Mtwa Abdallah Mkwawa

Mtwa Abdallah Mkwawa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MTWA ABDALLAH MKWAWA (1865 - 1898)

Nimefika leo asubuhi Kalenga nikielekea alipokuwa anaishi Mtwa Mkwawa ambapo hapo ilipokuwa nyumba yake sasa ni Mkwawa Museum.

Ukisimama barabarani na kuangalia nyumba zilizopo hapo na watu wakifanya biashara zao ndogo ndogo ni tabu kujijengea picha akilini mwako kuwa kijiji hicho kimebeba jina la kiongozi hodari na shujaa aliyepigana na Wajerumani na kuwashinda katika vita vilivyopiganwa Lugalo ambako Emil von Zelewski kamanda wa Kijerumani aliuawa.

Huyu Zelewiski alikuwa mtu mwenye kibri sana na anakumbukwa na watu wa Pangani kwa kuingiza mbwa msikitini siku ya Iddi Kubwa.

Msikiti huu ungalipo hadi leo mimi niliuona kwa mara ya kwanza Pangani mwaka wa 2003 nilipokuwa na Dr. Harith Ghassany katika utafiti wa kitabu chake, 'Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."

Historia ya Chief Mkwawa haihitaji maelezo.

Hii ni historia maarufu sana kupitia kiasi.

Lakini katika historia hii yapo mengi muhimu ambayo hayafahamiki kabisa kwa watu wengi.

Katika hayo mengi makubwa ambayo hayafahamiki mojawapo ni kuwa Mkwawa alikuwa Muislam na alijua kusoma na kuandika kwa hirabu za Kiarabu.

Nani Mwalimu wake aliyemfunza kusoma na kuandika na lini alisilimu?

Mwalimu wa Mtwa Mkwawa alikuwa Abushiri bin Salim Suriyama aliyekuwa mfanya biashara kutoka Pangani ambae alikuwa akifanya biashara na Mkwawa na watu wake.

Hii Suriyama inaweza ikawababaisha watu kwa kuuliza huyu Abushiri bin Salim Suriyama ni yupi.

Huyu ni Abushiri bin Salim Al Harith mtu maarufu katika vita dhidi ya Wajerumani.

Abushiri in Salim ndiye aliyemsilimisha Mkwawa na jina alilochagua Mtwa ni Abdallah.

Angalia hapo chini barua ya Mtwa Abdallah Mkwawa aliyoandika kwa mkono wake mwenyewe.

Abushiri alimletea Mtwa Mkwawa bunduki kama zawadi na bunduki hiyo ipo hapo Mkwawa Museum.

Kutokana na bunduki hii Mkwawa kwa mikono yake mwenyewe alitengeneza gobole ambalo lipo hapo pia limehifadhiwa.

Bunduki aliyopewa na rafiki yake Abushiri bin Salim Suriyama ndiyo Mkwawa aliyoitumia kujiua mwaka wa 1898.

Hiyo picha hapo chini ya kichuguu ni mahali Mkwawa alikuwa akisimama kuwahutubia watu wake.

Wakati ule kilikuwa kichuguu kirefu lakini jinsi miaka inavyokwenda kimekuwa kikipungua kwa kupigwa na mvua na sasa kimekuwa kifupi.

1656451543941.png
1656451686287.png
1656451923158.jpeg
 
Historia na wahehe kwa ujumla inamtambua mkwawa kama mkwawa jina orijino la kinyalukolo, hayo majina ya Abdallah hatujawahi kuyasikia, huenda yalitumika kwenye biashara tu baina yake mtwa na waarabu.

Pia tusipende kuchanganya lugha ya kiarabu na uislamu, lugha ni lugha na imani ni imani. kuna waarabu wengi tu wakristo, wasio na dini na wengine wachawi wanatumia lugha ya kiarabu fresh tu ..

Yaani chifu kama mkwawa aache imani yake ya kuabudu mizimu ya babu zake na kutambika akubali tu kupokea dini mpya kirahisi rahisu tu ? 😂😂 hio danganya toto peleka chekechea aisee.... Mnachukulia mambo poa sana haya, Acheni kumvunjia heshima Mtwa Mkwawa, haya ni matusi.

Halafu naskia hapo Iringa kuna waarabu wamejipa jina mkwawa, sijui ilikuwaje.

Namuona hata huyu dogo alierithi kiti ni kama mtu wa pwani huko, kakomba vingi kwa mama yake, yaani hata dada zake ni kama mashombe shombe hivi.

kiufupi ni kama vile kizazi cha mkwawa kimepoteza uasilia, kimekuwa diluted mno.
 
..huenda Mtwa Mkwawa alikuwa akifanya biashara ya Watumwa na Pembe za ndovu.
 
1. Kichuguu sikioni mkuu au bado inaendelea?

2. Tusichokijua ni kusilimu peke yake au utaongezea?

3. Dini ilikuwa na nafasi gani katika ushujaa wake tofauti na angekua na dini nyingine?
Glenn,
Usiniulize maswali mimi namuhadithia Mtwa Abdallah Mkwawa kwa yale ambayo hayafahamiki.

Sijasema kuwa Uislam wake ndiyo uliomtia ushujaa kwani alikuwa shujaa hata kabla hajasilimu.

Ikibidi nitaongeza.
Akili ya binadamu haikuumbwa kutuwama.

Angalia mfano wa Mtwa Mkwawa.

Alipopewa bunduki na Abushiri akatumia bunduki ile kutengeneza gobole ili asitegemee silaha za kununua kutoka kwa wengine.

Ningependa sana uone gobole alilotengeneza Mkwawa ushuhudie wewe mwenyewe kiasi chake cha uwezo wa ufundi alichokuwa nacho.

Aligundua chuma katika himaya yake na akawa anatumia chuma kutengeneza visu, majembe na vitu vingine.

Ingia hapa utakiona kichuguu:

Historia na wahehe kwa ujumla inamtambua mkwawa kama mkwawa jina orijino la kinyalukolo, hayo majina ya Abdallah hatujawahi kuyasikia, huenda yalitumika kwenye biashara tu baina yake mtwa na waarabu.

Pia tusipende kuchanganya lugha ya kiarabu na uislamu, lugha ni lugha na imani ni imani. kuna waarabu wengi tu wakristo, wasio na dini na wengine wachawi wanatumia lugha ya kiarabu fresh tu ..

Yaani chifu kama mkwawa aache imani yake ya kuabudu mizimu ya babu zake na kutambika akubali tu kupokea dini mpya kirahisi rahisu tu ? [emoji23][emoji23] hio danganya toto peleka chekechea aisee.... Mnachukulia mambo poa sana haya, Acheni kumvunjia heshima Mtwa Mkwawa, haya ni matusi.

Halafu naskia hapo Iringa kuna waarabu wamejipa jina mkwawa, sijui ilikuwaje.

Namuona hata huyu dogo alierithi kiti ni kama mtu wa pwani huko, kakomba vingi kwa mama yake, yaani hata dada zake ni kama mashombe shombe hivi.

kiufupi ni kama vile kizazi cha mkwawa kimepoteza uasilia, kimekuwa diluted mno.
Sky...
Una haki na fikra zako.

Ninachokusihi ni lugha ya staha ili mjadala uwe wa adabu.

Historia iliyoko hatukuiandika sisi hii ni nafasi yetu na sisi kujadili historia ya wazee wetu.
 
Siyo huenda, ni fact Mkwawa alikuwa anapiga dili za meno ya tembo na kina Abushiri kwa exchange ya mashuka meupe fedha na vitu mbalimbali na hata bunduki.

Usitegemee Mzee Mohamed Said aliandike hili.

Alikuwa akifanya biashara gani.

A. Pembe za ndovu tu.

B. Watumwa tu.

C.Pembe za ndovu na watumwa.

D. Hakuwa akifanya biashara ya Pembe za ndovu, wala watumwa.
 
1. Kichuguu sikioni mkuu au bado inaendelea?

2. Tusichokijua ni kusilimu peke yake au utaongezea?

3. Dini ilikuwa na nafasi gani katika ushujaa wake tofauti na angekua na dini nyingine?
  1. Mimi sijaona bunduki na gobore
  2. Ningetamani kuona tafsiri ya hayo maandishi ya kiarabu
 
Siyo huenda, ni fact Mkwawa alikuwa anapiga dili za meno ya tembo na kina Abushiri kwa exchange ya mashuka meupe fedha na vitu mbalimbali na hata bunduki.

Usitegemee Mzee Mohamed Said aliandike hili.
Matola,
Si lazima mimi ndiye niandike.
Hata wewe unaweza kuandika.

Mimi nimekuandikieni yale yote niliyojifunza Mkwawa Museum Kalenga.

Bahati mbaya historia ya Mkwawa imewavunja moyo baadhi yenu.

In Shaa Allah nitakuelezeni historia ya urafiki wa Mkwawa na Muhammad bin Khalfani Khamis ambae anajulikana kwa jina la Rumaliza.
 
Historia na wahehe kwa ujumla inamtambua mkwawa kama mkwawa jina orijino la kinyalukolo, hayo majina ya Abdallah hatujawahi kuyasikia, huenda yalitumika kwenye biashara tu baina yake mtwa na waarabu.

Pia tusipende kuchanganya lugha ya kiarabu na uislamu, lugha ni lugha na imani ni imani. kuna waarabu wengi tu wakristo, wasio na dini na wengine wachawi wanatumia lugha ya kiarabu fresh tu ..

Yaani chifu kama mkwawa aache imani yake ya kuabudu mizimu ya babu zake na kutambika akubali tu kupokea dini mpya kirahisi rahisu tu ? [emoji23][emoji23] hio danganya toto peleka chekechea aisee.... Mnachukulia mambo poa sana haya, Acheni kumvunjia heshima Mtwa Mkwawa, haya ni matusi.

Halafu naskia hapo Iringa kuna waarabu wamejipa jina mkwawa, sijui ilikuwaje.

Namuona hata huyu dogo alierithi kiti ni kama mtu wa pwani huko, kakomba vingi kwa mama yake, yaani hata dada zake ni kama mashombe shombe hivi.

kiufupi ni kama vile kizazi cha mkwawa kimepoteza uasilia, kimekuwa diluted mno.
Mkuu umeongea ukweli mtupu kumlink Mkwawa na Uislam ni matusi kwa jamii ya Kihehe na hilo jambo sio kweli hata kwenye matambiko ya kimila huwezi kusikia habari sijui ya Abdala huu ni Wuudesi va kwivala nye vayawe
 
Dudu...
Mimi si niliyesema kuwa Mkwawa alisilimu na kuwa Muislam na aliyemsilimisha ni Abushiri bin Salim.
Historia hii iko Mkwawa Museum.

Ukifika pale utayakuta haya pamoja na barua ambazo yeye mwenyewe kaandika kwa herufi za Kiarabu.
Hapana haja ya kuchukia kwani hiyo ni sehemu ya historia yake.

Halikadhalika nimeonyeshwa sehemu za matambiko ya Mkwawa na nimepata maelezo ya kina na nimepiga picha sehemu zote hizo.

Labda suala linalohitaji utafiti zaidi ni kwa nini matambiko yamerudi nyuma na Uislam ukasonga mbele.

Kutokana na huu Uislam wa Mkwawa ndiyo ikawa mwanae Sapi akawa Muislam na Uislam ukaendelea katika ukoo huo hadi leo.

Ukifanya utafiti utaona kuwa Manispaa ya Iringa kuna misikiti 25 na yote inasaliwa Ijumaa.
Mkoa mzima una zaidi ya misikiti 80.

Msikiti wa zamani sana Iringa ni msikiti wa Miyomboni huo hapo chini:

1657397474434.png
 
Pamoja na kwamba mambo ya dini zote hua sipo kwa nini inaonekana uislamu wa mkwawa unawaumiza watu? Ukweli ni kwamba mkwawa alikua muislamu na wapigania uhuru wengi Tanganyika huwezi watenga na uislam anzia TAA Na TANU wazee wa ujiji, Tabora, Tanga, Pwani hadi Dar alipopokelewa mwalimu na hao hao waislamu na wakamwamini kumpa madaraka, sio kwa sababu alisoma kuliko wao la hasha, waliamua tu kumpa na nadhani baada ya kuona ni kijana na ataongoza muda mrefu ukiacha wakristo akina japhet kirilo na akina marialle ambao walitaka wao nchi yao iwe kaskazini na wapate uhuru wao huku wakiwaacha wenzao wa Tanganyika waendelee kutawaliwa miaka yote kipi kipya? Hakipo
 
Chotera,
Kuna historia ya mazungumzo kati ya Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe yaliyofanyika nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe mwaka wa 1953.

Mazungumzo yalihusu uchaguzi wa TAA mwaka huo na kumtia Nyerere katika uongozi wa TAA.

Wagombea walikuwa wawili.
Abdul Sykes na Julius Nyerere.

Abdul achukue uongozi kutoka Secretary na Act. President wa TAA au ampishe Nyerere?

Hamza Mwapachu alishauri kuwa Abdul amwachie nafasi ile Nyerere na 1954 waunde TANU.

Sababu aliyotoa Mwapachu ni kuwa Nyerere ni Mkristo akiwa kiongozi itawavuta Wakristo kuunga mkono harakati za uhuru.

Wakati ule Waislam ndiyo walikuwa mbele katika TAA na Mwapachu alihofu harakati zisionekane ni za Waislam peke yao kudai uhuru.
 
Pamoja na kwamba mambo ya dini zote hua sipo kwa nini inaonekana uislamu wa mkwawa unawaumiza watu? Ukweli ni kwamba mkwawa alikua muislamu na wapigania uhuru wengi Tanganyika huwezi watenga na uislam anzia TAA Na TANU wazee wa ujiji, Tabora, Tanga, Pwani hadi Dar alipopokelewa mwalimu na hao hao waislamu na wakamwamini kumpa madaraka, sio kwa sababu alisoma kuliko wao la hasha, waliamua tu kumpa na nadhani baada ya kuona ni kijana na ataongoza muda mrefu ukiacha wakristo akina japhet kirilo na akina marialle ambao walitaka wao nchi yao iwe kaskazini na wapate uhuru wao huku wakiwaacha wenzao wa Tanganyika waendelee kutawaliwa miaka yote kipi kipya? Hakipo

..madai kwamba Marealle alitaka uhuru wa Wachaga peke yao sio za kweli.

..ushahidi ulioko ktk nyaraka za UN unaonyesha kwamba Marealle alidai uhuru wa Watanganyika wote bila kubagua.
 
Naomba hizo nyaraka,
 
Back
Top Bottom