Muda ni Mwalimu mzuri sana: Siasa ni kama upepo, hubadilika wakati wowote

Madini tupu haya
 
Mkuu fanya kutoa na effects matokeo kwetu sisi raia wa kawaida iwapo mswaada wa USA utapita. Tujue namna ya kujipanga mapema
 
Mkuu naunga Mkono hoja zako zote.

BUT napenda niongeze pia hata Wananchi bado nao hawajajiandaa na mabadiliko yanayoendelea Tanzania.

Hili la USA na Serikali ya CCM acha tuone mwisho wake.
Mtanzania wa kawaida hajui hata analipaje kodi kwenye kila bidhaa.

Hajui hata deni la taifa likikua lina impact gani kwenye maisha ya kawaida

Mtanzania wa kawaida hajali mtoto au mjukuu wake ataishije ili mradi kuna uwezekano wa kula milo miwili na kulala kwenye nyumba ya mbavu za mbwa. Kiufupi umaskini unamfanya mtanzania aishi hand to mouth kwa hiyo ni ngumu kuifikiria demokrasia ama macro problems ilhali tumbo ni tupu

Mtanzania wa kawaida anafikiri kazi ya serikali ni kutoa basic social services tena kwa ihsani na si kwa kufikiri ni haki yao, kutokana na utaifa na kodi zao "naomba serikali itusaidie kupata maji"

Mtanzania wa kawaida anaangalia kitu kinachomuathiri directly ndio maana kunaripoti ya CAG haikuwauma kama kuchomwa vituo vya mwendokasi na wakati, hizo pesa zinazopotea zinatosha kujenga vitu na kushusha bei ya usafiri mkoa mzima

Kiufupi mtanzania ni mtu unaetakiwa kuongea nae kama hajui anachokitaka na umtafunie kwa lugha nyepesi inayoakisi maisha yake.

Hiki ndicho kiini cha mafanikio ya Magufuli na Mange Kimambi. Wanaweza kuiongea lugha ya maskini kwa ufasaha hata kama wao wanaishi kwenye mansion
 
Naomba nimnukuu MTAZAMO kwamba hakuna taifa linaloshinda vita yoyote likiwa limegawanyika.

Ukiona taifa liko vipande vipande haliwezi kushinda chochote.

Ukipitia mitandao ya kijamii unaona picha halisi ikitokea vita /vikwazo/vifo vya wakandamizaji wa wananchi mapokeo yao ni yapi.

Guess what? Msigwa na wenzie wanasema hizo account ni feki na mtu mmoja anatengeneza account 200 uhalisia hali ni mbaya lifuatalo baada ya October 29 najua litaacha fundisho kubwa sana .
 
Uko vizuri mkuu sana,hii ni sawa na Ile ndoto ya mfalme Nebukneza kwenye kitabu cha Daniel (Biblia)! Daniel akamwambia Mfalme Nebukneza,uliota ndoto ya jitu KUBWA ambalo Lina kichwa cha dhahabu,kifua cha chumba,miguu na nyayo ni Udongo na chuma,Kichwa cha dhahabu ni Wewe mfalme na ufalme Wako, Baadae zitatokea falme zingine badala Yako!Akafurahi na hakuchukua hatua, mwisho wa siku kweli zikatokea falme zingine.
 
Dharau kwa wananchi na kuendelea kuamini kwamba watanzania hawa ni sawa na wale wa enzi za kidumu, zimepelekea na zitaendelea kuwangamiza kwa kuwa hadi sasa hawataki kubadilika kama unavyosema.

Husemwa," kama hutaki mabadiliko,mabadiliko, yatakubadilisha, Dunia imejaa mifano mingi ya mamlaka na taasidi ambazo lro zimefutika kwa sababu ya kuyakataa mabadiliko.

Wameshindwa kubadilika na kuendelea kuwadharau wananchi wakati kila kitu kimechorwa ukutani na bahati nzuri anayechora ni wao wenyewe.

Kuendelea kudanganya mambo yaliyodhahiri na ukategemea hao watu watakuamini kwa sababu wewe ni mwenye mammala kama ilivyofanyika miaka dahari iliyoputa ukitegemea itafanya kazi hata sasa ni kuyakaa mabadiliko.

Wenye mamlaka wanakula keki yote ya taifa huku wanaostahili kunufaika wakitupwa nje ni dalili mbaya ya kuyakataa mabadiliko.
 
Huwa huji wala kuandika mara kwa mara kwenye jukwaa hili iwe ni komenti au kuanzishwa mada..

Lakini, ukitokeaga tu, basi huwa unakuja na hoja fikirishi sana, yenye uchambuzi na mtazamo wa kisomi kwelikweli..

Asante kwa andiko zuri. Mimi nimejifunza na kukuelewa vizuri sana..

Sijui hizi robots@Tlaatlaah, Lucas Mwashambwa, Dr wa Manesi, Pascal Mayalla, Stroke and the likes kama wanaweza kusoma mpaka mwisho na kuielewa hii lecture kwa ufasaha...

Hawa wenzetu ni kama robots ambazo ziko programmed kutetea kila ujinga wa watawala..

Inawezekana hawawezi kukosoa. Lakini cha ajabu hawa wenzetu hata kushauri hawawezi...!

Oooh, God Yahweh, have mercy on us Lord...🙏🙏
 
Wewe ni mwehu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…