Mtwa Mkwawa hakuwa muhehe

Mtwa Mkwawa hakuwa muhehe

kimpe

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
911
Reaction score
862

1). Mtwa Mkwawa hakuwa mhehe na wala hakuwa mtoto wa Mnyigumba (kama historia iliyoandikwa na Wajerumani inavyopotosha); bali Mkwawa alikuwa ni mtoto wa dada wa Mnyigumba aliyeolewa na mtemi wa Waluguru; hivyo Mkwawa alikuwa Mluguru kwa asili.

Akiwa mdogo alikwenda kumtembelea mjomba wake (Mnyigumba) na kutokana na ushujaa wa Mkwawa akafanikiwa kumuokoa mjomba wake katika vita kali dhidi ya Wangoni pale Makambako. Mnyigumba akampenda Mkwawa kuliko watoto wake, na ndio chanzo cha kupewa urithi pamoja na mtoto wa Mnyigumba aliyeitwa Muhenga.

2). Sherehe za kuapishwa Mtwa Mkwawa zilifanyika Dodoma eneo linaloitwa Mpwapwa. Sherehe zilihudhuriwa na wajomba zake Mtemi Mazengo, Kimweri, Lugulu na Mirambo; ambapo walikuwa wakiimba "Mpwa! Mpwa!" na ndipo neno Mpwapwa likazaliwa.

3) Mtwa Mkwawa alikua na vikosi vinne vya majeshi ya vita; kimojawapo kilikuwa cha upelelezi na ushambuliaji [Kiitwacho Vamalavanu] ambacho kilikuwa kikila nyama ya mbwa ikichanganywa na dawa ya tambiko; wakiamini kuwa watakuwa na uwezo wa kunusa maadui na wao kutoonekana. Hivi ndivyo ulaji nyama ya mbwa ulivyoanza.

4). Mtwa Mkwawa alijua kusoma na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiarabu na alikuwa muumini wa dini ya Kiislamu.

5). Mtwa Mkwawa hakujipiga risasi bali alijitumbukiza katika daraja la Kikongoma (lililopo mto Ruaha) mahali ambapo mama yake mzazi pia alijitumbukiza na kujiua pale. Lile fuvu linalodaiwa kuwa la Mtwa Mkwawa inadaiwa ni la mlinzi wake. Hadi leo hakujawahi kufanyika DNA tests kuthibitisha fuvu hilo.

6). Kwenye vita iliyomsambaratisha Mtwa Mkwawa, Wajerumani walifanikiwa kumkamata mdogo wa Mkwawa aliyeitwa Mpangile, walimtundika kitanzini-hakufa, wakampiga risasi-hakufa! Baadae akatoboa siri kuwa wammwagie maji na wamchome mkuki-ndipo akafa! Baada ya kuona hivyo wakampa jina "Mpangelwangindo Mgopisala Sasisinagopi" likimaanisha: Mpangile anaeogopa mkuki risasi haogopi.

7). Kutokana na kuwa Mluguru kwa asili ndio maana Mtwa Mkwawa alikuwa na uhusiano wa karibu na mtemi Mazengo (Ugogo Dodoma) pamoja na mtemi Mirambo wa Unyamwezini Tabora. Mazengo, Mirambo na mtemi wa Uluguru walikuwa ndugu wa damu na walikuwa Wajomba wa Mkwawa.

8) Mtwa Mkwawa alikuwa na rada za asili alizozitega milimani ambazo zilikuwa zikimjulisha hali ya vita na ujio wa maadui katika himaya yake. Rada hizi zilizoitwa "Kimwanyula" zilopoangushwa na Wajerumani ndio ulikuwa mwanzo wa kushindwa kwa Mtwa Mkwawa katika vita.

9). Askari mkuu wa kikosi cha usalama wa ufalme wa Mtwa Mkwawa aitwae Chavala ndie aliesababisha anguko la Mkwawa mbele ya Wajerumani baada ya kuanika siri zote za kijeshi, kimizimu na kiganga alizokuwa akitumia Mkwawa. Chavala alishawishika kumuasi Mkwawa baada ya kupewa rupia 5,000 na Wajerumani.

10). Mtwa Mkwawa alikuwa na wake 63, waliokuwa wakiishi Ipamba na mamia ya watoto aliowajengea makazi eneo la Tosamaganga

Historia imesimama hiyo kama ni kweli, ila nimeshindwa kuunganisha dots kwa uhusiano Wa Mkwawa na Mirambo maana mmoja alikuwa Mkimbu na mwingine unasema alikuwa Mluguru! Chanzo cha simulizi hii ni wapi?

Sijui kwa nini wanahistoria Wa Tz ni wavivu kiasi hicho? Vitu vingi vimepotoshwa lakini hawataki kufanya uchunguzi Wa kina! Hata kule kwetu inafahamika kuwa Mwl.JK hakuwa damu ya Mzanaki bali ya Msukuma lakini hakuna anayejishughulisha kutafiti ukweli Wa historia hiyo!! Kazi tu nayo!
 
Unaeleza habari inayomhusu mtu anayeheshimika kwenye historia ya Tanzania halafu mwisho badala ya kuweka source ijulikanayo unaleta utani wa kuandika 'smart mind?'. If you are not serious who will take you seriously? Not me!
 
Mengne umeanda chaka,hao wajerumani walikuwa wanaongea kihehe?mpaka wamwambie huyo jamaa anaogopa mkuki bunduki haogopi
 
Hapo Kwenye Namba 5 Nakuunga Mkono. All In All Hakuna Anayeweza Kutupa Historia Kamili Ya Mkwawa Zaidi Ya Story Za Mitaani Kwani HATUKUWEPO KIPINDI HICHO.
 
Hapo Kwenye Namba 5 Nakuunga Mkono. All In All Hakuna Anayeweza Kutupa Historia Kamili Ya Mkwawa Zaidi Ya Story Za Mitaani Kwani HATUKUWEPO KIPINDI HICHO.

Ingekuwa hiyo ni sababu ya msingi basi kusingekuwa na HISTORY duaniani.
 
Mtwa Mkwawa alijua kusoma na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiarabu na alikuwa muumini wa dini ya Kiislamu.

Ni kweli Mkwawa alikuwa mwislamu na kuna simulizi za ajabu kuna mahali nilielezwa kuwa alikuwa ni mjahidina wa mwanzo kabisa ambaye alitumiwa kama proxy na waarabu kupigana na wajerumani kuwazuia wasieneze dini yao ya kilutheli kwenye maeneo yake ya utawala ambako uislamu ulikuwa ukijaribu kuyafikia.

Silaha zake za vita inasemekana alikuwa akipata toka kwa waarabu ushahidi ni aina ya bunduki alizotumia vitani ni zile ambazo waarabu walikuwa nazo.
 
Kwa hiyo mwafrika hawezi kuwa shujaa,mpaka asaidiwe?Mbona twajiangusha.
 
Ni kweli Mkwawa alikuwa mwislamu na kuna simulizi za ajabu kuna mahali nilielezwa kuwa alikuwa ni mjahidina wa mwanzo kabisa ambaye alitumiwa kama proxy na waarabu kupigana na wajerumani kuwazuia wasieneze dini yao ya kilutheli kwenye maeneo yake ya utawala ambako uislamu ulikuwa ukijaribu kuyafikia.

Silaha zake za vita inasemekana alikuwa akipata toka kwa waarabu ushahidi ni aina ya bunduki alizotumia vitani ni zile ambazo waarabu walikuwa nazo.
Kwa hiyo ukristo ulienezwa kwa njia ya vita.
 
Uongo mwingine kanyongwa kapigwa risasi hakufa. Halafu akawashauri jinsi ya kufa yeye. Ndio maana waongo wengi wamepewa majina v8 turbo wewe nakupa nakupa jina la intercooler. Hahahahaha.
 
Back
Top Bottom