Muafrika hawezi kuendelea asipoachana na hizi dini za wageni

Muafrika hawezi kuendelea asipoachana na hizi dini za wageni

Afrocentric view

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
1,374
Reaction score
2,280
Hello wakuu.
Nyerere aliwahi kusema anashangaa wanyonge wanatengana wakati wenye nguvu wanaungana kumtawala mnyonge.
Umoja ni nguvu, Afrika haiwezi kujitawala tusipokuwa wamoja.

Huwa inaniuma sana kuona vijana kwa wazee wa kike kwa kiume wote wenye ngozi nyeusi wakitukanana, wakibaguana na kutengana kisa hizi dini zilizoletwa na watu weupe.

Dini zimeletwa kwaajili ya kututawala na hili liko wazi kabisa.
Ndiyomaana nchi kama China na Urusi hazitaki raia wake kulewa hizi dini za wageni. Kwasababu wanajua raia wakishalewa hizi dini ni rahisi kutawaliwa.

Raia wa Urusi wangekuwa wakristo wote wangemtetea marekani na kumpinga Putin.

Hata hapa bongo,utakuta dini hii wako upande wa waarabu na nyingine wako upande wa wazungu.
So tayari psychologically wanatugawa na wanaweza kutufanya chochote.

Sudan,Somalia,Nigeria nk. Kuna machafuko na watu weusi wanauana wao kwa wao kisa hizi dini za wageni.

Njia pekee ya Afrika kujitegemea ni kuachana na hizi dini za wageni na kuzikemea kwa nguvu zote maana hazina faida kwetu isipokuwa kututenganisha na kutufitinisha.
Hazina faida yoyote hizi dini.
 
Back
Top Bottom