Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mtumishi wa Serikali aliyechana Quraan Tukufu asimamishwa kazi, Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo.

RPC Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Maleki, kwa kosa la kuchana na kuchoma moto kitabu cha Juzuu Amma ambacho ni sehemu ya Quran Tukufu.

“Maleki ni Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, alionekana akichana na kuchoma kitabu hicho Kitakatifu cha dini ya Kiislamu, kitendo ambacho kiliwakasirisha Waumini wa dini hiyo na wananchi waliokuwa maeneo hayo na kuamua kutoa taarifa kwa Polisi” RPC Mutafungwa.

Muheshimiwa Jafo amesema, Mtumishi huyo yuko chini ya ofisi ya Rais na jambo alilofanya halileti afya kwa jamii. Muheshimiwa Jafo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa kumsimamisha kazi mtumishi huyo pia afanye uchunguzi na kamati au mamlaka yake ya nidhamu iweze kuchukua hatua kadiri atakavyoona inafaa mara baada ya uchunguzi huo



MUTAFUNGWA.jpeg
MUTAFUNGWA 2.JPG
 
Oooooh My god!! amechana heshima yake na amechana karatasi yenye maandishiya Qurani. Hiyo ni Provocation isiyo na tija! QURAAN ipo ndani ya mioyo ya Waumini na haitoweza kunyakuliwa au kuchanwa! Tunapo hifadhi Quraan tunaiweka kifuani na kuitumikia. Waisalm tuwe wavumilivu na tuondoe jazba!

Uhuni huu wa uchokozi haukuanza leo.... walishindwa wengi miaka 1441 iliyopita
Tumemsamehe aalipwa na mwenye msahafu.
 
Back
Top Bottom