Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MTWA ABDALLAH MKWAWA (1865 - 1898)
Nimefika leo asubuhi Kalenga nikielekea alipokuwa anaishi Mtwa Mkwawa ambapo hapo ilipokuwa nyumba yake sasa ni Mkwawa Museum.
Ukisimama barabarani na kuangalia nyumba zilizopo hapo na watu wakifanya biashara zao ndogo ndogo ni tabu kujijengea picha akilini mwako kuwa kijiji hicho kimebeba jina la kiongozi hodari na shujaa aliyepigana na Wajerumani na kuwashinda katika vita vilivyopiganwa Lugalo ambako Emil von Zelewski kamanda wa Kijerumani aliuawa.
Huyu Zelewiski alikuwa mtu mwenye kibri sana na anakumbukwa na watu wa Pangani kwa kuingiza mbwa msikitini siku ya Iddi Kubwa.
Msikiti huu ungalipo hadi leo mimi niliuona kwa mara ya kwanza Pangani mwaka wa 2003 nilipokuwa na Dr. Harith Ghassany katika utafiti wa kitabu chake, 'Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."
Historia ya Chief Mkwawa haihitaji maelezo.
Hii ni historia maarufu sana kupitia kiasi.
Lakini katika historia hii yapo mengi muhimu ambayo hayafahamiki kabisa kwa watu wengi.
Katika hayo mengi makubwa ambayo hayafahamiki mojawapo ni kuwa Mkwawa alikuwa Muislam na alijua kusoma na kuandika kwa hirabu za Kiarabu.
Nani Mwalimu wake aliyemfunza kusoma na kuandika na lini alisilimu?
Mwalimu wa Mtwa Mkwawa alikuwa Abushiri bin Salim Suriyama aliyekuwa mfanya biashara kutoka Pangani ambae alikuwa akifanya biashara na Mkwawa na watu wake.
Hii Suriyama inaweza ikawababaisha watu kwa kuuliza huyu Abushiri bin Salim Suriyama ni yupi.
Huyu ni Abushiri bin Salim Al Harith mtu maarufu katika vita dhidi ya Wajerumani.
Abushiri in Salim ndiye aliyemsilimisha Mkwawa na jina alilochagua Mtwa ni Abdallah.
Angalia hapo chini barua ya Mtwa Abdallah Mkwawa aliyoandika kwa mkono wake mwenyewe.
Abushiri alimletea Mtwa Mkwawa bunduki kama zawadi na bunduki hiyo ipo hapo Mkwawa Museum.
Kutokana na bunduki hii Mkwawa kwa mikono yake mwenyewe alitengeneza gobole ambalo lipo hapo pia limehifadhiwa.
Bunduki aliyopewa na rafiki yake Abushiri bin Salim Suriyama ndiyo Mkwawa aliyoitumia kujiua mwaka wa 1898.
Hiyo picha hapo chini ya kichuguu ni mahali Mkwawa alikuwa akisimama kuwahutubia watu wake.
Wakati ule kilikuwa kichuguu kirefu lakini jinsi miaka inavyokwenda kimekuwa kikipungua kwa kupigwa na mvua na sasa kimekuwa kifupi.