Mtwara: Wanafunzi 74 wa shule mpya ya sekondari walazimika kuanza masomo bila sare ili kuendana na ratiba

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Uongozi wa shule ya sekondari ya Kiyanga halmashauri ya mji Nanyamba mkoani Mtwara, umelazimika kuanza masomo na wanafunzi 74 wa kidato cha kwanza wasiokuwa na sare, ili kuendana na ratiba za masomo.

Mkuu wa shule hiyo Vagrey Kidava, amesema shule yao ni mpya na imefunguliwa Februari 10, 2025, hivyo wameona ni bora waanze masomo kisha sare zitafuata baadaye.

Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota, amefika kukagua shule hiyo yenye vyumba Vutatu vya madarasa na matundu Sita ya vyoo, ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 80.

Amesema changamoto za uhaba wa nyumba za walimu na walimu kwa ujumla zinakwenda kutatuliwa na serikali, huku akiwataka wanafunzi kuweka jitihada kwenye masomo.
 
umaskini mbaya mno tupo tunaingia mwezi march lakin hola
 
Ila hawapo happy maana kuanza shule inatakiwa ubadilike tokea uvaaji na upokeaji wa masomo
 
Halafu NETO wanaonekana hawana hoja ya msingi wakati bado kuna shule zina uhaba wa walimu.
 
Mambo ni moto
 

Attachments

  • IMG_20250223_221115.jpg
    326.8 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…