Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa kati ya miaka nane hadi kumi, mkazi wa Mtaa wa Lilungu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, amefariki dunia baada ya kunyongwa na watu wasiojulikana.
Tukio hilo limetokea jioni ya Juni 21, 2026, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Moreen ambaye ni mtoto wa askari magereza, alikuwa akicheza na wenzake wanne kabla ya watu wasiojulikana kujitokeza, kumchukua na kutoweka naye kusikojulikana.
Mashuhuda hao pia wameeleza wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama katika eneo hilo, wakidai kuwepo kwa mazingira yanayochochea uhalifu, huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula amethibitisha kupokea mwili wa marehemu Moreen kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi (postmortem) ili kubaini chanzo halisi cha kifo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limeanza uchunguzi wa kina kubaini mazingira ya tukio hilo pamoja na kuwakamata waliohusika. Aidha, limewataka wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa sahihi na za siri zitakazosaidia kufanikisha uchunguzi.
RAI YANGU NI HII:
Kwanza kabsa sijawahi kuunga mkono masuala ya violence kwa namna yoyote, haswa kwenye kulipiza kisasi. Askari magereza anaweza kuwa na bifu na raia lakini pia wao kama wao. Kama ni uchunguzi anzeni huko huko kwa Maaskari Magereza kisha muelekee kwa wananchi.
Lakini la pili ni kwamba lazma tukubaliane kuwa hali ya usalama imekuwa ni kwenye kiwango cha ovyo sana sio kwa watu wazma na wala sio kwa watoto. Na ukizingatia imani ya watu wengi ilivyodhaifu kwa majeshi yetu. Huyu mtoto sio wa kwanza kupoteza maisha, tusisahau kuna watoto kibao waliopoteza maisha October mwaka jana, na hakuna uchunguzi uliofanyika.
Pole kwa familia pamoja na ndugu na jamaa kwa msiba huu ila twendeni mbele turudi nyuma, kuna mengi ya kufanya ili amani na usalama urejee kama zamani.