Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Roho Takatifu Ni Nini?
Jibu la Biblia
Roho takatifu ni nguvu za utendaji za Mungu. (Mika 3:8; Luka 1:35) Mungu huituma roho yake kwa kuelekeza nguvu zake mahali popote anapotaka ili kutimiza mapenzi yake.—Zaburi 104:30; 139:7.
Katika Biblia, neno “roho” limetafsiriwa kutokana na neno la Kiebrania ruʹach na neno la Kigiriki pneuʹma. Mara nyingi, maneno hayo hurejelea nguvu za utendaji za Mungu, au roho takatifu. (Mwanzo 1:2) Hata hivyo, Biblia pia hutumia maneno hayo kwa njia nyingine:
Pumzi.—Habakuki 2:19; Ufunuo 13:15.
Upepo.—Mwanzo 8:1; Yohana 3:8.
Nguvu inayotendesha viumbe hai.—Ayubu 34:14, 15.
Mwelekeo wa mtu au mtazamo wake.—Hesabu 14:24.
Mungu na viumbe wenye miili ya roho kama malaika.—1 Wafalme 22:21; Yohana 4:24.
Maana hizo zote zinatoa wazo la kitu kisichoonekana na wanadamu ambacho hufanya mambo yanayoweza kuonekana. Vivyo hivyo, roho ya Mungu, “kama tu upepo, haionekani, si kitu halisi, na ina nguvu.”—An Expository Dictionary of New Testament Words, by W. E. Vine.
Biblia pia hurejelea roho takatifu ya Mungu kuwa “mikono” au “vidole” vyake. (Zaburi 8:3; 19:1; Luka 11:20; linganisha Mathayo 12:28.) Kama tu msanii anavyotumia mikono na vidole vyake kufanya kazi zake, Mungu ametumia roho yake kutokeza vitu kama hivi:
Ulimwengu.—Zaburi 33:6; Isaya 66:1, 2.
Biblia.—2 Petro 1:20, 21.
Miujiza iliyofanywa na watumishi wake katika nyakati za kale na pia kazi yao ya kuhubiri kwa bidii.—Luka 4:18; Matendo 1:8; 1 Wakorintho 12:4-11.
Sifa nzuri zinazoonyeshwa na watu wanaomtii.—Wagalatia 5:22, 23.
Roho takatifu si mtu
Inaporejelea roho ya Mungu kama “mikono,” “vidole,” au “pumzi” yake, Biblia inaonyesha kwamba roho takatifu si mtu. (Kutoka 15:8, 10) Mikono ya msanii haiwezi kufanya kazi bila akili au mwili wake; vivyo hivyo, roho takatifu ya Mungu hutenda tu anapoielekeza. (Luka 11:13) Pia Biblia hulinganisha roho ya Mungu na maji na kuihusianisha na vitu kama vile imani na ujuzi. Ulinganifu huo huonyesha kwamba roho takatifu si mtu.—Isaya 44:3; Matendo 6:5; 2 Wakorintho 6:6.
Ndugu si Kweli. Roho Mtakatifu ni halisi kabisa ni Person ama Mtu. Ndiye Mwalimu. Sio Pumzi wala Nguvu ama vyovyote unavyotaka kuelewa.
Inawezekana zile zinazoitwa Roho Saba za Mungu zikaendana na Theory yako. Lakini sio Kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni personality kamili atokaye kwa Baba na Mwana.
Sent using Jamii Forums mobile app
JE, YESU (AS) ANATHIBITISHA UFAHAMU WA ROHO MTAKATIFU?
Mungu kwa hekima na Rehema zake zisizo na kikomo, ameshatuma mitume mara kadhaa kusambaza UJUMBE Wake na kuwaita viumbe katika kufanya wema (yaani njia ya AMANI na UTIIFU kwa Mungu Mmoja wa Kweli). Huo Ujumbe unaitwa UISLAMU (kutii matakwa ya Mungu).
Ujumbe huu ulisambazwa kwa mataifa na makabila yote ulimwenguni kwa kufuatia mlolongo wa vizazi ukiwaita wanadamu kutii Matakwa ya Mungu. Hata hivyo, funuo zote za mwanzo zilibadilishwa na kupotoshwa na vizazi vilivyokuja baadaye, na mitume wakapuuzwa na kuteswa. Ufunuo safi wa Mungu umechafuliwa na maruweruwe, ushirikina, kuabudu masanamu na imani za kijinga. Kwa hiyo, dini ya Mungu ilipotezwa na kuingizwa katika mkondo wa ibada mbalimbali za uongo.
Historia ya nyendo za binadamu imekokotwa kati ya nuru na kiza. Mungu, kwa wingi wa Mapenzi na Rehema zake kwa wanadamu hajatuacha kizani tugundue njia ya haki kwa kujaribu na kukosea pekee. Amemtuma mjumbe wake wa mwisho, Mtume Muhammad (SAW) kuwaongoza binadamu katika kipindi kinachojulikana kuwa ni zama za kiza. Ufunuo, (yaani Quran Takatifu kwa kupitia malaika (Gabriel) Jibrilu) alioupokea Muhammad (SAW) unawakilisha chanzo cha msingi cha uongozi, chanzo chenye kukusanya mambo yote na cha maumbile ya dunia nzima. Mwongozo huu Mtakatifu unatoa muhtasari wa maarifa na hakika kuhusu Muumba Muweza, ulimwengu, lengo la kuumbwa kwetu na maisha yetu ya hapa duniani na Ahera. Ufunuo huo utawaongoza wanadamu kuelekea NJIA YA KWELI, WEMA na MAFANIKIO katika maisha haya na ya baadaye.
Kusema kuwa atakuja "mpatanishi /mshauri/ Mwombezi/ Roho wa kweli mwingine akiwa ni "mtume mwingine" kama vile Musa na Yesu (AS) ni sahihi kabisa. Ufahamu wa "Roho Mtakatifu" badala ya "mtume mwingine" umekanwa kikamilifu na Injili ya Yohana.
Ili kufahamu ujumbe wa Yesu (AS) juu ya maudhui hii, unatakiwa uanze na waraka wa kwanza wa (1 Yohana 2:1) Hapa, utamfahamu Yesu (AS) alikuwa ni "Mwombezi halisi", "Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,"
Yesu (AS) aliyekuwa "Mwombezi halisi" ameshatabiri kuja kwa "Mwombezi mwingine". Hata hivyo, ikirejewa Biblia kama ilivyotafsiri hilo neno "Mwombezi" kwa maneno mbalimbali ambayo msomaji anaweza kuyafikia kwa kutegemea nani aliyeandika Biblia, (yaani Msaidizi/ mpatanishi/ mshauri/ mwombezi/ Roho wa kweli/ Roho Mtakatifu).
Neno hilo hilo "Paraclete" linatumiwa katika Injili ya Yohana likiashiria utabiri wa Yesu (AS) kwa kuja kwa "Paraclete mwingine". Anasema: "Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;" (Yohana 14:16) Pia amewaambia wanafunzi wake kuwa huyo "msaidizi" atafundisha kila kitu na atawaletea kila kitu ili wakumbuke. Amesema katika (Yohana 15:26) "Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia."
Utaona katika mistari iliyopo hapo juu kuwa BIBLIA ya (RSV) imetumia neno "Counsellor" na neno hilo hilo limetajwa hapo juu (14:25) kuwa ni "Roho Mtakatifu". Lakini neno hilo hilo limebadilishwa katika (Yohana 15:26) hapo juu na kuwa ni "Roho wa kweli". Tena, katika aya zifuatazo hapa chini, imerejeshwa kwa "Counsellor" lakini utagundua baadaye kuwa neno hilo hilo kwa mara nyingine linarejeshwa kwa "Roho wa kweli" katika (Yohana 16:13).
(Yohana 16:7-8): "Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu." Hili limeshathibitishwa katika Quran pale Mungu alipomnyanyua Yesu (AS) na sio kusulubiwa kama ilivyodaiwa.
Katika aya ya hapo juu, (Yohana 16:7-8), kuja kwa "Counsellor" au "Paraclete" kunategemea kuondoka kwa Yesu (AS). Kando ya hayo, Yesu (AS) hajaashiria kuwa huyu "Mpatanishi" atakuja katika kipindi hiki.
Katika (Yohana 16:12-15), Yesu (AS) ameendeleza utabiri wake wa kuja kwa huyu Mpatanishi mwingine aliyemwita kuwa ni "Roho wa kweli". Anasema: "Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahamili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hata nena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari."
Aya ya hapo juu inavunja utata ulioundwa na neno Roho Mtakatifu [Holy Ghost] au Roho Mtakatifu [Holy Spirit] uliodaiwa na Wakristo kwa sababu, kwa mujibu wa Biblia katika (Mwanzo 1:2), huyu Roho Mtakatifu ameshakuwepo duniani tangu siku ya kuumbwa dunia.
"Huyo-Roho Mtakatifu" vilevile alikuwepo kule mto Jordan wakati Yohana alipombatiza Yesu (AS). Kwa hiyo, vipi Yesu (AS) aseme: "bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu." (Yohana 16:7).
Kile alichomaanisha Yesu (AS) ni kuwa "Msaidizi mwingine" au "Mtume mwingine" akiwa kama yeye atakuja kwa sababu kuletwa kwa Roho Mtakatifu kumeshafutiliwa mbali kabisa kwa kuwa huyo Roho Mtakatifu ameshakuwa hapa duniani tangu siku ya kuumbwa.
Zaidi, Roho Mtakatifu na Roho wa kweli hayo ni maneno mawili tofauti na kila moja linajitegemea kikamilifu. Hilo la mwisho limechukuwa kiwakilishi "he" nacho kinamaanisha yeye mwanamume, wakati ambapo ya kwanza (Roho Mtakatifu) inachukuwa kiwakilishi "it" nacho kinamaanisha hicho kitu. Yesu (AS) ametuambia kwa maneno ya sawasawa kuwa Counsellor au Roho wa kweli (paraclete) aliyemtabiri ni Mtu atakayetufundisha vitu vyote.
Viwakilishi vyote vya he vimerejea kwa "Roho wa kweli" jambo linalodhihirisha jinsi ya kiume ili liafikiane na neno "Counsellor" katika (Yohana 16:7). Hilo neno "Counsellor" ni neno kivumishi (descriptive - la kueleza sifa) linalotumika sehemu ya "Roho wa kweli", na kwa kisarufi (kigrama), kiwakilishi lazima kiafikiane kijinsia na jina linalofungamana nalo. Kwa hiyo, aya ya 13 na 15 ya Yohana 16 zinathibitisha kuwa Roho wa kweli si sehemu ya Utatu.[1]
Kando ya hayo, katika (Yohana 16:13) Yesu (AS) ametilia mkazo nukta inayomhusu huyu Roho wa kweli, kuwa ndiye mtume wa pekee atakayefundishwa cha kufanya kutoka kwa Aliye Juu: "Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hata nena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena," Kuwa ni mtume wa pekee (si Mungu wala Roho Mtakatifu), hatokuwa na mamlaka yake mwenyewe, bali atapewa ufunuo kutoka kwa Mungu huko Mbinguni.
[1] Victor Paul Wierwille: "Jesus Christ is not God", American Christian Press, the Way International, New Knoxville, Ohio 45871, p. 143.
Zaidi, utagundua kuwa katika (Yohana 16:14), Yesu (AS) anasema juu ya Roho wa kweli: "Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari." Quran, ambayo ni ujumbe wa Muhammad (SAW) umewatukuza wote wawili Yesu (AS) na mama yake Mariamu. Jina Isa [Yesu (AS)] limetajwa katika Quran Takatifu mara tano zaidi ya jina Muhammad. Na ukweli ni kuwa, sura kamili ya 19 ya Quran Takatifu bayana kabisa, imeitwa jina la mama yake Yesu ambaye ni Mariamu (yaani Surat Maryam), imethibitisha kiumbuji (utaalamu wa kueleza) hoja yetu kuwa, kwa hakika, Yesu (AS) ametukuzwa sana.
Kwa kuongezea, Yesu (AS), anasema: "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia." Hiyo ndio sababu kuwa ujumbe wa Muhammad (SAW) ambao ni Quran Takatifu ni ujumbe uliokamilika, unaojumuisha ujumbe wa Yesu (AS) na ujumbe wote uliotangulia. Kwa hakika, Quran ni kithibitisho cha ujumbe wa Yesu (AS) na wale wote waliokuja kabla yake. Huo ni ujumbe mpana unaokusanya mitazamo yote ya juhudi za wanadamu, sawa ni za kibinafsi, kijamii, kisiasa, kiuchumi au mahusiano ya kimataifa. Unaitwa UISLAMU (dini ya kutii Matakwa ya Mungu Mmoja wa Kweli – Allah) hiyo ni sheria kamili ya maisha, na vilevile ni ujumbe wa dunia nzima ulioelekezwa kwa wanadamu wote unaomwongoza mwanadamu kusuluhisha nafsi yake na Mungu Ujumbe ambao unaweza kuuita, Matakwa ya Mungu, matunda ya Uokovu.
Pia, katika (1 Waraka wa Yohana 4:6) maneno mawili "Roho wa kweli" na "Roho mwovu" yametumika kwa ajili ya mwanadamu. Na, katika MSS, Codex Syriacus ya zamani imegunduliwa mwaka 1812 katika Mlima Sinai na Bibi Agnes S. Lewis na Bibi Bensley, andiko la (Yohana 14:26), linalosomeka: "Paraclete, the Spirit" na sio "Paraclete, the Holy Spirit". Hilo neno "Roho" imerejeshwa na MSS, ya zamani, kwa "Roho wa kweli" katika (Yohana 15:26) ya Biblia za kisasa.
Mwisho, akisi kile alichokisema Mtume Isa - Yesu (AS), katika (Mathayo 21:43): "Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake."
Zingatia kuwa, onyo la Yesu (AS) kwa wayahudi pale walipokuwa waasi kwa kuamini na kuabudu miungu mingine kinyume na Mungu Muweza wa asili katika (Mwanzo 49:10) na Mtume Yakobo (AS) ameonya kuhusu Yuda. Kwa kweli ilikuwa ni kukamilisha utabiri wa awali katika (Kumbukumbu la Torati. 32:21): Mungu anasema: "Wamenitia wivu kwa kisicho cha Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo."
Warabu wa kabla ya Uislamu walikuwa wakielezwa na watu wa Magharibi kuwa ni taifa jinga. Mwandishi mmoja amewatolea taswira ya kuwa ni "wanyama wakiwa na ngozi ya mwanadamu", ndipo, pale walipoletewa Uislamu, wakawa ni kiigizo cha wanadamu. Mtume Muhammad (SAW) ameondosha aina zote za kuabudu masanamu na kuhubiri upweke wa Mungu – Muumba. Yeye peke yake ndiye Mungu, Mlezi na Mpaji wa ulimwengu wote Asiye na Mke, Mwenza, Mshirika, Familia, mtoto wala msaidizi. Taifa la Kiarabu kwa ujumla na mtume Muhammad (SAW) kwa kipekee walikuwa ni ukamilisho wa tabiri zote za hapo juu.