The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Uongozi wa shule ya sekondari ya Kiyanga halmashauri ya mji Nanyamba mkoani Mtwara, umelazimika kuanza masomo na wanafunzi 74 wa kidato cha kwanza wasiokuwa na sare, ili kuendana na ratiba za masomo.
Mkuu wa shule hiyo Vagrey Kidava, amesema shule yao ni mpya na imefunguliwa Februari 10, 2025, hivyo wameona ni bora waanze masomo kisha sare zitafuata baadaye.
Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota, amefika kukagua shule hiyo yenye vyumba Vutatu vya madarasa na matundu Sita ya vyoo, ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 80.
Amesema changamoto za uhaba wa nyumba za walimu na walimu kwa ujumla zinakwenda kutatuliwa na serikali, huku akiwataka wanafunzi kuweka jitihada kwenye masomo.