Mtwa Mkwawa hakuwa muhehe

Mtwa Mkwawa hakuwa muhehe

Wideta bhe!.

Muongo mkubwa sana!.

1). Mtwa Mkwawa hakuwa mhehe na wala hakuwa mtoto wa Mnyigumba (kama historia iliyoandikwa na Wajerumani inavyopotosha); bali Mkwawa alikuwa ni mtoto wa dada wa Mnyigumba aliyeolewa na mtemi wa Waluguru; hivyo Mkwawa alikuwa Mluguru kwa asili.

Akiwa mdogo alikwenda kumtembelea mjomba wake (Mnyigumba) na kutokana na ushujaa wa Mkwawa akafanikiwa kumuokoa mjomba wake katika vita kali dhidi ya Wangoni pale Makambako. Mnyigumba akampenda Mkwawa kuliko watoto wake, na ndio chanzo cha kupewa urithi pamoja na mtoto wa Mnyigumba aliyeitwa Muhenga.

2). Sherehe za kuapishwa Mtwa Mkwawa zilifanyika Dodoma eneo linaloitwa Mpwapwa. Sherehe zilihudhuriwa na wajomba zake Mtemi Mazengo, Kimweri, Lugulu na Mirambo; ambapo walikuwa wakiimba "Mpwa! Mpwa!" na ndipo neno Mpwapwa likazaliwa.

3) Mtwa Mkwawa alikua na vikosi vinne vya majeshi ya vita; kimojawapo kilikuwa cha upelelezi na ushambuliaji [Kiitwacho Vamalavanu] ambacho kilikuwa kikila nyama ya mbwa ikichanganywa na dawa ya tambiko; wakiamini kuwa watakuwa na uwezo wa kunusa maadui na wao kutoonekana. Hivi ndivyo ulaji nyama ya mbwa ulivyoanza.

4). Mtwa Mkwawa alijua kusoma na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiarabu na alikuwa muumini wa dini ya Kiislamu.

5). Mtwa Mkwawa hakujipiga risasi bali alijitumbukiza katika daraja la Kikongoma (lililopo mto Ruaha) mahali ambapo mama yake mzazi pia alijitumbukiza na kujiua pale. Lile fuvu linalodaiwa kuwa la Mtwa Mkwawa inadaiwa ni la mlinzi wake. Hadi leo hakujawahi kufanyika DNA tests kuthibitisha fuvu hilo.

6). Kwenye vita iliyomsambaratisha Mtwa Mkwawa, Wajerumani walifanikiwa kumkamata mdogo wa Mkwawa aliyeitwa Mpangile, walimtundika kitanzini-hakufa, wakampiga risasi-hakufa! Baadae akatoboa siri kuwa wammwagie maji na wamchome mkuki-ndipo akafa! Baada ya kuona hivyo wakampa jina "Mpangelwangindo Mgopisala Sasisinagopi" likimaanisha: Mpangile anaeogopa mkuki risasi haogopi.

7). Kutokana na kuwa Mluguru kwa asili ndio maana Mtwa Mkwawa alikuwa na uhusiano wa karibu na mtemi Mazengo (Ugogo Dodoma) pamoja na mtemi Mirambo wa Unyamwezini Tabora. Mazengo, Mirambo na mtemi wa Uluguru walikuwa ndugu wa damu na walikuwa Wajomba wa Mkwawa.

8) Mtwa Mkwawa alikuwa na rada za asili alizozitega milimani ambazo zilikuwa zikimjulisha hali ya vita na ujio wa maadui katika himaya yake. Rada hizi zilizoitwa "Kimwanyula" zilopoangushwa na Wajerumani ndio ulikuwa mwanzo wa kushindwa kwa Mtwa Mkwawa katika vita.

9). Askari mkuu wa kikosi cha usalama wa ufalme wa Mtwa Mkwawa aitwae Chavala ndie aliesababisha anguko la Mkwawa mbele ya Wajerumani baada ya kuanika siri zote za kijeshi, kimizimu na kiganga alizokuwa akitumia Mkwawa. Chavala alishawishika kumuasi Mkwawa baada ya kupewa rupia 5,000 na Wajerumani.

10). Mtwa Mkwawa alikuwa na wake 63, waliokuwa wakiishi Ipamba na mamia ya watoto aliowajengea makazi eneo la Tosamaganga

Hii habari haina ukweli ikiwa mkwawa alikua muislam iweje tena awe anakula mbwa wakati dini take inamkataza muislam yuko tayari kunywa pombe na kuzini lakini kumlisha nguruwe seize mbwa hatokula
 
Hii habari ina uwongo mwingi kuliko ukweli. Nia yako nzuri lakini ulihitaji maandalizi ikiwemo kupata taarifa sahihi. Vinginevyo, uwongo huu haukujengi wewe, wahehe, wala warugulu.

1. Unaweza kuelezea kabila la wahehe lilianzaje? Maana kumbuka hapakuwahi kuwa na kabila la wahehe.

2. Unaweza kuelezea uhusiano uliokuwepo baina na Mkwawa na Mwambande?

3. Eti radar za asili, uwongo gani huu?

4. Mkwawa alienda Dodoma kwa chief Mazengo kuapishwa kweli? Mbona wewe mwongo hivi?

KWA UJUMLA HISTORIA YAKO IMEBUMBWA BUMBWA SANA. UNAPOKOSA TAARIFA UNALAZIMISHA USHIRIKINA ILI WATU WASIHOJI. ACHA HIZO. HISTORIA SAHIHI YA MKWAWA TUNAIJUA JAPO HUWA IKO TOFAUTI KIASI NA YA WAJERUMANI LAKINI NA YA KWAKO IKO KIVYAKO VYAKO SANA.

Wewe unaesema uongo unatakiwa uje na ukweli, pinga kwa hoja mkuu
 
Wewe ndiye mwenye publicity. Umeandika uwongo nimeuona, nikakupa maeneo ya kufanyia utafiti ili uboreshe mada habari yako. Sasa hutaki kufanya research unataka nikupe majibu, wakati kazi ni ya kwako. Hii siyo ajabu kijana wangu?

Nenda kakusanye taarifa upya. Hiki ulichokiandika hapa ni uwongo mwingi sana. Kama huwezi kuonana na wenye ukoo wao nenda kalenga ukapate taarifa sahihi. Hii biashara ya kutungatunga, hapana kijana wangu.

Wewe unaesema uongo unatakiwa uje na ukweli, pinga kwa hoja mkuu
 
Si wametaka kujua smart mind ni nani?

Swali ni ''amekuruhusu uweke jina lake?'' Hivi wakitaka kujua Patrickn ni nani? na kukawa anayekujua, akurupuke tu kuleta jina lako hapa na details zingine bila idhini yako?
 
1). Mtwa Mkwawa hakuwa mhehe na wala hakuwa mtoto wa Mnyigumba (kama historia iliyoandikwa na Wajerumani inavyopotosha); bali Mkwawa alikuwa ni mtoto wa dada wa Mnyigumba aliyeolewa na mtemi wa Waluguru; hivyo Mkwawa alikuwa Mluguru kwa asili.

Akiwa mdogo alikwenda kumtembelea mjomba wake (Mnyigumba) na kutokana na ushujaa wa Mkwawa akafanikiwa kumuokoa mjomba wake katika vita kali dhidi ya Wangoni pale Makambako. Mnyigumba akampenda Mkwawa kuliko watoto wake, na ndio chanzo cha kupewa urithi pamoja na mtoto wa Mnyigumba aliyeitwa Muhenga.

2). Sherehe za kuapishwa Mtwa Mkwawa zilifanyika Dodoma eneo linaloitwa Mpwapwa. Sherehe zilihudhuriwa na wajomba zake Mtemi Mazengo, Kimweri, Lugulu na Mirambo; ambapo walikuwa wakiimba "Mpwa! Mpwa!" na ndipo neno Mpwapwa likazaliwa.

3) Mtwa Mkwawa alikua na vikosi vinne vya majeshi ya vita; kimojawapo kilikuwa cha upelelezi na ushambuliaji [Kiitwacho Vamalavanu] ambacho kilikuwa kikila nyama ya mbwa ikichanganywa na dawa ya tambiko; wakiamini kuwa watakuwa na uwezo wa kunusa maadui na wao kutoonekana. Hivi ndivyo ulaji nyama ya mbwa ulivyoanza.

4). Mtwa Mkwawa alijua kusoma na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiarabu na alikuwa muumini wa dini ya Kiislamu.

5). Mtwa Mkwawa hakujipiga risasi bali alijitumbukiza katika daraja la Kikongoma (lililopo mto Ruaha) mahali ambapo mama yake mzazi pia alijitumbukiza na kujiua pale. Lile fuvu linalodaiwa kuwa la Mtwa Mkwawa inadaiwa ni la mlinzi wake. Hadi leo hakujawahi kufanyika DNA tests kuthibitisha fuvu hilo.

6). Kwenye vita iliyomsambaratisha Mtwa Mkwawa, Wajerumani walifanikiwa kumkamata mdogo wa Mkwawa aliyeitwa Mpangile, walimtundika kitanzini-hakufa, wakampiga risasi-hakufa! Baadae akatoboa siri kuwa wammwagie maji na wamchome mkuki-ndipo akafa! Baada ya kuona hivyo wakampa jina "Mpangelwangindo Mgopisala Sasisinagopi" likimaanisha: Mpangile anaeogopa mkuki risasi haogopi.

7). Kutokana na kuwa Mluguru kwa asili ndio maana Mtwa Mkwawa alikuwa na uhusiano wa karibu na mtemi Mazengo (Ugogo Dodoma) pamoja na mtemi Mirambo wa Unyamwezini Tabora. Mazengo, Mirambo na mtemi wa Uluguru walikuwa ndugu wa damu na walikuwa Wajomba wa Mkwawa.

8) Mtwa Mkwawa alikuwa na rada za asili alizozitega milimani ambazo zilikuwa zikimjulisha hali ya vita na ujio wa maadui katika himaya yake. Rada hizi zilizoitwa "Kimwanyula" zilopoangushwa na Wajerumani ndio ulikuwa mwanzo wa kushindwa kwa Mtwa Mkwawa katika vita.

9). Askari mkuu wa kikosi cha usalama wa ufalme wa Mtwa Mkwawa aitwae Chavala ndie aliesababisha anguko la Mkwawa mbele ya Wajerumani baada ya kuanika siri zote za kijeshi, kimizimu na kiganga alizokuwa akitumia Mkwawa. Chavala alishawishika kumuasi Mkwawa baada ya kupewa rupia 5,000 na Wajerumani.

10). Mtwa Mkwawa alikuwa na wake 63, waliokuwa wakiishi Ipamba na mamia ya watoto aliowajengea makazi eneo la Tosamaganga

Citation please, kuna mengine yanaeleweka ila mengine yamejaa utata tu!
 
Nadhani ni vizuri walio na taarifa sahihi wangeileta hapa ili tusiojua kwa undani historia ya Mkwawa tukaijua zaidi.
 
Back
Top Bottom