Mtungie shairi lenye ubeti mmoja au zaidi mwanadada umpendaye hapa JF

haliihitaji hirizi,naomba sana welewe
nikumbatie mpenzi,usi hofu wenginewe
wabaki na simulizi,watuige wapagawa
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,mwandani wangu ujuwe
niote katika njozi,ulalapo niko nawe
mimi kwako ndio dozi,ukiumwa upatiwe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,wala usijisumbuwe
watakupiga fitizi,wataka wakuganguwe
hao wote ni walozi,nimekupenda mwenyewe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


halihitaji hirizi,nimekupenda mwenyewe
sitaki masimulizi,,juu yako niambiwe
kwa hila za kibazazi,kwangu zitangonga jiwe
pendo langu mimi nawe halihitaji hirizi


Kwako popote ulipo !,
 

Hii kweli imenoga.

Na ili kutukomesha ukatunga shairi zima.

Nakupa 'A'
 
we ndo pozo la moyo wangu usije nitenda
ukanifanya ikala kwangu, mapenzi.yakaenda,wewe ni wangu, i need you, wewe ni wangu i love you
najua umeniridhia, tunza chako kiapo
give me baby...i give it to you
 
Gogle Siku hizi hauji na zile nyuzi zako nishakugaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…