Muda mwingine Mwanamke hudanganya/ hukasirika ili kumjaribu Mwanaume, sio kwamba hapendi

Muda mwingine Mwanamke hudanganya/ hukasirika ili kumjaribu Mwanaume, sio kwamba hapendi

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Ni muhimu kwa mwanamke kumjaribu mwanaume. Ni njia yao ya kujilinda na kujua ujasiri wa mwanaume. Mwanamke hupima ujasiri wa mwanaume mara kwa mara.

Haijalishi we ni rafiki yake, mpenzi wake, baba yake au jirani tu. Sababu ndivyo alivyoumbwa. Anahitaji kujua haraka nani atafaa kuwa kiongozi kwake, nani amuonee, nani amchune au nani atafaa kuwa mpenzi wake. Sio jambo la kuwalaumu.

Ila wengi hawatambui pale mwanamke anapowajaribu. Mwingine anaweza kuona anadhalilishwa na mwanamke. Mwingine anaweza kuona mwanamke hamtaki. Mwingine anaweza kuona wanawake hawafai. Lakini mwanamke anakupima ili kujua kama kweli unamaanisha kile ulichokisema au unachokipenda au kweli we ni jasiri kama usemavyo. Je, kweli utasimamia ujasiri wako bila kuogopa kukataliwa?

Jinsi ya kujua majaribu.
Atakukejeli/ kukukataa lakini mwili wake unakukubali.
Angalia vitendo vya mwanamke. Anaweza akakuambia hakupendi au hajavutiwa na wewe lakini amekushika mkono, au anakuchekea chekea au nguvu zake zote zipo kwako. Kwa maneno anakukataa lakini vitendo vinaonesha anakukubali. Apo anakujaribu kama unajiamini mwenyewe? Au unataka mwanamke akuambie maneno mazuri ndo ujisikie vizuri?

Jibu lako au vitendo vyako inabidi vioneshe kuwa huyumbishwi na maneno yake.

Atakupinga katika kitu unachokiamini kwa moyo.
Anaweza kukununia kabisa. Anataka ajue kama anaweza kukuyumbisha, kama utabadili mawazo kumfuata yeye.

Utabadili mawazo ili kumfurahisha. Utabadili mawazo ili akupende. Utabadili mawazo ili asikuache au utabaki na unachokiamini. Mfano, kuna mwanamke nilikua naye, tukaanza kuongea mada kuwa mwanaume akiwa kiongozi mzuri wa mahusiano, mahusiano yanakua mazuri.

Akacharuka hapo hapo, na kuonesha kukasirishwa kuwa mwanaume anataka kuwa kiongozi ili amnyanyase na kumkandamiza mwanamke, akataka nibadili ninachokiamini, na akakazia kwamba “sisi wanawake tunajiweza, sisi ndo inabidi tuwe viongozi angalia hata raisi wetu ni mwanamke”. Nilicheka tu, na sikutaka kubishana naye nikajua tu anadanganya kunipima mana muda wote tuliokua pamoja amekua akifuata uongozi wangu na kuukubali uongozi wangu kwake.

Mifano mingine.
Mnaweza kuwa mmekubaliana kukutana alafu muda kabla ya kukutana anakutafuta kuwa hatoweza kuonana na wewe, na sababu zake hazieleweki. Wala usitake kumbembeleza, mwambie tu tutakutana muda tuliopanga.

Mwanamke anaweza akakuambia nataka mwanaume ambaye atakua ananipigia simu kila saa. Lakini ukimfanyia ivo anakuchoka haraka.

Mnaweza kuwa mnaongea kuhusu vitu mnavyopenda, ukamuambia unapenda Vanguard alafu ghafla muda huo huo akanuna na kuiponda Vanguard na kukazia kuwa hawezi kuwa na mwanaume mwenye Vanguard ye anapenda Rav 4 na mwanaume anayependa Rav 4 ndio atampa chochote. Usije kubadili mawazo na kuanza kujitetea zamani ulikua unapenda Rav 4 ili upewe penzi, ila mwache na wazo lake we simama kwenye lako.

Muhimu ni kujua kuna muda mwanamke atakujaribu tu, kujua we ni dhaifu au jasiri. Na akijua sehemu fulani una udhaifu ataendelea kukubania hapo hapo.

Ukiona unabadili badili mawazo ili yafanane na mwanamke ujue unafeli majaribu yake. Na ukiona kila anachokisema/ anachokifanya mwanamke kinakukasirisha au kinakufanya umbembekeze mara kwa mara ujue unafeli majaribu yake.

Njia nzuri ya kuyapita majaribu yake ni kupotezea akisemacho/ akifanyacho. Lakini ni muhimu ujue kutofautisha majaribu na matatizo/ wasiwasi/ changamoto ya mwanamke mana muda mwingine yanafanana kwa mbali.
 
Mwanamke usinijaribu kwasababu sina muda wa kujaribiana na wewe. Kichwa changu kina mambo mengi sana.
 
Hawa viumbe walishashindikana Toka enzi za Adam huko bustani ya Eden,Sasa nyie mnaojifanya mnataka kuwaelewa wanawake endeleeni kupoteza muda.

Mimi huwa namtokea mwanamke Mara Moja tu, akianza kupindisha pindisha ajue ndo imetoka hiyo, hatokaa anione Tena.
 
Back
Top Bottom