Muda (Kilometre) wa kubadilisha Automatic transmission fluid (ATF)

tamsana

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2012
Posts
3,739
Reaction score
8,044
Habari ya majukumu wadau.
Baada ya kuagiza gari used kutoka Japan ilipofika nchini nilibadilisha engine oil na ATF. Kwa maelezo ya wataalam (garage) ambako nilifanyia service walinishauri kubadili ATF baada ya kutembea angalau 50k kilometres.
Hadi sasa nimetembea 20k kilometres na kwa sababu sio mtaalam wa magari ningependa kupata ushauri kwa wadau humu kuhusu muda mahususi wa kubadili ATF.
Naomba kuwasilisha.
 
Kama waliiekea dextro 3 ATF, unaeza iacha hadi hizo kilomita. Ila ningekushauri ubadili ifikapo 30k km kwa ajili ya ulinzi wa engine yako na efficiency ya gari
 
Asante sana mkuu. Kabla ya kutumia niliweka oil recommended ya subaru na nimejaribu kusoma mitandaoni wameandika unaweza kubadilisha baada ya mile 30k ambayo ni sawa na 48k. Lakini kwa sababu ya mazingira ya barabara zetu nitazingatia ushauri wako wa kubadilisha baada ya 30k.
 
Hapo ndipo tatizo linapoanzia. Oil ya giaboksi inayokuja na gari ni nzuri sana. Wengi waimwaga inapofka hapa TZ na unajaza oil fake ya bongo
 
Gari gani?

Kama Yota, wameandika kabisa, No need to change ATF under normal driving conditions.

Nishawahi muuliza fundi wa Yota akasema under normal driving conditions wanamaanisha chini ya 5 hours per day per week.

Kwahiyo ulibugi apo ulipoanza kubadirisha.

Kama Yota weka Type IV hafu acha milele.
 
Mkuu kwa hiyo kila kinachopatikana bongo ni fake. Anyway mimi sio mtaalam wa magari lakini naamini kuna wakati inatakiwa kubadilishwa hata ukiacha inayokuja na gari.
Asante kwa ushauri though!
 
Hivi ni kwa nini mtu mweusi huwa hasomi manual ya gari?Tatizo ni nini?

Ili gari yako iwe salama unahitaji kufanya mambo yafuatayo:

1.Kusoma manual yote ya gari na kuielewa na kuizingatia

2.Kuwa na fundi wa uhakika ambae alienda shule na akafuzu masomo yake.

3.Kuzingatia vifaa original wakati wa service.

4.Wewe mwenye gari unapaswa kuwa fundi namba moja na fundi wa garage kuwa fundi namba mbili.(Hapa maana yake unapaswa kujifunza juu ya magari na kuyaelewa mechanically)
 
Gari gani?

Kama Yota, wameandika kabisa, No need to change ATF under normal driving conditions.

Nishawahi muuliza fundi wa Yota akasema under normal driving conditions wanamaanisha chini ya 5 hours per day per week.

Kwahiyo ulibugi apo ulipoanza kubadirisha.

Kama Yota weka Type IV hafu acha milele.
Ikichoka itaanza ku slip gears! Au rpm zinakuwa juu sababu gear changes zinachelewa kidogo so inakuchapa kwenye efficiency drop ya mafuta na pia uta experience jerks!

Chomoa dipstick ya ATF kisha nusa ukiskia burnt smell jua imechoka badili!
 
mie huwa nafahamu ni 3:1 Engine oil kwa ATF respectively
Kwahio unabadiligi badiligi kila mara? Hio gari ni basi la mkoani kwamba linasafiri kila siku? Hebu tuache ujuaji utakuja wekewa atf feki siku moja ukaange clutch za gearbox.

Gearbox ni kitu sensitive sana hakitakiwi kuchezewa chezewa
 
Gari gani?

Kama Yota, wameandika kabisa, No need to change ATF under normal driving conditions.

Nishawahi muuliza fundi wa Yota akasema under normal driving conditions wanamaanisha chini ya 5 hours per day per week.

Kwahiyo ulibugi apo ulipoanza kubadirisha.

Kama Yota weka Type IV

Hivi ni kwa nini mtu mweusi huwa hasomi manual ya gari?Tatizo ni nini?

Ili gari yako iwe salama unahitaji kufanya mambo yafuatayo:

1.Kusoma manual yote ya gari na kuielewa na kuizingatia

2.Kuwa na fundi wa uhakika ambae alienda shule na akafuzu masomo yake.

3.Kuzingatia vifaa original wakati wa service.

4.Wewe mwenye gari unapaswa kuwa fundi namba moja na fundi wa garage kuwa fundi namba mbili.(Hapa maana yake unapaswa kujifunza juu ya magari na kuyaelewa mechanically)
Mkuu manual huwa zinaswomwa lakini wakati mwingine hazielezi kila kitu. Mfano kwenye manual ya subaru wameandika kuwa ATF unatakiwa kuongeza ikiwa imepungua kulingana na vipimo ambavyo wameweka. Suala la kubadilisha halijawekwa kwenye manual kabisa.
Sasa mimi naamini kuwa pamoja na kutowekwa maelezo ya kubadili ATF kwenye manual sio sababu kuwa huwa haibadilishwi. Uzuri ni kwamba, japo hawajasema kama inatakiwa kubadilisha, ila wameweka recommended ATF in case ukitakiwa kuongeza kama ikipungua kulingana na vipimo walivyovianinisha.
Ni kweli wengine hawasomi lakini ukipata nafasi ya kumsaidia mtu na kwa kuwa wewe umesoma inakuwa advantage kwako kusaudia muhitaji.
 
Mkuu kama hawajasema kuwa inatakiwa kubadilishwa na wewe umebadilisha basi huna gear box hapo.

Magari mengi huwa hawaruhusu kabisa kubadili oil ya gear box,hadi mengine yameandika kwenye dip stick.Kama manufacturer amesema kuwa ikipungua ongeza basi hicho ndicho kilikuwa cha kuzingatia.Hakuna kitu muhimu na chenye tija kama manual.Unatakiwa utii ambacho manual inaelekeza.

Sasa wewe unapomsikiliza fundi au akili zako badala ya kuisikiliza manual ina maana fundi/akili zako ni zaidi ya manufacturer wa gari?!
 
Sawa mtaalam.
Ila hilo la kusema nimeharibu gear box naweza nisikubaliane nalo (umeandika kivitisho zaidi ya utaalam). Naenda mwaka wa pili sasa chuma iko njema sijawahi kupata any fault isipokuwa kubadili engine oil. Kama manual inatuhusu kuongeza tena recommended ATF ina maana hakuna impact yoyote inayoweza kujiuokeza katika kubadilisha.
Anyway, nashukuru sana kwa ushauri na utaalam wako, naamini utasaidia wadau wengine pia wanaosoma uzi huu.
 
Sawa mtaalam.
Ila hilo la kusema nimeharibu gear box naweza nisikubaliane nalo (umeandika kivitisho zaidi ya utaalam).
Hiyo ni fact na wala siyo kitisho kwamba kama manufacturer anasema ongeza ATF na wewe ukabadilisha, maana yake umeenda kinyume na manufacturer na matokeo yake ni kuua/kupunguza life span ya gearbox yako.
Naenda mwaka wa pili sasa chuma iko njema sijawahi kupata any fault isipokuwa kubadili engine oil.
Kupunguza life span ya gearbox siyo lazima upate madhara saa hiyohiyo.Ni ishu ya time.
Kama manual inatuhusu kuongeza tena recommended ATF ina maana hakuna impact yoyote inayoweza kujiuokeza katika kubadilisha.
Kubadilisha ATF na kuongeza ATF ni vitu viwili tofauti vyenye matokeo mawili tofauti.
Anyway, nashukuru sana kwa ushauri na utaalam wako, naamini utasaidia wadau wengine pia wanaosoma uzi huu.
Shukrani nzuri na yenye faida ni kuzingatia manual ya gari yako.
 
Hakuna ATF isiyobadilishwa ktk gari.
ATF huongezwa endapo tu imepungua.
ATF hubadilishwa pale endapo imechoka, na hutoa ishara kadhaa pindi ikichoka, ikiwemo kutoka kwenye wekudu na kuwa nyeusi au kijivu, pia huanza kuchelewesh gia kubadili, utajua hili kupitia RPM ya gari lako.
ATF hubadilishwa pia kwa idadi ya km zilizotembea, cha msingi ni kujua ni aina gani ya ATF itumikayo ktk gear box/gari yako amabayo huandikwa ktk dipstik ya gear box pale chini kama ni ATF TYPE IV/ ATF-WS, au CVT-FE/ CVT-TC. Hizi hubadilishwa kila baada ya 40,000km endapo utatumia og, bei yake ni kubwa maana sio za kopo la elfu 3,3.
Asikuambie mtu eti ATF haibadilishwi.
Pia inapendeza sana ukinunua gari iwe mkononi au from Japan, ni muhimu kubadili ATF ili uwe na uhakika wa km za service ya chombo chako na kuondokana na mashaka ya chombo chao.
Habari ya majukumu wadau.
Baada ya kuagiza gari used kutoka Japan ilipofika nchini nilibadilisha engine oil na ATF. Kwa maelezo ya wataalam (garage) ambako nilifanyia service walinishauri kubadili ATF baada ya kutembea angalau 50k kilometres.
Hadi sasa nimetembea 20k kilometres na kwa sababu sio mtaalam wa magari ningependa kupata ushauri kwa wadau humu kuhusu muda mahususi wa kubadili ATF.
Naomba kuwasilisha.
 
Hakuna ATF isiyobadilishwa ktk gari.
ATF huongezwa endapo tu imepungua.
ATF hubadilishwa pale endapo imechoka, na hutoa ishara kadhaa pindi ikichoka, ikiwemo kutoka kwenye wekudu na kuwa nyeusi au kijivu, pia huanza kuchelewesh gia kubadili, utajua hili kupitia RPM ya gari lako.
ATF hubadilishwa pia kwa idadi ya km zilizotembea, cha msingi ni kujua ni aina gani ya ATF itumikayo ktk gear box/gari yako amabayo huandikwa ktk dipstik ya gear box pale chini kama ni ATF TYPE IV/ ATF-WS, au CVT-FE/ CVT-TC. Hizi hubadilishwa kila baada ya 40,000km endapo utatumia og, bei yake ni kubwa maana sio za kopo la elfu 3,3.
Asikuambie mtu eti ATF haibadilishwi.
Pia inapendeza sana ukinunua gari iwe mkononi au from Japan, ni muhimu kubadili ATF ili uwe na uhakika wa km za service ya chombo chako na kuondokana na mashaka ya chombo chao.
Asante sana mkuu. Umeeleweka vizuri sana.
 
mie huwa nafahamu ni 3:1 Engine oil kwa ATF respectively
Hapa wewe umejiwekea formula yako mkuu watengeneza magari wengi wanashauri usibadilishe Atf Kama unaendesha in normal condition na hii normal condition ni ile gari haitembei zaidi ya masaa 24 kwa wiki na kwa mazingira ya hapa bongo ni ngumu gari nyingi kuendeshwa in normal condition badala yake unashauliwa ubadilishe atf kuanzia km 20elfu tu 30elfu
 
Back
Top Bottom