Wale vijana wa kataa ndoa wana haki ya kusema ndoa sio lazima kwa sababu hata Biblia Takatifu inasema kama hujaoa ama kuolewa ama mjane, basi usijaribu kabisa kuingia kwenye ndoa.
Wakorintho 1, Sura ya 7: 8-9 Mtume Paulo anasema ndoa iwe ni last option baada ya kua umeshindwa kabisa na huna namna ya kuishi lakini yeye binafsi kwa maono yake makubwa aliyovuviwa na roho mtakatifu anashauri watu wasioe wala kuolewa.
Hoja ya Mtume Paulo ni moja, kwamba kama unaweza kupata maziwa huna sababu ya kulazimika kununua ng'ombe mzima ufuge zizini kwako. Nunua ng'ombe tu pale huna namna ya kupata maziwa.
Mtume Paulo anaenda mbali zaidi mstari wa 27-29 anasema kama umeoa basi hakuna kumpa mke talaka lakini kama hujaoa basi usijaribu hata kidogo kutafta mke. Paulo anasisitiza kwamba kuoa ni kujutaftia matatizo makubwa sana bora usioe. Mtume anasema wanao oa wanakabiliwa na matatizo makubwa sana maishani mwao.
Kama biblia inaonya kwamba kuoa ni kujitaftia matatizo, why uoe?