Muda pekee kwa wananchi kuwatumbua wanasiasa wao ni sasa

Muda pekee kwa wananchi kuwatumbua wanasiasa wao ni sasa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Fursa pekee aliyonayo mwananchi kwa mujibu wa katiba yetu wa kumuondoa na kumuweka madarakani mwanasiasa Ni huu Basi. Baada ya uchaguzi hakuna fursa hiyo Tena. Baada ya uchaguzi wanasiasa wanasahau kuwa watarudi Tena kwa wananchi kwa kusema na kufanya vitendo bila kujali vinakubalika au la kwa wapiga kura.

Mwananchi tumia nafasi kwa umakini mkubwa Sana maana ndiyo fursa pekee uliyonayo kikatiba ya kumtumbua mwanasiasa, baada ya uchaguzi wanasiasa wanageuka miungu watu kwetu.

Hakikisha unapiga kura kwa kuelewa unaempigia kura na unachopigia kura, baada ya hapo ni zamu ya wanasiasa walioshinda uchaguzi kwa kura yako wewe na Mimi. Hivyo usipange kukosa kwenda kupiga kura yako trh 28 Oct 2020. Anaekuhonga umpigie kura atakudharau Sana baada ya uchaguzi , na anaudharau uwezo wako wa kutafakari kwa kina.

Vitu vya kuangalia wakati wa kuchagua Ni:
1. Maslahi yako binafsi na familia yako na ndugu zako kwa miaka 5 ijayo. (maji, chakula, nyumba, shuka ya kujifunika, mavazi, elimu, afya, barabara, usalama, soko, pembejeo, kipato, nk)
2. Maslahi ya mtaa wako kwa miaka 5 ijayo.
3. Maslahi ya Kijiji, mtaa, kata, tarafa, wilaya na mkoa wako kwa kipindi Cha miaka 5 ijayo
4. Mwisho Ni maslahi ya Taifa lako kwa miaka 5 ijayo.
 
Mkifanya kosa la kuichagua CCM tena mtajuta.
 
Mkifanya kosa la kuichagua CCM tena mtajuta.
Tuichague ipi kwanini?

Issue wakati mwingine sio tusichague chama fulani Bali Ni tukichague chama gani kwasababu gani?
 
Back
Top Bottom