Mubashara: Maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM

Mubashara: Maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka uwanja wa Karume - Musoma mkoani Mara katika maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi. Kaulimbiu ya maadhimisho haya ni "CCM Imara, Shiriki Uchaguzi Kwa Uadilifu."

Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Samia Suluhu Hassan.

Pia maadhimisho haya yataambatana na uzinduzi wa kadi za uanachama wa CCM za kielektroniki, maonyesho kutoka halaiki/chipukizi, burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Alikiba, Dulla Makabila, Hamadai, Sholo Mwamba na wengineo sambamba na mambo mengine mengi.

Fuatilia matangazo kupitia kiunganishi hiki



FK0wEEXWUAMqxjx.jpeg
 
Hizi kadi za Kielectronic zingekuwepo tangu zamani Chama chetu kingeweza kuzuia kuwa na Katibu Mkuu toka CUF na Katibu wa Itikadi na Uenezi kutoka kwny NGO ya Femina

CCM bila ya wahamiaji haramu inawezekana
 
Mukumbushane pia chama kina miaka 45 madarakani ila maendeleo kwa wananchi wake ni hafifu.

Chama bado kinashindwa ata maliza tatizo la maji au madawati kwa shule.

Ccm ni ile ile, tumeipenda wenyewe, chaguo letu wenyewe
 
Baba Askofu hongera kwa ibada nzuri sana. Nimekusikiliza na tumesali pamoja. Mwenyezi Mungu aendelee kuidumisha amani iliyopo, na watawala watawale kwa haki na kwa umoja.

Hongera pia Kagibu Mwenezi, Kaka yangu Shaka. Upo vizuri pia.
 
Miaka 45 lkn chama kimeshindwa kujenga ofisi zake tena hapo bado na ile miaka mingine ya Tanu na Taa.

Wameng'ang'ania tu kwenye ofisi za serikali sasa sijui siku wakibanduliwa madarakani watakuwa mgeni wa nani.

Ni yale yale yaliyowakuta Kanu kule Kenya, Unip kule Zambia na UPC kule Uganda ambao leo havina hata ofisi baada ya kutimuliwa kwenye ofisi za serikali walizokuwa wametwaa kibabe wakati walipokuwa madarakani.

Ccm needs to borrow a leaf 🌿 from those moribund political parties, who like ccm, had a dream that they could rule their respective countries forever before the dream was shattered.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anashiriki katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ikiwa ni miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho. Sherehe hizo zinafanyika Mkoani Mara, Leo Februari 05, 2022.

Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Samia Suluhu Hassan.
 
Hapo kwny neno ujinga weka umakini

Kama vyama vingekuwa vinakodishwa kutawala CCM ingekuwa ina maombi mengi sana ya kuombwa kuongoza Mataifa mengi sana ya Africa

Nani katika Africa hataki kutawalila na Chama kinacholinda Amani?
Kwa ujinga tulio nao bara CCM bado ina miaka 100 ijayo
 
Sisi wakazi wa kingolwira majengo mapya (mtaa wa bomba la mafuta).

Kuna miundo mbinu ya maji iliwekwa zamani na miradi ya Mh Mariam ditopile ambayo ilifika kwetu na maji tulikuwa tunapata vizuri tu hadi april mwaka jana 2021.(sisi tunaamini before JPM passing).

Yalitoka vizuri iwe mvua liwe jua.ila kwa sasa hatupati maji .

Toka august mita zetu hazisomi maji tunauziwa na bowser kwa sh 20000 kwa lt 1000 kwa vile huku ni mbali.(inatugharimu).

Mwanzo tuliambiwa ni ukame, mvua imenyesha tunaambiwa ni matope,

Ajabu ni taasisi za karibu tunaotumia mradi hii ya karibu karibu yaani maeneo ya chem chem ya mlima yaani magereza, jeshi na mkambarani hadi mikese wao hawakuwa na kadhia hii, Jeshi la pangawe wanauza masaa 24 mabomba 4 na utokaji ni presha nzuri sana.ajabu sisi tulio chini ya mlima wa jeshi hatupati ni IMANI pamefungwa mahali kututaabisha.

Sisi tunaambiwa ufumbuzi ni kuusubiria mradi wa mwindu, mazimbu, lukobe, yepsa , tungi na kingolwira ufike.

Tunachokiona moja SSH anahujumiwa.watu kauli zao ni kabla yalitoka ila baada ya kutenguliwa mkurugenzi wa moruwasa hatupati maji.

Pili, Diwani ni magumashi ni mbabe na watu tunamuogopa.
Tatu mkuu wa wilaya amekagua sana vyanzo vya maji lakini waliandaa mabomba na kumwambia wanabadili mradi wa zamani kwenye ule mradi aliowahi simamia Ditopile.

Sasa mvua zinanyesha hatujapata hata tone na ni wiki ya pili mvua zinanyesha.
 
Matajiri wanaotuzunguka wanaongozwa na Republic au ANC?

Kuna Wakinga wengi tu wamezaliwa Masikini lakin leo hii ni matajiri kwa viwango vya kuridhisha

Fanya kazi kwa juhudi na maarifa na punguza lawama…kila changamoto ni fursa ya kukutajirisha
Kuna taifa linataka kuletewa umasikini na CCM zaidi ya Tz?
 
Matajiri wanaotuzunguka wanaongozwa na Republic au ANC?

Kuna Wakinga wengi tu wamezaliwa Masikini lakin leo hii ni matajiri kwa viwango vya kuridhisha

Fanya kazi kwa juhudi na maarifa na punguza lawama…kila changamoto ni fursa ya kukutajirisha
Mpuuzi wewe, Iringa kuna matajiri sn?
 
Ngoja kwanza nijitibu hang over za chupa za jana.
 
Back
Top Bottom