Muda umeisha, Babu Seya ndio basi tena?

Muda umeisha, Babu Seya ndio basi tena?

sinafungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Posts
1,527
Reaction score
865
Wanamuziki Nguza Viking na Papii Kocha wanaotumikia kifungo cha maisha jela, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete awasamehe kwa makosa waliyofanya.

Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi hilo kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Nguza maarufu Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete.

TAARIFA HII NI YA TEREHE 21/JUNI/2014. Mhe. Rais anamaliza muda na juzi alikuwa kule magereza akitunuku nishani. Alisema akisamehe baada ya muda wanaorudi kifungoni ni zaidi ya aliowasamehe.
 
Nawapa pole Babu Seya,lkn naamini wasiposamehewa na mkuu wa nchi Yupo Mungu muumba mbingu na nchi,huyu ni Mungu mwenye Rehema huwasamehe wanaotubu makosa yao,hivyo aweke tumaini lake kwa Bwana.Wakumbuke akina Paulo na Sira ambao milango ya gereza ilifunga na wakatoka gerezani,Mungu yupo aliye mkuu zaidi ya wote,Naamini kuwa yataisha tu Maana Mungu humpenda mtu anayetubu.
 
Nawapa pole Babu Seya na mwanaye,lkn naamini wasiposamehewa na mkuu wa nchi Yupo Mungu muumba mbingu na nchi,huyu ni Mungu mwenye Rehema huwasamehe wanaotubu makosa yao,hivyo aweke tumaini lake kwa Bwana.Wakumbuke akina Paulo na Sira ambao milango ya gereza ilifunga na wakatoka gerezani,Mungu yupo aliye mkuu zaidi ya wote,Naamini kuwa yataisha tu Maana Mungu humpenda mtu anayetubu.
 
inaskitisha sana,duniani hakuna haki. mbinguni wote sawa kudadadeki.hakuna uchungu unaokosa utamu
 
Lowassa mcha mungu atawatoa jela punde atakapochukua nchi
 
Awasamehe kwa kosa walilofanya? kosa gani tena? si walisingiziwa?
 
Nauliza wameshakaa jela muda gani hadi sasa
 
Daaah Mungu ni mwema atasikia kilio chao, sitaki kuamini kama ni kweli wote wametenda hilo kosa,
 
Wanamuziki Nguza Viking na Papii Kocha wanaotumikiakifungo cha maisha jela, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete awasamehe kwa makosawaliyofanya.
Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi hilo kupitia wimbowakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuocha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapoNguza maarufu Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuizawakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwaRais Kikwete.
TAARIFA HII NI YA TEREHE 21/JUNI/2014.........MHE Rais anamaliza muda na juzi alikuwa kule magereza akitunuku nishani.alisema akisamehe baada ya muda ya muda wanaorudi kifungoni ni zaidi a aliowasamehe.

naamini wale watoto waliodaiwa kufanyiwa unyama na babu seya na wanawe wameshakuwa watu wazima sasa,kwanini wasiitwe na wahojiwe kama wana kumbukumbu zozote za kufanyiwa vitendo hivyo?au hata uchunguzi wa kina ufanyike kama ni kweli walishawahi kufanyiwa vitendo hivyo?naamini hata mashaid lazima wajichanganye tu kwa kipindi hiki kwani uongo ni rahisi kusahau.kama ni kweli babu seya na wanawe walitenda kosa hilo basi adhabu hiyo inawafaa na kama hawakutenda basi haki itendeke
 
Kwanni wanaomba wasamehewe wakati wanasema walisingiziwa???
Mhe. le professeri, daktari wa madaktari, dokta wa madokta hata kama walitenda kweli wasamehe ila warudishe kwao Congo
 
Jamani si kweli kyfungwa kwa babu seya JK anausika waliwanajisi kweli na laiti wewe yngekuwa wewe umefanyiwa ungeomba wewe ndio umsamehe kwanza na sio rais ambaye watu wamemsingizia.Mimi nilukuwa nakaa jirani nao na walukuwa wanaingiza hao watoto na kuwafanyia mambo ya kishenzi kwa kuagizwa na mganga wa kuenyeji ili mambo yao yanyooke.Kama anamsingizia JK atoke adharani au aandike kwa haki za binadam wamtetee.Hata hivyo ungekuta kaonewa ungekuta akina Lissu na wenzake walishaibebea bango.Mimi JK sio baba yangu wala sio nini ila watu wanajua kusema vitu wasivyovijua
 
Back
Top Bottom