Mtwara: Jinsi Askari Polisi akiwemo Mkuu wa Kituo na Upelelezi walivyoshiriki Mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini

Awali kabisa Dr alielezwa na Kalanje kwamba huyu ni mtu wetu amefanya matukio mengi ya wizi wa pikipiki katika mikoa ya Dar, Mtwara na Lindi sasa tumechoka tunataka TUMALIZANE NAE. Akatoa wazo la Dr amchome sindano ya sumu, lakini yeye Dr akapendekeza kuwa amchome sindano ya usingizi kisha akiamka ataanza kueleza ukweli wa matukio yote aliyofanya.

Hapa najiuliza Dr hakumsikia kuwa SASA WANATAKA WAMALIZANE NAYE?
Je kitendo cha kumchoma sindano ya usingizi kingeleta jambo gani jipya zaidi ya alichosema Kalanje. Kitendo cha Kalanje kumziba pua na mdomo yeye kama Dr hakuona kuwa ni hatari kwa mtu ambaye yuko katika usingizi mzito akaweza kukanya kuto mziba pua na mdomo.
Alipoitwa na kuuliza " TAYARI?" Je Dr anataka kusema hakujua kitendo cha kumziba pua na mdomo kingepelekea kifo? Alipoona TAYARI mbona hatuoni akimfokea mfunikaji pua na mdomo kwamba kwanini umefanya kinyume na nilivyokuelekeza?

Dr alitoa maelekezo kwa Kalanje kwamba ili isipnekane amekufa bila purukushani isionekane kapigwa mzibe pumzi. Huyu ni mhalifu kama wenzie.
Halafu kuhusu huyu aliyejinyonga inaonekana alinyongwa na wenzie baada ya kujilipua kuonyesha mahali walipoutupa mwili wakaona huyu atakuwa shahidi dhidi yao wakammaliza. Hiyo kamba aliipata wapi? Wakati mwingine hawa polisi wanatuona sisi raia ni wajinga kumbe wao ndiyo.
 
Je, Kesi hii imeishia wapi?

Watu mliopo huko Mtwara tunaomba mtupatie mrejesho. Tujulisheni Nini hasa kinaendelea kuhusiana na Kesi hii ya Jinai Na. 15 ya Mwaka 2023.

Mawakili na Wanaharakati wa Haki za Binadamu mliopo mjini Mtwara mwende kwenye Masijala ya Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara na fanyeni mapitio ya Jalada la Kesi hii (File Perusal) na kisha muujulishe umma juu ya nini hasa kinaendelea kuhusiana na Kesi hii.
 
Polisi na mfanyabiashara wa madini. Haya matukio yanaonekana yako mengi sana, ni vile wengine wanamuachie Mungu.

Ukiletewa uhuni na maskini mwenzio unamloga kwa mganga, ukifanyiwa uhuni na polisi na mwanasiasa unamawachia Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…