Mtungi wa gesi uoneshe kilichopo ndani kama chupa ya soda.

Mtungi wa gesi uoneshe kilichopo ndani kama chupa ya soda.

TzComedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2017
Posts
890
Reaction score
700
Hakuna kulemba, ngoja nende kwenye point directly.

Ni wangapi kati yetu tunaofaamu kiasi cha pesa tunacholipa kwa ajili ya manunuzi ya gase ya matumizi ya nyumbani kinaendana na ujazo halisi haliyakuwa baadhi yetu mara nyingi tumekuwa tu wapiga simu ili tuletewe ujazo wa gase unaofanana na mtungi ulioisha?.

Aidha ni wangapi wenye Mizani kwa ajili ya kupima mtungi wenye ujazo lengwa mara tu uletewapo na mletaji (mfanya biashara) huyo?.

Maoni yangu, ni vema sasa nyie wafanya biashara mtuletee mitungi ionekanayo hadi ndani kama chupa ya soda au konyagi ili kutuondolea wasisi wa kuuziwa Mbuzi kwenye gunia(kuchakachuliwa).

Ahsanten.
 
Hivi wewe unawaeza kuona gesi? Nadhani hukusoma kemia, na kama ulisoma utagundua kuwa gesi nyingi zina 'the following physical properties'... They are color less, test less and in most cases odor less...
KUMEKUCHA NILIJUA TU HUYU MZEE HAJUI KAMA GESI HAIJUI HAINA RANGI.ILA NIMEMUOGOPA KWANI AKITAKA KILA KITU KIWE KINAONEKANA ILI ASIIBIWE.MKE WAKE ATAWEKEA MITA AU GEJI KUPIMA MATUMIZI YA PAPUCHI
 
KUMEKUCHA NILIJUA TU HUYU MZEE HAJUI KAMA GESI HAIJUI HAINA RANGI.ILA NIMEMUOGOPA KWANI AKITAKA KILA KITU KIWE KINAONEKANA ILI ASIIBIWE.MKE WAKE ATAWEKEA MITA AU GEJI KUPIMA MATUMIZI YA PAPUCHI
Kama inawezekana kuchangia kwa sitara, inashindikana nini kufanya hvo? Najua tuna malezi tofauti, basi kupitia jf ni vema tukajifunza kwa wale wenye malezi safi.
 
Mbna inaezekana tu kuifanya tuone kilichopo ndani teknologia sa hv ipo juu Sana sema hawajaamua
 
Rahisi sana, inua mtungi wako wa gesi utikise taratibu utaweza gundua ujazo wa gesi ulipo ndani ya mtugi.
 
Kama inawezekana kuchangia kwa sitara, inashindikana nini kufanya hvo? Najua tuna malezi tofauti, basi kupitia jf ni vema tukajifunza kwa wale wenye malezi safi.
Mbona unalia lia mkuu,
Muhudumu ongeza pombe apa Kaunta, naona Magufuli anatunyoosha sana
 
Hivi wewe unawaeza kuona gesi? Nadhani hukusoma kemia, na kama ulisoma utagundua kuwa gesi nyingi zina 'the following physical properties'... They are color less, test less and in most cases odor less...
Wewe ni kati ya wakemia bomu kama yule jamaa yetu. Nani kakuambia kitu kikiwa colourless hakionekani?

Hebu tizama maji ya Kilimanjaro kwenye chupa uone kama hutayaona kwa kuwa ni colourless. Pili vitu vinavyoitwa si kwamba havina rangi Ila rangi yake hubadilika kutokana na reflection ya mahali kilipo.

Ni vema pia kufahamu gesi za kupikia zote zina harufu kutegemeana na source ( Odor). Do your homework. Mleta mada kafikiri nje ya box.
 
Mbna inaezekana tu kuifanya tuone kilichopo ndani teknologia sa hv ipo juu Sana sema hawajaamua
Kina nani hawajaamua mkuu...mbona unajitoa wewe kwenye kuamua (kwa maana nyingine inawezekana pia hakuna hiyo teknolojia kwa kuwa unawategemea wengine waamue)
 
If can't change don't blame others why they not change it
 
Wangeweka kifaa cha kujulisha kama gesi imekaribia kuishaa
vifaa kujua kama gesi imekaribia kuisha vipo // mtungi hauwezi kuwa kama chupa ya soda sababu za kiusalama maana kama ikitokea umepasuka bahati mbaya imagine kweye lori limesheheni mitungi huo moto wake ni hatari sana // kumaliza tatizo ni vyema ukapimiwa gesi yako kila ununuapo wapo wauza gesi wengi tuu wanalijua hilo na wanaweka mizani kwenye maduka yao //

angalizo langu ni kwamba hakikisha unakagua mtungi wako vyema ununuapo kama umechoka sana unaweza kuwa na hatari za leakage, // pia hakikisha umepimiwa vizuri mtungi wako kabla ya kulipia na kuubeba kwaajili ya matumizi //
umakini wako ndio usalama wako
 
Kama inawezekana kuchangia kwa sitara, inashindikana nini kufanya hvo? Najua tuna malezi tofauti, basi kupitia jf ni vema tukajifunza kwa wale wenye malezi safi.
mkuu kama una buku karibu hapo nikupe jero na offa juu
 
Hili likitoke hapa kwetu, Itakuwa ugunduzi utakao tuweka WaTz katika safu ya wana sayansi.
 
Back
Top Bottom