Muda tunaopoteza katika msururu/foleni za magari, Dar es Salaam

Sababu ni kwamba wale wote waliokwenda vacation mwaka mpya na christmas wamerudi.na wanafunzi wamefungua leo shule.na magufuli anachakarika na barabara zake.mpo.hapo?
 
Ahsante sana mkuu, nadhani inabidi ifike kipindi tuache haya magari yetu na mjini tuwe tunatumia alternative transport, maana Parking nayo ni changamoto nyingine.

Ni kweli mkuu.... Ni bora kutumia public transport kama bajaj na bodaboda ili kuwahi maana unaweza kukaa kwenye foleni ukiwa na private mpk ukatamani kuliacha gari ukapanda bodaboda ila ndo huezi!!!
 
Boda boda nazo zina shida yake, mwendeshaji anafundishwa asubuhi, anapakia abiria jioni..Pia Kofia ngumu za kichwani(Helmet) hazipatikani kwa wingi, na zinazopatikana haziko katika hali ya Usafi.
 
Ni wakati muafaka sasa kujitambua na kubadilika kwa manufaa ya jamii ya watanzania na maendeleo ya nchi yetu, nasema hili kwa sababu nami nilikuwa kama wengi wa wanaolalamika bila kutafuta suluhisho la kudumu, Dar ina tatizo la miundombinu muda mrefu na kila mmoja analifahamu fika, serikali imeshanyoosha mikono juu kutuhakikishia kuwa imeshindwa kupata suluhisho na hivyo imebaki ni kwa wajanja wachache kubuni vijimiradi feki vya kudai kuwa wanatatua tatizo la foleni huku wakijinufaisha na nyumba ndogo zao! Sasa basi, baada ya kumwaga utangulizi huo natoa suluhisho la kweli kwa maisha ya foleni za DAR, watu tuamue kutumia usafiri wa pikipiki na baiskeli kama mbadala wa haya magari yetu ya starehe tuendeshayo! Mimi natumia pikipiki, inahitaji kiwango cha kati mpaka cha juu cha adabu kuitumia katika jiji kama la Dar, kuwa makini na madereva wazembe, waenda kwa miguu na vyombo vyote vinavyotumia barabara huku ukiwa na vifaa vya kujikinga na hatari ya aina yoyote kwa suala zima la afya na usalama wa mtumia pikipiki! Najua kuna wataodhani ni utani lkn nakuhakikishia ukiweza kuwa mtumiaji wa pkpk kwa Dar basi utafaulu sana katika suala zima la kuokoa muda wako na wa mwajiri, hivyo kuongeza uzalishaji kwako na kwa mwajiri huku ukiiongezea nchi kipato na kukuza uchumi wetu hohehahe!

Ndo nimemaliza
 
Jiji Limeongezeka idadi ya watu pia bado ofisi nyingi zimejikusanya sehemu moja , posta na kariakoo , hz ofisi zetu zingeendelea kutawanywa na kuhamishwa , mfano wizara zingine ziwepo gongolamboto , tegeta , mbagala na tabata maana asubuh watu wengi wanatoka maeneo hayo kuelekea posta au kariakoo.
 
Nadhani, katika hili, ninaunga mkono hoja...ukitazama miji mikubwa yenye kuwa na Msongamano wa magari, ambapo wakati fulani hata City Trams, Trains hazisaidii hada Asia mf. Bangkok, Beijing, n.k...bado pikipiki imekuwa njia mojawapo ya usafiri mbadala.
 
Jiji Limeongezeka idadi ya watu pia bado ofisi nyingi zimejikusanya sehemu moja , posta na kariakoo , hz ofisi zetu zingeendelea kutawanywa na kuhamishwa , mfano wizara zingine ziwepo gongolamboto , tegeta , mbagala na tabata maana asubuh watu wengi wanatoka maeneo hayo kuelekea posta au kariakoo.

Bado Serikali inadhani kuhamisha Wizara toka katikati ya mji, ni gharama kuliko hasara itokanayo na shida/madhara ya foleni!

Lakini pia katika hili, nadhani kungekuwa na umuhimu wa Ofisi za Wizara husika kila mkoa, zenye kuweza kuhudumia huko huko. Kukiko watu kuja huku na shida hii kuzidi.
 
Solution ni highways tu

umemaanish flying over?
kama ni hivyo kwa kweli kwa mji ulivyopangwa dar sijui itawezekanaje labda sehemu kubw ya makazi ya watu huduma za kijamii zibomolewe!

mfano nilielezwa kuwa ili kuweka flying over pale ubungo ni lazima ile petrol/diesel filling station lazima iondoke kwz mfano kama huo utaona ni jinsi gani sehemu kubwa ya dsm itaathirika.

tatizo la mango yetu ni ya miaka mitano wakati wenzetu mbele wanapanga miaka 50-100 mbele!
 
Wakitufikisha hapa, sijui itakuwa lini?

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    7.8 KB · Views: 103
Ukiacha Walimu , Idadi kubwa ya graduate na watu wengine wanatoka mikoani kuja jjin kupata fursa za 'maisha bora', cha umuhimu ni kuzitawanya ofisi ili kuuwa msululu wa uelekeo mmoja kila asubuhi na jioni. Tusipoangalia itafika muda tutachukua masaa matano kwenda maofisini kutokana na foleni.
 
Hapo tutafika soon!! Wanaanza Ubungo na Tazara, sasa hv wapo kwenye kipindi cha kuandaa michoro!!

Mkuu, nilisikia kuwa ile plan ya michoro ya Fly- over/ Fly over, imeshahauliwa(kwamba huo mpango haupo tena na Rapid Bus Transport, ndio itakuwa mbadala, ma uwezekano huo(wa kuweka flyover ni katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ina ikiwezakana hapa Dar iwe Kigamboni tu, sijui kama lina ukweli hili.
 
Kwa hapa dsm nina uhakika mpango upo maana nishawah kukutana na vijana wanachukua topographic surveying data kwa ajili ya ku design daraja la ubungo hivi majuzi tu! na benchmark zao nimeziona!
 
Poleni sana, nina mwaka na nusu sasa tangia niiache hiyo adha, kimsingi ni shida kubwa japo tunaizoea, ukitoka na kuanza kuishi sehemu isiyo na foleni utashangaa ulivyokuwa unapata shida. nilikuwa naishi Africana Mbezi beach kazi upanga unaamka saa 11 unarudi nyumbani saa mbili au tatu usiku unatumia takribani masaa 5 kusafiri kwa siku. Ikifika wikiend ndo unaona nyumbani kunavyofanana wakati wa mchana. mda unapotea sana kwa kusafiri tu.
 
Back
Top Bottom