Muda wa Mungu ulipofika, muda wa Majaliwa ukakaa pembeni

Muda wa Mungu ulipofika, muda wa Majaliwa ukakaa pembeni

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Si kila muda ni muda sahihi bali muda wa Bwana,rejea Yohana 7:6 Yesu akawajibu, “Wakati wangu wa kwenda huko haujafika, ninyi mnaweza kwenda wakati wowote,ni kweli asubuhi yako inaweza kuamua ni kwa kiasi gani siku yako itakuwa kwa mjumuisho ni kweli asubuhi ndio uwa na matayarisho juu ya siku husika, lakini muda wa Mungu unapofika ndio kilele cha mjumuisho wa siku yako njema, mapito yako yaweza kuwa ni kwa ajili ya kukuimarisha kwa jambo kubwa lijalo,changamoto unazopitia zaweza kuwa ni kukuhifadhi kwa ajili ya siku ngumu zijazo,pengine kukutia nguvu, usilaumu lolote katika jambo lolote unalopitia,Malaika wa Mungu wapo kazini kukuandaa.

Miaka ishirini ya maisha ufukara na umasikini ya Majaliwa yalikuwa ni mazoezi kwa ajili ya siku moja tu Mungu aliyoiandaa kwa ajili ya kuokoa watu waliozama na ndege,miaka ya ufukara aliyoishi Majaliwa yalikuwa kwenye kalenda ya Mungu, mpango wa wokovu na yaliyofuatia baada ya hapo yalikuwa ni zawadi baada ya kufaulu mtihani,maisha kukulia karibu na ziwa, kuogelea pindi unapokosa cha kufanya, kuuza dagaa mwaloni,kuoga ziwani kwa kuwa nyumbani hakuna bomba la maji, yote yalikuwa ni maandalizi kwa ajili ya siku moja tu ya kuja kuokoa watu waliozama na ndege ndani ya maji, pengine aliyachukia maisha hayo na kudhani labda ni maisha ya ufukara na umasikini lakini Mungu aliwaza tofauti katika ufukara na umasikini huo, Mungu alikuwa mpango kabambe wa siku moja ya uokoaji, mawazo yako si mawazo ya Mungu,yeye anatujua vyema na kutuwazia mema ili mapenzi yake yatimizwe katika muda wake sahihi,Mungu hachelewi wala hawahi.

Mungu mwenyezi tunaemwamini humpa kila mtu mkate wake kulingana na anavyo ona,huyu hupewa mkate na kufanyika daraja la kuwapitishia wengne, huyu hupewa kipaji na kuwa mtu wa miradi ya aina mbalimbali na sehemu ya sadaka na matoleo kwa wengine, huyu hupewa kiasi ili tu akidhi haja ya moyo wake asije akamdhiahaki alie muumba,huyu hupewa adhabj kwa kuwa tu ni sehemu ya funzo kwa wengine.Zaburi 91:5,7 hutaogopa hofu ya usiku,wala mshale urukao mchana,japo watu elfu waanguka ubavuni pako,naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! hata hivyo hautakukaribia wewe.

Kama kijana au kama binadamu yeyote wa kawaida ni lazima kuna mipango fulani itakuwa umejiwekea kwenye maisha,Mipango yako inaweza kuwa mizuri kwa ufahamu wako wa kawaida lakini upo uwezekano wa kutokutimia kwa mipango hiyo,haitimii sio kwasababu wewe ni mzembe sana na haupo makini katika kusimamia ndoto zako la hasha! bali haitimii kwasababu Mungu hajatoa kibali cha mipango hiyo kuweza kutimia,ikiwa binadamu tunapanga mambo yetu, nae Mungu anapanga yakwake,hivyo inawezekana kuwa mipango yako kuwa tofauti na mpango wa Mwenyezi Mungu katika maisha yako,ni kweli tunapaswa kuchekecha akili zetu sawasawa na kutumia nguvu zetu sawasawa,kanuni ya Malengo, Juhudi, maarifa hatuna budi kuifuata,lakini Mungu ndiye mwenye kibali cha hayo yote kufanikiwa.

Tutimize wajibu wetu vizuri, kisha tusubiri muda wa Bwana kutimiza mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu,tusitumie njia hatarishi kama vile kudhuru wengine au kutenda dhambi ili kupata tunayotaka,kilichopangwa na Mwenyezi Mungu kwaajili yako utakipa tu hata iweje ni lazima utakipata,usijali kuhusu muda, utakipata tu,mtaalamu wa mipango amepanga kila kitu hadi muda wa barikiwa kwako umepangwa,Usiwe na wasiwasi au kutafuta mbinu za ziada mala utoe kafara, eti uibe ndio ufanikiwe, eti uuze mwili wako acha hizo mambo. Master planner wetu, mtaalamu wa mipango ameshaweka mipango yote sawa kwaajili yako.

Mtanzania mwenzangu unayepitia mapito, changamoto, umasikini, ufukara, kutukanwa, manyanyaso kazini, kuonewa,kushushwa cheo, yupo Mungu ameandaa jambo jema mbele,muda wa Bwana Mungu utakapofika utatabasamu na kusema ooh kumbe Mungu alikuwa ananiepusha na retrenchment niliposhushwa cheo waliobakia wakaondoka, nilipokwenda kuogelea kumbe nilikuwa najifunza kuogelea ili kuja kuokoa watu,Mungu anayosababia ya wewe kupitia hali yoyote ile unayopitia, Yeremia 18:4-6 na chombo kile, alichokuwa akikifinyanga, kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi, alikifanyiza tena kuwa chombo kingine, kama alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya, ndipo neno la Bwana likanijia, kusema, Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana, angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi,ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078853

- Bachelor of Business Administration in International Business.

- Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
- Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Si kila muda ni muda sahihi bali muda wa Bwana,rejea Yohana 7:6 Yesu akawajibu, “Wakati wangu wa kwenda huko haujafika,ninyi mnaweza kwenda wakati wowote,ni kweli asubuhi yako inaweza kuamua ni kwa kiasi gani siku yako itakuwa kwa mjumuisho,ni kweli asubuhi ndio uwa na matayarisho juu ya siku husika,lakini muda wa Mungu unapofika ndio kilele cha mjumuisho wa siku yako njema,mapito yako yaweza kuwa ni kwa ajili ya kukuimarisha kwa jambo kubwa lijalo,changamoto unazopitia zaweza kuwa ni kukuhifadhi kwa ajili ya siku ngumu zijazo,pengine kukutia nguvu,usilaumu lolote katika jambo lolote unalopitia,Malaika wa Mungu wapo kazini kukuandaa.

Miaka ishirini ya maisha ufukara na umasikini ya Majaliwa yalikuwa ni mazoezi kwa ajili ya siku moja tu Mungu aliyoiandaa kwa ajili ya kuokoa watu waliozama na ndege,miaka ya ufukara aliyoishi Majaliwa yalikuwa kwenye kalenda ya Mungu,mpango wa wokovu na yaliyofuatia baada ya hapo yalikuwa ni zawadi baada ya kufaulu mtihani,maisha kukulia karibu na ziwa,kuogelea pindi unapokosa cha kufanya,kuuza dagaa mwaloni,kuoga ziwani kwa kuwa nyumbani hakuna bomba la maji, yote yalikuwa ni maandalizi kwa ajili ya siku moja tu ya kuja kuokoa watu waliozama na ndege ndani ya maji, pengine aliyachukia maisha hayo na kudhani labda ni maisha ya ufukara na umasikini lakini Mungu aliwaza tofauti katika ufukara na umasikini huo,Mungu alikuwa mpango kabambe wa siku moja ya uokoaji, mawazo yako si mawazo ya Mungu,yeye anatujua vyema na kutuwazia mema ili mapenzi yake yatimizwe katika muda wake sahihi,Mungu hachelewi wala hawahi.

Mungu mwenyezi tunaemwamini humpa kila mtu mkate wake kulingana na anavyo ona,huyu hupewa mkate na kufanyika daraja la kuwapitishia wengne, huyu hupewa kipaji na kuwa mtu wa miradi ya aina mbalimbali na sehemu ya sadaka na matoleo kwa wengine, huyu hupewa kiasi ili tu akidhi haja ya moyo wake asije akamdhiahaki alie muumba,huyu hupewa adhabj kwa kuwa tu ni sehemu ya funzo kwa wengine.Zaburi 91:5,7 hutaogopa hofu ya usiku,wala mshale urukao mchana,japo watu elfu waanguka ubavuni pako,naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! hata hivyo hautakukaribia wewe.

Kama kijana au kama binadamu yeyote wa kawaida ni lazima kuna mipango fulani itakuwa umejiwekea kwenye maisha,Mipango yako inaweza kuwa mizuri kwa ufahamu wako wa kawaida lakini upo uwezekano wa kutokutimia kwa mipango hiyo,haitimii sio kwasababu wewe ni mzembe sana na haupo makini katika kusimamia ndoto zako la hasha! bali haitimii kwasababu Mungu hajatoa kibali cha mipango hiyo kuweza kutimia,ikiwa binadamu tunapanga mambo yetu,nae Mungu anapanga yakwake,hivyo inawezekana kuwa mipango yako kuwa tofauti na mpango wa Mwenyezi Mungu katika maisha yako,ni kweli tunapaswa kuchekecha akili zetu sawasawa na kutumia nguvu zetu sawasawa,kanuni ya Malengo, Juhudi, maarifa hatuna budi kuifuata,lakini Mungu ndiye mwenye kibali cha hayo yote kufanikiwa.

Tutimize wajibu wetu vizuri, kisha tusubiri muda wa Bwana kutimiza mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu,tusitumie njia hatarishi kama vile kudhuru wengine au kutenda dhambi ili kupata tunayotaka,kilichopangwa na Mwenyezi Mungu kwaajili yako utakipa tu hata iweje ni lazima utakipata,usijali kuhusu muda, utakipata tu,mtaalamu wa mipango amepanga kila kitu hadi muda wa barikiwa kwako umepangwa,Usiwe na wasiwasi au kutafuta mbinu za ziada mala utoe kafara, eti uibe ndio ufanikiwe, eti uuze mwili wako acha hizo mambo. Master planner wetu, mtaalamu wa mipango ameshaweka mipango yote sawa kwaajili yako.

Mtanzania mwenzangu unayepitia mapito,changamoto,umasikini,ufukara,kutukanwa,manyanyaso kazini,kuonewa,kushushwa cheo,yupo Mungu ameandaa jambo jema mbele,muda wa Bwana Mungu utakapofika utatabasamu na kusema ooh kumbe Mungu alikuwa ananiepusha na retrenchment niliposhushwa cheo waliobakia wakaondoka,nilipokwenda kuogelea kumbe nilikuwa najifunza kuogelea ili kuja kuokoa watu,Mungu anayosababia ya wewe kupitia hali yoyote ile unayopitia,Yeremia 18:4-6 na chombo kile,alichokuwa akikifinyanga,kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi,alikifanyiza tena kuwa chombo kingine,kama alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya,ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana,angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi,ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu,Ee nyumba ya Israeli.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078853

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Hivyo vyote vyeo vyako!!??
 
Unaonekana ur very bright mindicaly but ur have decide to bury ur mind kwa kuwa mpika debe wa CCM
 
Back
Top Bottom