Muda si mrefu Tanzania na Watanzania tutavuna tulichopanda kwa kukumbatia Katiba iliyopitwa na wakati

Muda si mrefu Tanzania na Watanzania tutavuna tulichopanda kwa kukumbatia Katiba iliyopitwa na wakati

Mbongo4life

Senior Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
132
Reaction score
270
Mjadala wa Katiba umekuwa ni suala la muda mrefu sana na watanzania walio wengi wanalichukulia ili suala kimasihara masihara lakini ukweli ni kwamba tukiendelea na hii Katiba muda si mrefu itatupatia dikteta wetu.

Katiba hii imempa rais madalaka makubwa mno , rais anauwezo hata wa kulivunja bunge liliochaguliwa kwa kura za wananchi kwa nguvu hiyo nini kingine anashindwa?

Maana kikatiba Bunge ndio muhimili wa wanyonge ,ndio mtetezi wa wanyonge . Sasa hivi kwa Katiba hii Rais akiamua kubaki madarakani milele nani wa kumzuia ?

Chief Justice mwenyewe anateuliwa na kutenguliwa na Rais, Mkuu wa Majeshi anawekwa na kuondolewa na Rais

Katiba imempa Rais mamlaka yasiyo na kikomo halafu basi hata akiondoka madarakani kwa Katiba hii hawezi kushitakiwa hata kama alifanya kosa gani hata akiua mtu hadharani hawezi shtakiwa.

Ebu watanzania tuwe serious kidogo huwezi mpa binadamu mamlaka makubwa hivyo na kutegemea maombi asitokee kichaa.
 
Back
Top Bottom