Mualiko kwa wana JamiiForum: Tarehe 12/12/2022 tutakuwa na Mawlid ya Mtume Muhammad (S.A.W) hapa BAKIIF ISLAMIC

Mualiko kwa wana JamiiForum: Tarehe 12/12/2022 tutakuwa na Mawlid ya Mtume Muhammad (S.A.W) hapa BAKIIF ISLAMIC

السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ

Kama mjuavyo uislamu sio dini ngumu, thamani ya Biriani, Pilau na Ubwabwa, viliwe katika mjumuiko wa kheri ambao MUNGU anauridhia, hivyo tunachukua fursa hii kuwatangazia waislamu wote wa JamiiForum kwamba Tare 12/12/2022 siku ya Jumamosi saa mbili kamili usiku tutakuwa na Mawlid ya kumuadhimisha mtukufu wa Umma, Nabii Muhammad S.a.w hapa BAKIIF ISLAMIC, Kimara-Korogwe Dar es salaam, Tanzania.

Nachukua fursa hii kukukaribisha ufike bila kukosa, tusherehekee kwa pamoja khafla hii ya Mazazi ya Mtume Muhammad s.a.w, na pia unaweza kuchangia kufanikisha shughuli hii adhwim kwa kuwakilisha mchango wako au swadaka yako hapa BAKIIF ISLAMIC. Katika siku hiyo tutapata wasaa wa kuwarehemu ndugu zetu walio tangulia mbele za haki. Hivyo usikose kujumuika nasi katika viwanja vya BAKIIF.

Wabillahi taufiq walhidayah"

BAKIIF ISLAMIC
P.O.BOX 55185
Kimara Korogwe,
KAM College Road, Kivulini Street
House no 36

Phone +255 755 351 262

View attachment 2420271

Hapa chini Waeza burudika na Qasida (Annayu Watwaru)

View attachment 2420274
Sema mie si wa maulidi ningekuja
 
Sisi Waislamu husoma maulidi kwa sababu mbalimbali. Kati ya hizo ni kuikumbuka na kuitukuza siku aliyozaliwa mbora wa viumbe vyote, aliyetutoa vizani na kututia kwenye nuru, ni njia moja ya kutoa shukrani zetu kwa neema hiyo, katika sherehe hizo, hupatikana fursa ya kukumbushana maisha ya bwana mkubwa huyo na mafunzo yake, hupatikana fursa ya Waislamu wa madhihabi mbalimbali kushirikiana na kuziweka kando hitilafu zao, mikusanyiko hiyo huleta athari kwa wasio Waislamu ya kuupenda Uislamu, na hata kusilimu. Karibu tujumuike hapa BAKIIF
bila ya kusahau na kutukumbusha ya kuwa mwisho wa hafra ya Mtume kuna Ikramu ya chakula....ama hapo kwenu mmepanga kutulisha Ugali
 
Utatukumbusha tena Ikisalia siku 2 hivi mkuu.

Waislam hawanaga baya kwenye mialiko.

Kwakweli nitakuja.
 
Wabillah Tawfiq! Assalaam alleykum!!

Nitakuwepo siku hiyo kwa ajili ya kufinya Sheikh.
Ahsante sana ndugu, save number +255 755 351 262 usisite kuwasiliana nasi, pia mlango uko wazi kama una chochote cha kuchangia katika kukamilisha khafla hii adhwim. Karibu sana
 
kwani tarehe alizaliwa mtume mmeijulia wapi na lini?
Muhammad (S.A.W) alizaliwa tarehe 12 Rabi' al-awwal. mawlid au mīlad, katika Uislamu, ni siku ya kuzaliwa kwa mtu mtakatifu, kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Mawlid al-Nabi). Mtukufu Mtume Muhammad alizaliwa mwaka 570 CE (53 BH) · Maka, Hejaz, Bala la Arabia; Alikufa, (632-06-08)8 Juni 632 (11 AH) (umri wa miaka 61-62). Madina, Hejaz, Arabia. Hayo yanapatikana katika historia yake.
 
Tatizo wamealikwa waislam pekee....wapendwa wa Mnyaazi mungu
Karibu sana ndugu, hata kama ni Mkristo, tumealika waislamu kwakuwa hii ni imani yao, lakini hakuna ubaya kwa mkristo kutufikia hapa. Tunawakaribisha sana. Tuungane katika kusherehekea usiku huo. Save number +255 755 351 262
 
Alooo huu nimeuona ukweli mm mkristo ila Skuhyo ntakuja na kanzu maridadi sana ilimradi niupige mwingi.
Takbiiiiiiiiiiiirrrrrrrrrrr.....
Ahsante, upigilie na kizbao kwa juu, na manukato mazuri. Karibu sana hapa BAKIIF.
 
Nawatakia shughuli njema nipo mbali na dar
Tutakuwa live kwa social media zetu kuitangaza Mawlid al-Nabiy, uwe mwenye furaha na baraka za Mtume Muhammad ziwe nawe daima! Ni Wakati wetu sasa, Kukumbuka, Kusherehekea, Kuwa na Fahari. Nakutakia Wewe na Familia Yako Nyakati Nyingi za Furaha kwenye Mawlid al-Nabi na Mafundisho ya Nabii yakuongoze Daima. Pia waeza jumuika nasi kwa kuwasilisha mchango wako katika ukamilishaji wa shughuli hii, MUNGU atakulipa na kukufungulia zaidi.
 
52BDD0BC-47A6-4AE1-BC89-D0DB27AE968C.jpeg
 
السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ

Kama mjuavyo uislamu sio dini ngumu, thamani ya Biriani, Pilau na Ubwabwa, viliwe katika mjumuiko wa kheri ambao MUNGU anauridhia, hivyo tunachukua fursa hii kuwatangazia waislamu wote wa JamiiForum kwamba Tare 12/12/2022 siku ya Jumamosi saa mbili kamili usiku tutakuwa na Mawlid ya kumuadhimisha mtukufu wa Umma, Nabii Muhammad S.a.w hapa BAKIIF ISLAMIC, Kimara-Korogwe Dar es salaam, Tanzania.

Nachukua fursa hii kukukaribisha ufike bila kukosa, tusherehekee kwa pamoja khafla hii ya Mazazi ya Mtume Muhammad s.a.w, na pia unaweza kuchangia kufanikisha shughuli hii adhwim kwa kuwakilisha mchango wako au swadaka yako hapa BAKIIF ISLAMIC. Katika siku hiyo tutapata wasaa wa kuwarehemu ndugu zetu walio tangulia mbele za haki. Hivyo usikose kujumuika nasi katika viwanja vya BAKIIF.

Wabillahi taufiq walhidayah"

BAKIIF ISLAMIC
P.O.BOX 55185
Kimara Korogwe,
KAM College Road, Kivulini Street
House no 36

Phone +255 755 351 262

View attachment 2420271

Hapa chini Waeza burudika na Qasida (Annayu Watwaru)

View attachment 2420274
Mkuu samahani kidogo naomba unieleweshe kitu,hivi kwa nini katika huu Uislam kuna Waislam wengine hawataki kusikia habari za Maulid?hasa hawa Sunni,naomba unieleweshe mkuu

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Madhehebu ni mafundisho, maadili na matendo ya ibada yaliyo ya msingi katika dini fulani. Ni makundi ndani ya dini fulani ambayo yanatofautiana bila ya kuvunja umoja wa msingi. Madhehebu mbalimbali ya dini ileile yanaweza kushindana hata kupigana vita. Kwa kifupi madhehebu ni mapokeo ya ufahamu kunako dini husika. Wakati alipoishi

Yesu Kristo, dini ya Uyahudi ilikuwa na madhehebu yaliyoshindana sana, hasa Masadukayo, Mafarisayo na Waeseni lakini wote walibakia kuwa ni dini ya uyahudi japokuwa walikuwa wanatofautiana kwa mengi.

Wafuasi wa dini ya Ukristo, kutokana na wingi wao katika urefu wa historia na upana wa jiografia, wamegawanyika katika madhehebu mengi, kuanzia Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki hadi makundi elfu kadhaa ya Uprotestanti na ushirika wa Anglikana na yanazidi kuongezeka siku kwa siku lakini wote wanabakia katika njia kuu ya UKristo ispokuwa mapokezi yao yametofautiana kwa baadhi ya vitu.

Sasa katika uislamu kuna mikondo mitatu mikubwa ambayo ni Sunni-Waljamaa, Shia na Wahabiyya ambao ni Answar Sunna. Shia ndani yao wamegawanyika katika makundi mengi zaidi.

Sunni-waljamaa kuna madhehebu au madhhab manne yanayokubaliwa rasmi. Wahabiyya wao walianza kujiita Answar Sunna' ni dhehebu ndani ya Sunni lililo vuka mipaka katika sheria za dini. Sunni wote wanafanya Mawlid ispokuwa hao 'Wahabiyya au Answar sunna' ambao kwasasa nao wamegawanyika ndani yake kuna dhehebu la 'Salafy Swaleh' ambalo lina misimamo mikali zaidi na sheria zao ni kali zaidi wao wanajihusisha na mambo ya itikadi zaidi (Tawhid).

Kwa hivyo Mawlid hupingwa na Wahabiya na sio Sunni. Mawahaby pia hupinga kupiga dufu, hupinga watu kusoma dua kwa pamoja, hupinga muandamo wa mwezi wao wanafuata mwezi wa Saudia arabia, hupinga kuwasomea Maiti Qur'an na dua ya Kaburini, hupinga mwanaume kuvaa kanzu ndefu, wanahimiza ufugaji wa ndevu kama sunna ya mtume s.a.w, wao ndio hujihusisha na uchezaji wa kareti, na makundi mengi ya kigaidi yamehusishwa na Uwahhaby kwasababu wao hufundisha zaidi itikadi (Tawhid) katika kumpwekesha Mwenyezi MUNGU. Kwa ufupi ni watu wenye misimamo mikali katika dini, na mambo mengi katika uislamu wameyakanusha.
 
Back
Top Bottom