Siku 30 HAZITOSHI, hata Kama una pesa yote.
Mchanganuo wangu upo hivi, Kama una mafundi wazuri na wapo makini;
- Msingi siku 6(kuchimba na kumwaga zege chini siku 1, kujenga Msingi siku 2, na kupinga mkanda siku 1, siku 1 ni kumwagilia na kuacha mkanda kukomaa vizuri ili nyumba ije ikae juu, kujaza Mchanga ndani siku 1)
- Nyumba siku 9(course ya kwanza hadi ya 11 siku 5, lintel siku 1, siku 1 ni kuacha ikauke vizuri, course 3 za juu ni siku 2)
- Bati siku 6(siku 2 mbao, siku 3 bati na siku 1 blunder)
- Grill siku 1. Ila unatakiwa kuanza kuandaa grill pindi unapomaliza boma.
- Umeme/wiring siku 3
- Plumbing siku 3
- Plaster siku 5
- Mkeka siku 1
- Gypsum siku 3
- Skimming siku 4(hapa ndio kuna uchawi, wafanya kwa utaratibu na umakini ili nyumba ije kuvutia, pia utaskim gypsum)
- Tiles siku 3
- Windows installation siku 1
- Colouring siku 4(hapa pia Usiwe Sana na haraka, pia utapaka rangi gypsum)
- usafi na kuweka sawa nyumba siku 1
N.b; kazi ya septic tanks ifanyike sambamba na wakati wa kujenga boma, gawanya mafundi wengine wachimba shimo na kuanza kulijengea huku wengine wakiendelea na boma.
Hadi hapo ni siku 50, na kumbuka hapo watu lazima wawe wengi kidogo. Na hapo ni kazi inaenda haraka sana.
Nakusisitiza hapo Ni endapo una mafundi wengi na wapo speed na wapo makini.
Ukisema utumie chini ya siku 50 Kuna sehemu utakuja kulia.
Wanaokuambia siku 30 zinatosha ni waongo wakubwa Sana.
Nimekushauri nikiwa Kama mtaalam mbobezi wa masuala ya ujenzi na pia ni civil contractor.