Mtwara: Waziri wa Afya Mchengerwa anazindua Bima ya Afya kesho. UVCCM hawataki niende kumsikiliza. Wananitishia

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Wakuu,

Kesho Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Bima ya Afya kwa Wote, Awamu ya Pili.

Hapa nilipo nipo njiani naelekea Mtwara.

Lakini nipo chonjo sana. Hawa UVCCM hawataki nihudhurie kisa niliandika habari ya wao kula Rushwa. Wanadai nilipost bila kuibalance. Walitaka niwaombe Ruhusa kabla ya kupost ulaji wao wa Rushwa. Na kesho UVCCM tutawabagaza na kuwabananga.

Je, watanifanya nini? Kwanza nikitoka Mtwara nawafuata Zanzibar kwenye mkutano wao. Aibu wataona wao.

So naenda Mtwara leo waje waniteke kama wanaweza. Kesho tukutane Viwanja vya Sabasaba tukajifunze Elimu kuhusu Bima ya Afya. Baada ya hapo tunawafuata UVCCM Zanzibar. Wala rushwa wakubwa.

Nilichogundua UVCCM wanakula Rushwa sana. Na ukitoa hiyo siri ya wao kula rushwa wanakuwa wakali kama pilipili.

Naenda Mtwara, na ntamshauri Mchengerwa awape kidonge kingine. Awanange... Halafu tuwaandike na Video tuzisambaze.

Kama itawauma wachomoe.
 
Waulize wao
 


Aiseee
 
Tatizo la Mchengerwa ni kuita spade, a spade and not a big spoon.
Mchengerwa alipaswa aseme kwamba UVCCM wanapenda kula 'posho' nao wangemjibu, brother huku kitaani hali ngumu, tunasongesha kibishi!
Huku kwenye siasa ni kupindisha maneno ili kufikisha ujumbe bila kuumiza mioyo ya watu.
Chuoni hii kozi ilikuwa inaitwa communication skills.
 
Hawa Uvccm ni waajiriwa wa CCM? Wanalipwa mishahara na CCM na kazi zao za kila siku huko CCM ni zipo?
Usimtuhumu mtu kuwa anakula rushes wakati hauja muajiri na haumlipi mshahara.
 
ACHA wapalulane wajinga sana
Lakini inanibidi nitafute msaada wa elimu kwenye swala hili la rushwa.

Hii rushwa huko UVCCM inahusiana na kitu gani hasa?

Hawa UVCCM wanakula rushwa toka kwa aikina nani, na ili wawafanyie nini hao watoa rushwa.
Huko UVCCM wanayo madaraka ya kuwafanya wawalazimishe watu; kwa mfano wafanya biashara matajiri watoe rushwa ili mambo yao yaende vizuri?
UVCCM wanazo njia za kuzuia uwekezaji mkubwa wa miradi mbalimbali kama hawatapewa rushwa?

Hizi rushwa za UVCCM zinahusu nini?
Vijana wanaotaka kuingia kwenye ulaji kwa kujiunga na umoja huo, '''kwamba bila ya kutoa rushwa kijana hapewi fursa ya kuingia UVCCM? Hii ndiyo anayoizungumzia Mchengerwa, na imemkera sana?

Ninachoona hapa ni maigizoi tu na hadaa kwa waTanzania. Mchengerwa na hao vijana wote ni bidhaa mbovu kabisa ndani ya taifa hili.
 
Lazima tuwaambie UVCCM waache tabia kama za BAVICHA za kina heche na genge lake za kula rushwa ,tutawaambia ukweli hadi hakome

USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…