Muda sahihi wa kuanza clinic

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,171
Reaction score
34,394
Assalam alayqum, ni matumaini yangu mu wazima alhamdulillah

Jamani madokta wa jukwaa hili ninaomba msaada ni wakati gani mama au msichana akishajigundua yu mjamzito yafaa kwenda clinic? Kuna mtu ananambia niende mimba ikifika miezi sita mume anambia kesho asubuh inshallah niamkie huko lakini bado tukawa tunajiuliza je hospital nitakayoenda s ndio itakua hiyo hiyo kwa kipindi chote cha clinic kama Allah akinijaalia uzima? Au waweza pia jiandikisha kwengine clinic ukafanya kwengine kujifungua kwengine

Ni matumaini yangu humu sitakosa msaada
 
Jibu ninalo lkn ngoja madaktari waje kwanza. Wa kwetu mambo tayari? Basi vema. Unasalimiwa na Kiba...
 
Jirani hahahaa mwambie ntakuja aje nifunga mjongoo tayar bana na naumwa sio kawaida nijibu private basi
Jibu ninalo lkn ngoja madaktari waje kwanza. Wa kwetu mambo tayari? Basi vema. Unasalimiwa na Kiba...
 
Baada ya miezi 3 ya ujauzito

Madokta, Wauguzi na Wakunga mtanisahihisha hapa
 
Mitatu? Asante kwa hilo Mwifwa lakini iko hivi baada ya kujifatilia na kujiona siko normal jana ndio nimejua nimenasa sasa tukawa tunashauriana na hilo lilikiwa mojawapo ambalo ushanijibia sasa kwa mfano hospital nitakayorudi kesho s ndio hapo hapo natakiwa clinic nifanyie au naweza kwenda kwengine clinic kwengine sjui kama utakua umenielewa
Baada ya miezi 3 ya ujauzito
Madokta, Wauguzi na Wakunga mtanisahihisha hapa
 
Kwa kawaida unaanza kuuzuria clinic mara tu unapojigundua ni mjamzito tho wengi wao huanza kwenda wakiwa na miezi mitatu

Mimi nimeanza kwenda clinic mimba ina week tatu, na pale hospital walinipongeza sana.

Kingine siyo lazima pale unapoohuzuria clinic ndo ujifungulie

Lakini ni vema kama kuna hospital nzuri unayohisi ndo utaenda kujifungulia hapo uwende hapo hapo clinic.
Nilianzia clinic Agakhan na kujifungulia hapo hapo nilipenda huduma zao na kila kitu yani unahuduliwa vema vipimo vyote haxi siku ya kujifungua unakuwa na details za uhakika zinazomsaidia mzalishaji kukuhudumia.

Kila la heri fata la mume na day one mnaongozana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante dada

Ukweli luna hospital mume wangu amenishauri hata siitaki hata kuiona sio tu kuisikia na yeye ndio ametaka hapo sina namna asante umenijuza mengi skua najua

Inshallah nikiamka nitakwenda tu
 
Hilo halina tatizo, utoaji wa huduma ya Afya una utaratibu wake. Lazima pawepo na mashauriano kwanza baina ya mtoa huduma na mhudumiwa.

Mhudumiwa ana haki ya kukataa huduma anayotaka kupewa endapo pakiwepo sababu za kufanya hivyo, na mhudumu lazima akubaliane na maamuzi ya mhudimiwa, hapaswi kumlazimisha.

Sasa kwenda clinic uitakayo ni maamuzi yako, sio kwamba ukienda clinic ya kwanza ndio ubakie hapo hapo kwa huduma zote hadi ujifungue. Pia uzingatie ushauri wa Daktari au Mkunga jinsi atakavyokushauri, lakini ushauri wao una haki ya kuukataa.

Bila shaka utakuwa umenielewa...
 
Ndio kwanza mkoko unaalika maua, ya kwanza na mambo inanifanyia hata sina ham nina complications nyingi hakuna kitu kinakaa tumboni hata maji nayatapika mikojo ninayokoa mwanzo nikaogopa nikajua nina kisukari wallah
Mimba ya kwanza na ya tano sita saba ni sharti ujifungulie Hospital, mimba za pili tatu nne unaweza kujifungulia health Centre au dispensary so inategemea hiyo mimba ya ngapi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clinic inatakiwa kuanza mara tu mwanamke anapogundua ni mjamzito
Kuna huduma zitolewazo ambazo ni muhimu kwa mama mjamzito na kiumbe kinachotengenezwa.
Si lazima ulipofanyia clinic ndio ujifungulie
Lakini kuanza clinic mapema ni lazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clinic haina formula mwezi huu unaweza kwenda clinic aghakhan mwezi ujao temeke, mwezi ujao mbagala mwezi ujao Morogoro mwezi ujao kigoma hakuna tatizo


But kama upo settled sehemu moja ni vema ukachagua sehemu moja ambayo utaenda clinic na utajifungulia hapo.

Nakumbuka wakati ni mjamzito nilipata safari ya nje ya nchi na tarehe za clinic zikanikuta huko, nilienda huko huko clinic za kwao na niliporudi niliendelea huku kwetu.

Inshort nilienda clinic zaidi ya mikoa minne mana nilikuwa nasafiri sana hadi nakaribia kujifungua ndo nikawa nahudhuria aghakhan hadi mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa bila shida kaka angu nitaufanyia kaz ushaur wako
 
Asante dada

Ukweli luna hospital mume wangu amenishauri hata siitaki hata kuiona sio tu kuisikia na yeye ndio ametaka hapo sina namna asante umenijuza mengi skua najua

Inshallah nikiamka nitakwenda tu
Tafuta hospital nzuri namanisha nzuri sana, kama una bima au upo vizuri kiuchumi chagua hospital ya private ambayo utaanzia hapo clinic hadi kujifungua

Mimi nilipata complications sana ila nashukuru madokta wa pale walijitahidi sana.

Uzazi umekuwa changamoto ni vema wanawake tukachagua mahali ambapo uwakika wa huduma nzuri upo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu ni ujauzito wa kwanza nitajifungulia hospital kubwa clinic nitachagua nitafata ushaur mlionipa asanteni sana jamani
 
Na hilo pia ndio limenitia woga sometimes utajiona uko sawa kumbe kuna vitu havijakaa sawa hivo n muhim kuwah hospital haraka nimejipanga nikiamka salama niende kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…