MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Mwaka 2024 ungefanya majadiliano na makada wa CCM na Maafisa Usalama wa Tanzania kwamba kuna siku watanganyika wanaweza kufanya vurugu za kutisha, na serikali kufanya mauaji makubwa ya kutisha kwa raia wake, wanufaika wakubwa wa mfumo kama Kikwete, Rostam, Harbinder, pamoja na walinda malango wa mfumo kama Mkuchika, Luhavi, Mombo, Sirro, Mafwele, Nkunda, Makonda na wengine wangekucheka na hata kukuita mwendawazimu. Hayo mambo yaliaminika ni ya Rwanda, Kongo, Somalia, Kenya, Burundi na Sudan, sisi watanzania amani ni haki yetu ya kuzaliwa hivyo hayawezi kabisa kutokea.
Mwaka 2020 ungeonana na kina Humprey Polepole, Bashiru Kakurwa, John Kijazi, Diwani Msuya na wafuasi wao wengine, na kuwaambia kwamba huu uchaguzi ambao mnatumia nguvu sana kuuvuruga na hii mifumo mnayoitengeneza itakuja kuwaumiza na Raisi Magufuli hawezi kuvuka 2021 ungeonekana Mwendawazimu. Nakumbuka mwaka 2019 kuna Mzee aliwahi kuniambia kwamba Uchaguzi wa 2020 hautakuwa na vurugu kwasababu pande zote hasimu zina cha kupoteza, na wanafahamu fika kwamba wakilianzisha basi wanaweza wakamshindwa JPM kwasababu alikuwa ni mtu asiyeogopa kumwaga damu. Raisi kufia madaraka ni jambo ambalo Tanzania lilikuwa haliwaingii kabisa kichwani watawala, zaidi-zaidi raisi kufariki kwa kifo chenye utata. Ugonjwa mkali kuwaruka watu wa MBAGALA na kumfikia yeye aliyekuwa kwenye SAFE-ZONE QUARANTINE.
Aliniambia vita ya JPM itakuwa baada ya uchaguzi, wakati ametulia, amejisahahu na kudhani kwamba ameshashinda kabisa vita hapo ndipo atashambuliwa vibaya. Huu ni wakati mzuri kwasababu joto la uchaguzi huwa linakuwa limeshuka na kile kohoro na kimuhemuhe cha ushindi kinakuwa kimewakaa watawala kichwani. Kama ambavyo alisema Shakespeare "Beware of the Odes of March" JPM alichomoka, na hakuna aliyeamini mpaka leo. Mimi niliposikia nikaona labda huyu Mzee anasema tu, lakini yalipotokea alikaa kimya na katika kumuuliza kwangu hajajibu mpaka leo kama hakuwahi kuongea na mimi. Nilifahamu kwamba kuna watu WAKO MBELE YA MUDA.
=============================================================================
Kuna msemo uko kwenye kitabu cha "The Art of War" ambapo Sun Tzu aliandika hivi "After Crossing the river, you should get far away from it". Jambo ambalo MAMA YENU na wenzake halijawaingia vizuri kichwani. Wameshavuka mto, lakini bado wamejenga mahema kwenye ukingo wa mto.
Mwaka 2021, mwezi MAY, ungemfuata Membe, Makamba, January, Nape, Rostam, Ridhiwani, Kikwete na kuwaambia kwamba kufika MAY 2026, watu wataikumbuka Tanzania na JPM na kutamani hata ule ukatili wake urudi kuliko hii serikali yenye matumanini ambayo imegeuka kuwa serikali inayochukiwa na kudharaurika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, sidhani kama kuna mtu angeamini. Ungemwambia Membe na January, binadamu ambao walikuwa na tamaa kali ya Uraisi wa JMT, kwamba miaka michache ninyi mtageuka kuwa wahanga wa hii serikali ambayo mnaamini uwepo wake ni tiketi zenu kisiasa, basi wangekuona una wazimu na kichaa. Membe na Makamba, walivuka mto, lakini bado wakajenga mahema kwenye ukingo wa mto (YAKAWAKATUKA WOTE)
Wachache ndani na nje ya mfumo mbali na kumchukia JPM, walipovuka mto waliondoka kabisa lile eneo na kufahamu hatari yake. Marehemu Lukuvi mbali na madhaifu yake, alikuwa moja kati ya watu waliousoma mchezo wiki chache tu baada ya JPM kufa, kwamba nchi inaenda kupoteza mwelekeo. Mbali na ujehuri (Kidada cha kihehe), tamaa za kupenda fedha na roho ya choyo, Lukuvi was an extemely competent and effective bureaucrat. He understood how systems work. Alifahamu fika kwamba MAMA YENU is a bad Gambit. Alivuka mto, akaenda mbali ya ukingo, lakini tamaa zikamrudisha pale-pale. Angekuwa na hekima angestaafu, maana alikuwa na ukwasi, heshima na mali. (YAKAMKUTA)
Mwingine ni Tundu Lissu, alimsoma MAMA YENU mapema kabisa na kumpa jina Malkia Mdanganyifu Mwenye Maneno Mazuri. Aliingia kwenye mtafaruku mkali, lakini huyu ni moja kati ya binadamu wachache mno hapa nchini Tanganyika mwenye uwezo wa kuyatazama mambo kama yalivyo, hata kama ni machungu. Hii sifa watanganyika asilimia 99% hawana. Bwana amevuka mto, na akaondoka kwenye ukingo. Mpaka sasa kuna jitihada za kumrudisha ukingoni lakini hazijafanikiwa.

Mwezi April 2022, akipokelewa Marekani na wabunge na msululu mkubwa wa vigogo wa dunia, MAMA YENU ungemwambia kwamba kuna siku hawa hawatataka kuzungumza nawewe asingekuamini. Marekani alipokelewa na Makamu wa Raisi Kamala Harris kwa bashasha na upendo. Kwenye mkutano wa WTO na IMF alipokelewa na Kristalina Gorgieva kwa kumbato kubwa la upendo. Akapokelewa na Ngozi Okonjo-Iweala kwa furaha kubwa mno. MAMA YENU, wafuasi wake na dunia ikaamini kwamba yeye ni viwango vya kina Kamala Harrs, Kristalina Gorgieva, Ngozi Okonjo-Iweala na Mia Motley. Lakini mwaka 2026 inakuwa ngumu kuamini kwamba MAMA YENU yuko kiwango kimoja na wahuni wa ukanda huu kama Rutto, Musseveni, Kagame, Munangagwa na Tinubu.
===================================================================================
Jambo ambalo wenzetu wa Magharibi walipewa NEEMA NA MUNGU kulichunguza, kulifahamuni, kulielewa na kuliheshimu sana ni suala zima linaloitwa MUDA. Hii ni rasilimali ya bure ambayo hairudi mara mbili. Hii rasilimali huleta kitu kinachoitwa MABADILIKO (Changes). Kitaalamu hakuna mwanadamu ambaye anaweza kupinga mabadiliko. Awe MWEMA au Awe MBAYA, lazima atakutwa na MABADILIKO.
Wenzetu wazungu walichotushinda ni hapa tu: NIDHAMU KWENYE MUDA, kwasababu wanafahamu muda huleta kitu kinachoitwa MABADILIKO katika nyanja zote za maisha: Binafsi, Kijamii, Kisiasa, Kiroho, Kiuchumi na Kitamaduni. Hivyo basi kuweza kukabiliana na MABADILIKO yanayoletwa na MUDA, wenzetu wakabuni kitu kinaitwa MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLANNING). Wenzetu walifahamu kwamba hawawezi kuzuia MABADILIKO lakini wanaweza kuyaratibu (MANAGE). You cannot stop changes, but you can manage and mitigate them.
================================================================================
Tanzania tumefika hapa tulipo kwasababu ya haya yafuatayo:
1. Hatutambui kwamba MUDA (An Independent Unit) ni rasimali inayoshikilia rasilimali zote.
2. Hatuukomboi MUDA/WAKATI (Sisi ni bora liende, ponda mali kufa kwaja)
3. Mabadiliko yanayoletwa na MUDA/WAKATI huwa yanatukuta tumelele usingizi wa pono.
4. Tunaamini kwamba utajiri wa nchi ni rasilimali watu na rasimali asilia pekee.
5. Hatufahamu kwamba, kama binadamu taifa nalo lina MUDA wa kuishi na kufariki.
Ndiyo maana wenzetu baada ya kufahamu haya, wakaanzisha taasisi za PREDICTIVE SCIENCES ambazo zina wataalamu ambao kazi yao kubwa ni kuweza kutengeneza PREDICTIVE MATHEMATICAL MODELS zilizojikita kwenye Wealth (Economy), Health and Weather ambayo wanasayansi wanaviita viashiria vikubwa mno vya maisha ya binadamu kwa miaka ijayo. Mwaka 2007, Prof David Orrell alindika kitabu kiitwacho "Apollo's Arrow: The Science of Prediction and The Future of Everything" ambacho kimechambua vitu vingi sana na kuonesha jinsi gani MABADILIKO yanaweza kumvamia binadamu hata yule ambaye amejipanga vizuri kwa kutaka kutabiri nini kitatokea.
Hichi kitabu kilileta ushawishi mkubwa sana nchini Marekani, hadi kupelekea baadhi ya vyuo vikuu na taasisi kukifundisha kama kozi maalumu na hata baadaye idara nyeti za nchi zikaanza kufuatilia mapendekezo yake. Ukweli mchungu hata ambao Proff David Orrell anasema kuhusu MABADILIKO ni kwamba huwa hayagondi hodi. Akitolea mifano mingi kama Venezuela ya Hugo Chavez na majanga ya hali ya hewa yaliyoikumbwa nchi hiyo mwaka 2001. Kitu kama hichi msomi Philipp Coggan ambaye ni mchumi na mwandishi wa habari nguli kutoka The Financial Times/The Economist anasema kwamba huwezi kubashiri uchumi kwa asilimia 70% sahihi, mabadiliko huja bila hodi.
=================================================================================
Hivyo nini kifanyike hata kama hatuwezi kubashiri kwa usahihi nini kitakachotokea ???
Ni lazima tujipange, ili MABDILIKO yakifika tusichanganyikiwe na kuleta taharuki. Watawala wasiokuwa na ufahamu na uelewa huwa wanajidanganya kwamba watazuia mabadiliko. Kilichotokea 29 OKTOBA 2025 ni sehemu ya mabadiliko. Bahati mbaya serikali haikujipanga endapo jambo kama lile lingetokea, ikaadhimu kuua watu wake kikatili kwasababu ilichanganyikiwa (Panicked) kwasababu ilikutwa imelela usingizi wa pono.
Hili la vikwazo limewakuta vibaya, mmelala kwenye ukingo wa mto. Sasa imetokea taharuki kubwa ambayo badala ya kupunguza tatizo, inaonesha wazi kabisa kwamba serikali haina mbinu mbadala zaidi ya kuhonga madini na rasilimali. Hatujajipanga, na tumelela kando ya mto.
Hebu fikiria ikatokea kweli Marekani imepitisha ule MUSWADA kuwa sheria. Tanzania mmejipanga namna gani kukabiliana na hizi changamoto ??? Binafsi nasema ombeni sana isitokeaa, maana ikitokea, sijui aiseeeh.

ENIWEI najua mada hii ni ngumu, lakini naamini wahusika wataelewa nachokisema.
Lakini ombeni sana maana yajayo yanafurahisha.