Muda umefika kukaa ukumbini kuangalia televisheni ni dalili za umasikini

Muda umefika kukaa ukumbini kuangalia televisheni ni dalili za umasikini

Sijasoma rhread yote ila aliyekwambia kuwa kuangalia tv kwenye kumbi tunafanya sisi tu Africa ni nani? Hata huku ughaibuni lounge kibao wazungu wanangalia mpira and etc sijui ushamba huu umeanzia wapi.
Ungesoma mpaka mwisho ungeona kuwa imebaki washamba tu na maskini wanaoangalia mipira kwenye hizo ndude.
 
Sijaelewa unamaana gani na ulikuwa unataka nini hasaaa
 
Ungesoma mpaka mwisho ungeona kuwa imebaki washamba tu na maskini wanaoangalia mipira kwenye hizo ndude.

Hapo mkuu si ishu ya umasikini, Haujajua vibe ya kuangalia mpira au live event yoyote na strangers kwenye hivyo vibanda au kumbi za starehe.
 
Hata kupangia watu maisha nako ni umaskini na ushamba ..

Acha mtu atembee na ratiba zake ..
 
Wewe mwenyewe ndo mshamba.Hata uandishi wako umekaa kishamba Sana
 
Sijasoma rhread yote ila aliyekwambia kuwa kuangalia tv kwenye kumbi tunafanya sisi tu Africa ni nani? Hata huku ughaibuni lounge kibao wazungu wanangalia mpira and etc sijui ushamba huu umeanzia wapi.
Kwani kasema ushamba ni Africa pekee?
 
Historia ya upashanaji habari ni ndefu sana. Sitaki nianzie mbali sana. Kutokana na kasi ya maendeleo ya kielimu na ukuaji wa teknolojia tumeshuhudia kupungua kasi ya usomaji magazeti mpaka magazeti makubwa duniani ikabidi yapotee au kujibadili kuwa ya kielektonik.

Miaka si mingi sana na redio maarufu duniani nazo hazina wasikilizaji nazo zikajaribu kujiingiza kwenye mitandao na bado hazijasalimika na mabadiliko ya dunia.

Tangu kuwepo kwa televisheni na radio za mitandao ambazo zinaweza kusikika duniani kote na urahisi wa kila mtu kuanzisha ya kwake imekuwa shida sana kupata wasikilizaji. Imefika muda kila mtu anajisikiliza mwenyewe au na rafiki zake wachache.

Kwa pesa ambazo sio nyingi sana kila mmoja anaweza akaanzisha televisheni au redio yake baada ya kuuza machungwa na kujidanganya kuwa anasikika au kuangaliwa na ulimwengu mzima.

Wale ambao hawana televisheni na redio zao za mtandao utawakuta wamejiinamia au kujikushanya wakiangalia kitu kinaitwa clip ama za vichekesho au wafungaji magoli na kadhalika. Hawana muda kabisa na kuangalia hizi televisheni za taifa na za mashirika zinazotokea kwenye majengo maalumu ndani ya miji.

Tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo video ilikuwa ni kitu cha kifakhari mpaka kila gari lilitangaza kuwa lina video ndani kuwavutia wasafiri.Ukifika majumbani unakuta televisheni na watu wanajikushanya kuangalia habari au vipindi vyengine muhimu.

Mambo ni tofauti kabisa miaka hii michache iliyopita.Unaweza ukawasha mitambo ya televisheni na kurusha matangazo maeneo ya karibu na kuunganisha na intaneti ukijidanganya kuwa unatazamwa na dunia nziam kumbe matangazo yenyewe yanapotea hewani bure na kuangaliwa na wachache sana.

Waangaliaji wa televisheni mara nyingi ni wageni kutoka shamba ambao wameingia mijini au wale wavivu ambao hawafanyi kazi au hawajapata kazi za kufanya.Hawa ni watazamaji ambao hawana faida sana kwa vituo vya televisheni.

Ukata wa wasikilizaji na watazamaji naamini umewakumba wote wanaomiliki vituo hivyo na hakuna wa kujidai mbele ya mwenzake. Mimi mwenyewe nilikuwa na cha kwangu nilipoona naangalia mwenyewe nikaamua kukifunga ili nisizidi kutumbukia kwenye umasikini.

Vituo vya televisheni vinavyopumulia mashine ni vile vinavyoonesha mechi za mipira tu na wengi wa waangaliaji huamua kujikushanya pamoja kwenye mabanda badla ya kukaa majumbani mwao.Hii nayo ni dalili ya ushamba na umasikini.
Ila wewe jamaa ni mhafidhina kila pahali.
 
Hizi mentality ndio ushamba wenyewe,yaani nikiwa na muda wa ziada niache kuangalia TV kisha ni ushamba! Huyu unakuta ni mzazi kwake vitu vizuri vyote anaona ni ushamba na anasa! Kuna watu mateso wanaona ni sifa...
 
Back
Top Bottom