Naomba hizo nyaraka,
..Unaahidi nini nikikuonyesha?
..Je, utakuwa tayari kuanzisha post kukiri kwamba Marealle alidai uhuru wa Watanganyika wote?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba hizo nyaraka,
Naomba hizo nyaraka,
Mashine...
- Mimi sijaona bunduki na gobore
- Ningetamani kuona tafsiri ya hayo maandishi ya kiarabu
Bhika...Mi nadhani ilipaswa kuandikwa kuwa:
Rifle gun which Abushir bin Salim Suriyama gifted Chief Mkwawa......
Badala ya:
Rifle gun was Abushir bin Salim Suriyama gifted Chief Mkwawa...…
Naomba wanaohusika na makumbusho hayo warekebishe hiyo 'grammatical error' na umakini uwepo katika kuhakiki/ kuhariri maandishi kabla ya kubandikwa mahali ili kuepusha fedheha kwa taifa jamani.View attachment 2317535
Mtwa...Mkwawa na famili yake alikuwa Muislamu ni Sawa... Ila jamii ya uhehe haikuipokea hiyo dini asilani. Kumuita mkwawa Abdalah ni dharau ambayo wahehe wote duniani tunailaaaaani
Kinachokera ni watu kupinga facts Kwa sababu haiwapendezi..Pamoja na kwamba mambo ya dini zote hua sipo kwa nini inaonekana uislamu wa mkwawa unawaumiza watu? Ukweli ni kwamba mkwawa alikua muislamu na wapigania uhuru wengi Tanganyika huwezi watenga na uislam anzia TAA Na TANU wazee wa ujiji, Tabora, Tanga, Pwani hadi Dar alipopokelewa mwalimu na hao hao waislamu na wakamwamini kumpa madaraka, sio kwa sababu alisoma kuliko wao la hasha, waliamua tu kumpa na nadhani baada ya kuona ni kijana na ataongoza muda mrefu ukiacha wakristo akina japhet kirilo na akina marialle ambao walitaka wao nchi yao iwe kaskazini na wapate uhuru wao huku wakiwaacha wenzao wa Tanganyika waendelee kutawaliwa miaka yote kipi kipya? Hakipo
Hongera Kwa kukili Jambo mojaMkwawa na famili yake alikuwa Muislamu ni Sawa... Ila jamii ya uhehe haikuipokea hiyo dini asilani. Kumuita mkwawa Abdalah ni dharau ambayo wahehe wote duniani tunailaaaaani
Historia na wahehe kwa ujumla inamtambua mkwawa kama mkwawa jina orijino la kinyalukolo, hayo majina ya Abdallah hatujawahi kuyasikia, huenda yalitumika kwenye biashara tu baina yake mtwa na waarabu.
Pia tusipende kuchanganya lugha ya kiarabu na uislamu, lugha ni lugha na imani ni imani. kuna waarabu wengi tu wakristo, wasio na dini na wengine wachawi wanatumia lugha ya kiarabu fresh tu ..
Yaani chifu kama mkwawa aache imani yake ya kuabudu mizimu ya babu zake na kutambika akubali tu kupokea dini mpya kirahisi rahisu tu ? 😂😂 hio danganya toto peleka chekechea aisee.... Mnachukulia mambo poa sana haya, Acheni kumvunjia heshima Mtwa Mkwawa, haya ni matusi.
Halafu naskia hapo Iringa kuna waarabu wamejipa jina mkwawa, sijui ilikuwaje.
Namuona hata huyu dogo alierithi kiti ni kama mtu wa pwani huko, kakomba vingi kwa mama yake, yaani hata dada zake ni kama mashombe shombe hivi.
kiufupi ni kama vile kizazi cha mkwawa kimepoteza uasilia, kimekuwa diluted mno.
Mwana...Huyo ni Mohammed Said bwana. Yeye ajenda yake kuu ni kutukuza Uislam. Historia zake zote anazoandika ajenda kuu ni kutukuza Uislam, sio kuelimisha au kuandika historia kwa ukamilifu.
Mwana...
Umesema kweli kabisa agenda yangu kuu ni Uislam.
Hii inatokana na ukoloni kuandika historia kwa maslahi yao.
Hili halikukoma baada ya uhuru na ndiyo nikanyanyua kalamu na kuandika historia ya kweli.
Uislam historia yake Tanganyika yenyewe ukiisoma utaona utukufu wake katika kupamba na ukoloni kuanzia Vita Vya Maji Maji hadi katika siasa za utaifa baada ya Vita Kuu Vya Pili.
Ikiwa kuna mahali nimekosea katika kuiandika historia hii uko huru kunisahihisha.
Jina la Abdallah ni jina alilochagua Mtwa Mkwawa baada ya kutoa shahada na aliyemtamkisha ni Abushiri bin Salim wa Pangani.
Lakini Mkwawa siku zote atabakia kuwa Mkwawa kuwa alichukua jina la Abdallah alipoingia Uislam hakubadilishi chochote katika utambulisho wa Mtwa.
Abdallah litabakia kama moja ya majina yake pamoja na jina la Mkwawa.
Mwana...Huo ni utumwa wa akili.
Dini za Uislam na Ukristo hazikuletwa kwetu watu weusi kwa nia njema. Zililetwa kama dawa ya kutupumbaza ili kuwasaidia waliozileta kututawala na kufanikisha mambo yao.
Vita kati ya Mwarabu na Mzungu sio vita yetu waafrika. Kwa hiyo kama Uislam ulikuwa ndo ajenda kuu katika vita vya majimaji basi hiyo ilikuwa ni vita ya waarabu dhidi ya wazungu. Maana wazungu nao walikuja kututawala ila wakamkuta Mwarabu amewatangulia.
Sasa kwa wewe mtu mweusi kutukuza Uislam (au mtu mweusi mwingine kutukuza Ukristo) wote ni utumwa wa akili tu.
Wazee wetu hawakuwa na taarifa za kutosha kuwachambua hao wageni wa kutoka Arabuni, Uajemi na Ulaya. Sidhani kama huo Uislam unaotaka kuwapandikizia ni kama unavyouona wewe ambaye umezaliwa katika Uislam na pengine hata kuusomea.
Wazee wetu walikuwa kama Mangungo aliyesaini kuuza himaya yake kwa Mjerumani bila ya kujua.
Badee...Wewe ni Taa kwayo tunapata Mwanga, na Nguvu hauna ila Mwenyeezi Mungu anakuwezesha. Historia yko kila nikiipitia nianza kuifuatilia naikuta iko vilevle unavyoieleza. May God keep U survive mzee Mohqmmed Said. We love you
Mkuu umeongea ukweli mtupu kumlink Mkwawa na Uislam ni matusi kwa jamii ya Kihehe na hilo jambo sio kweli hata kwenye matambiko ya kimila huwezi kusikia habari sijui ya Abdala huu ni Wuudesi va kwivala nye vayawe