Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Si kweli,wapo Askari wema tena wokovu kabisa,yaani hata umpe Rushwa ambayo hajakuomba kama Asante tu unakuta anakataa anasema ametimiza wajibu wake,acha ku-generalise mambo
Hao Askari Polisi unaodai kuwa ni "wema na wokovu ambao wanakataa rushwa na kusema kwamba wametimiza wajibu wao" ni Waajiriwa wa Jeshi la Polisi la nchi hii hii ya Tanzania tuliomo au nchi nyingine tusiyoifahamu?
 
Hao Askari Polisi unaodai kuwa ni "wema na wokovu ambao wanakataa rushwa na kusema kwamba wametimiza wajibu wao" ni Waajiriwa wa Jeshi la Polisi la nchi hii hii ya Tanzania tuliomo au nchi nyingine tusiyoifahamu???!!??
Acha UJINGA, nimelitumikia Jeshi la Polisi Tanzania kwa miaka 9 na kwa level zote Junior Officer na Senior Officer(Inspector), hivyo nina uhakika wa Asilimia 100 kwa ninachokisema
 
Na yote kwa yote, wakati wewe umelala nyumbani kwako umemkumbatia mkeo, kumbuka kuna watu wapo mtaani doria usiku kucha kuhakikisha usalama wako wewe na huyo uliyemkumbatia,hivyo lawama zote za humu dhidi ya Jeshi la Polisi ni LAZIMA ziwe na kipimo,isiwe makosa ya matukio machache kama hili la Mtwara basi wote mlilaumu Jeshi la Polisi kwamba limeoza,ni la Makatili,Wazulumaji na Wauaji,eti mjinga mmoja anakuja JF na kuandika UPUUZI kwamba Askari Polisi wote ni Wauaji,Majangili nk, si SAWA.

Nilikuwa Askari Polisi na nikaacha kazi kwa hiari yangu kwa notisi ya masaa 24, nitaendelea kulitetea Jeshi la Polisi kwamba si wote ni wabaya mpaka naingia kaburini,na kimsingi hakuna sekta wala taaluma iliyo sahihi kwa Asilimia 100, Taaluma zote zina watendaji waovu ndio maana CAG miaka yote anagundua ubadhilifu wa kutisha kwenye sekta zote nchini.
 
Yeye kama Daktari unaambiwa mchome mtu Sindano ya usingizi alafu unamchoma tu.Daktari anayo kesi kubwa ya kujibu pia.

Ukisoma Maelezo ya Dr ya mwanzoni kabisa alikana kuwa hajawahi kuchoma MTU sindano ya sumu / kuua??, Halafu eti akatoa wazo kuwa anaweza kumchoma sindano ya usingizi ambayo itapelekea mtuhumiwa kusema mambo yote ya kiukweli ambayo yatasaidia Police, hapa nafikiri alikuwa anaongelea "Ketamine" kitu ambacho sidhani kama ACP Mgonja alikiulizia na kama kweli ilikuwa Ni Ketamine Je Dr alikuwa na resuscitation kit kwenye tukio ili kujua kuwa hakuwa na Nia ovu kama wenzie? Dr huyu anaweza kupenya ila kwenye tundu la sindano.
 
Kumbe wewe ni Askari Polisi, Ndio maana unawatetea Askari wenzako.

Kumbuka tu kwamba kwa uovu mbaya kabisa ambao Jeshi la Polisi Tz limekuwa likijihusisha nao kwa miaka mingi sasa, haliteteeki tena na kuweza kueleweka na wananchi. Mifano mibaya juu ya uovu wa Jeshi hili ni mingi sana ukilinganisha na mifano mizuri ya mema yake ambayo limefanya. Ni vigumu sana kulitetea Jeshi la Polisi na kisha ukaeleweka na wananchi wa kawaida wenye akili timamu vichwani mwao. Wananchi wengi zaidi hapa nchini hawana Imani kabisa na Jeshi la Polisi, wananchi wamepoteza kabisa Imani dhidi ya Jeshi hili, pamoja na kukosa Imani dhidi ya Askari Polisi mmoja mmoja.

Askari Polisi walio wasafi, waadilifu na waaminifu ni wachache sana kupita kiasi, idadi yao haifiki hata asilimia 0.01 ya idadi ya Askari Polisi wote ndani ya Jeshi hilo, Askari Polisi waovu na wahalifu ni wengi zaidi ktk Jeshi hilo(zaidi ya asilimia 99.90 ya Askari wote) hivyo kuwafunika kabisa wale Askari wachache walio waadilifu na kulifanya Jeshi lote kuonekana kuwa ni Jeshi la watu Waovu na Wahalifu, Jeshi la Wauaji na waporaji, Jeshi liliojaa kila aina ya uovu na ushetani.

Njia iliyo sahihi kwenu ya kulitetea na kulisafisha Jeshi hili la Polisi nikubadilika na kuacha uovu sambamba na kuwashughulikia kikamilifu na waziwazi kabisa wale Askari Polisi wote wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi, wale Askari Polisi watakaobainika kujihusisha na makosa makubwa au uhalifu mkubwa kabisa kama hao walioshitakiwa huko Mtwara ni kutumia Sheria kali kabisa za Jeshi ili kumalizana nao. Mathani, hao Askari Pilisi wenye.

Makosa makubwa kama hao wa Mtwara walipaswa kufikishwa kwenye Mahakama ya Kijeshi(Court Marshall) kwa kosa la Kufanya Uasi au Usaliti dhidi ya Umma/Raia wa Tz, wangekutwa na hatia na kisha kumalizana nao kuwanyonga kwa "Firing Squad". Jeshi hilo lingefanya hivi kwa kiasi fulani Askari Polisi wangeanza kuwa waadilifu, na hata raia wa kawaida wangeanza kurejesha Imani yao dhidi ya Jeshi la Polisi.
 
Doria ni kazi yao, asubuhi wao wanalala na wake zao na sisi tunakuwa maofisini kukusanya mapato ya malipo yao.
Tumia akili boya wewe, kwahiyo unataka tukalinde wote?
 
Huyo mpelelezi alishawahi nipiga mikwala siku moja nikiwa eneo fulani hivi lindi the way nilivyomuona siku ile jicho la tatu likaona sio mtu mwemaa...anyway baada ya kujua nipo pale kwa ajili ya bosi wake akajifanya kuwa friendly.police wanapigana sana majungu aisee ukiwa mtu wa watu .... Utajikuta ushapangiwa uswekeni porini huko...sio kama hawaoni tunavyoteseka nao hawana nguvu jifanye kiherehere cha kutetea raia utundikee jeziii...police nao binadamu wapo wema na wabaya
 
Si kweli,wapo Askari wema tena wokovu kabisa,yaani hata umpe Rushwa ambayo hajakuomba kama Asante tu unakuta anakataa anasema ametimiza wajibu wake,acha ku-generalise mambo
Nakuunga mkono mkuu.ninao marafiki zangu tena wameokoka kabisa..tatizo tumezoea kutoa lawama sana kwa police..
 
Polisi wema ni wachache sana ukilinganisha na idadi ya Polisi wabaya ambao ni wengi zaidi ndani ya Jeshi la Polisi, na hai ndio walioliteka Jeshi hili kiasi cha kuwafunika kabisa Polisi wema ambao ni wachache.
Kumbuka: "Mabaya huvuma zaidi kuliko mema."
 
Daktari hana pa kuchomokea hapa,

Ktendo tu cha kuambiwa amchome sindano.... Na yeye kuhiyari kutekeleza... Tayari ni Attempt Murder!...

Alikuwa anajua dhumuni la anachoenda kukitenda•

Kwa ushahidi alioutoa ACP Mgonja kama shahidi namba moja inaonyesha hakuna mahali kamtaja Dr kumchoma marehemu sindano ya sumu na hata majibu toka kwa mkemia wa serikali hayakuonyesha kuwa yale mabaki ya mbavu na funza kuwa na sumu wala Aina yoyote ya dawa ya usingizi na ukirejeaa maswali ya ufafanuzi toka kwa wakili wa Dr Msuya utaona kuwa ACP shahidi kamtoa Dr kwa asiilimia 💯, naona kwambaaali Dr Hana kesi ya Kujibu ila atasota na kujifunza kuwa smart
 
Polis ni majAmbaz yeny kibal cha kikaz'_ in voice of langa kileo
 
Hii kesi inaendelea au?
Nilitaka kujua,hivi polisi hawanaga mahakama zao za jeshi la polisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…