yake juu ya msalaba.
Kwangu mimi hamna hapa hitilafu bali yote yanalingana na kuafikiana.
Alihesabiwa kuwa mfu kwa sababu ya maoni ya mtazamaji fulani ambaye hakuwa daktari wala hakupata nafasi ya kumkagua.
Mtazamaji tu mmoja aliyekuwa anamwangalia kutoka mbali akihangaika na kufadhaika isije Bwana wake mpendwa akafa, akaona tu kichwa chake kilichochoka sana kikainama na kikaegemea kifuani pake, basi akapaza tu sauti:
Lo, ametoa roho yake.
Hapa shabaha yetu ni kukagua tu mantiki na busara ya falsafa na itikadi ya Kikristo. Jambo ambalo limethibitika barabara ni kuwa Yesu alizimia au alikufa lakini kwa vyovyote mshangao wake unahakikisha ya kuwa yeye alitazamia kinyume kabisa cha kilichotendeka.
Kama ni kifo alichotaka, basi mshangao wake aliodhihirisha hauna maana kabisa
. Maelezo yetu sisi Waislamu ni kwamba Yesu alishangaa kwa sababu yeye aliahidiwa usiku mmoja kabla alipofanya maombi mbele ya Mungu ya kwamba ataokolewa katika kifo cha Msalabani.
Lakini Mungu alitimiza ahadi yake kwa mpango wa kumfanya azirai ili walinzi waamini kwamba amekufa na wakamkabidhi Yusufu wa Arimathaya mwili wake ili kuwatolea jamaa zake.
Mshangao wa Yesu tunaouona katika kauli yake ya mwisho, hata Pilato alishirikiana katika mshangao huo. Maana alipopashwa habari ya kifo cha Yesu, Pilato akasema kwa mshangao: 'Amekwisha kufa' (Marko 15:44).
Haikosi yeye Pilato alitambua kwa sababu ya kazi yake hiyo ya kuwa Gavana wa Uyahudi kwa muda mrefu ya kwamba mtu hawezi kufa haraka hivyo juu ya msalaba.
Alielewa sana ya kwamba mtu kupata kufa juu ya msalaba katika muda mdogo wa saa chache ni kinyume cha kawaida.
Hata hivyo akakubali ombi la kutoa mwili katika hali hiyo kwa siri. Ndiyo sababu yeye analaumiwa siku zote kwamba alifanya mpango wa kumwokoa Yesu. Inasemekana ya kwamba kwa sababu ya kushawishiwa na mkewe alipanga kumtundika msalabani katika wakati ulio karibu sana na Sabato.
Pili aliruhusu kutoa mwili ilhali ripoti ya kifo cha Yesu ilikuwana shaka shaka. Uamuzi huo wa Pilato uliwahangaisha sana
Wayahudi waliomlalamikia na kueleza shaka yao kuhusu kifo cha Yesu. (Mathayo 27:62-66). INAENDELEA