Mtwara: Wanafunzi wasababisha tatizo la umeme kwa wilaya nne

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Wilaya nne za mkoa wa Mtwara zimekosa nishati ya umeme kwa takribani saa ishirini na nne na kupelekea baadhi ya shughuli za kiuchumi kusimama, baada wanafunzi wa kidato cha tatu na cha pili wa shule ya sekondari Mnyawi kuchezea laini kubwa ya umeme kwa kurusha miti na kufurahia mwanga pale nyaya zinapogusana.

Meneja wa TANESCO wilaya ya Tandahimba Edward Namoto amesema michezo hiyo ni hatari lakini pia inaumiza wananchi wanaotegemea nishati hiyo kujipatia kipato.

Aidha, Wanafunzi hao wa kidato cha tatu ambao wamepanga katika kijiji hicho kwa ajili ya ukaribu wa shule wamekiri hilo.

Chanzo: ITV
 
Hata hivyo ni wajasiri sana, wanacheza na moto bila hata ya woga!
 
Nawalaumu tena Tanesco, kwanini wanaweka insulated wire tena zikiwa loose mpaka zikaribiane na kuweza kugusana zinaporushiwa vijiti tu, why no tight the cables?

Nadhani wameajiri wahandisi uchwara
 

[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Pelekeni umeme huko acheni visingizio ule DSM mlisema kunguru wakikaa vikao kwenye nyaya umeme hauvuki mara ooh kwani mkisema kuna mgao mtaumwa COVD 19?
Ina maana hao kunguru wamekuwa na nguvu kama yule Mzee wa Iringa
 
Ngoja waje wakanushe usikute hata hapo walipopanga hizo nyumba hazina umeme na nguzo zimepita karibu tu hapo ndo maana wanaamua
Kumpopoa shetani mawe!

Anway hao vijana waipib akhera yakhe!
 
Visingizio vya uongo kabisa
 
Pamoja na kwamba sikubaliani na huu utetezi wa tanesco kwa kukosekana umeme masaa 24, lakini huu mchezo wa kurusha miti mibichi kwenye nyaya za umeme nimeufanya sana miaka ya 1985/86. ule mlipuko unaotokea pale ilikuwa ni burudani tosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…