SoC02 Muelekeo hasi kwa Wanafunzi katika Elimu

Stories of Change - 2022 Competition

Lapluto

Member
Joined
Jul 14, 2022
Posts
80
Reaction score
129
UTANGULIZI.

Elimu ni mfumo wa mafunzo utolewao mashuleni na hata katika jamii zetu tunazoishi.Elimu ni moja ya nguzo kubwa sana iletayo mapinduzi makubwa kwa kuirahisishia jamii kupambana na changamoto za kila siku ambazo huchochea maendeleo chanya kwenye sekta mbalimbali iwe kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Mfumo wa elimu kwa Tanzania hutokewa kwa ngazi tofauti kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, mfumo huu humuandaa mwanafunzi kupata maarifa ili atimize ndoto zake na kuisaidia jamii.

Katika kipindi cha masomo wanafunzi hukutana na changamoto nyingi sana za kielimu iwe kiujumla au kwa mtu mmoja mmoja. Kila mwanafunzi huwa na ndoto yake amvayo hutamani kuifikia kama vile kuwa mwalimu, mwanasheria, daktari pamoja na mhabdisi. Hata hivyo kuna baadhi waliofanikiwa na wengine kutofanikiwa kwa sababu mbalimbali kama vile ada, miundombinu, kufeli au kusimamishwa shule. Hivyo, muelekeo wa elimu kwao huenda kinyume na matarajio yao ambayo huzaa majuto na lawama ndani ya nafsi yake na jamii inayomzunguka. Kwa wanafunzi waliifaulu kuendelea husona masomo iwe kwa bidii au la bila kuzingatia ni masomo yapi yatanifikisha ninapokwenda ili ayashike vilivyo kwa kuyaelewa zaidi.

Baadhi ya mifano halisi ni Kama ifuatavyo :

Chando : Jukwaa la elimu

Sababu ziletazo muelekeo hasi kwa wanafunzi.
1. Kuchaguliwa mchepuo au fani (diploma) asizozitarajia, kwa mfano mwanafunzi kuchaguliwa mchepuo wa sanaa badala ya sayansi au fani ya ufundi badala ya afya(kwa ngazi ya diploma).

2.Uelewa finyu juu ya michepuo na fani husika, hapa mwanafunzi hujua baadhi ya michupuo Kama vile PCB, PCN, EGM, HKL na CBG au kozi fulani kwa mfano ualimu, udaktari na sheria.

3.Kufuata mkumbo wa wanafunzi wenzake (marafiki), mwanafunzi hushindwa kuwa na maamuzi binafsi (madhubuti) kwa kuzingatia hitaji lake. Kwa mfano kuacha baadhi ya masomo kwa kufuta mkumbo.

4. Upeo mdogo wa wazazi, ndugu na hata marafiki kuhusu uhusu masomo na kozi au fani husika. Baadhi ya wazazi au walezi hukosa au huwa hawana maarifa juu ya kipi mwanafunzi akipe kipaumbele zaidi ili afanikiwe kutimiza ndoto zake na mwanafunzi afikie malengo yake. Hivyo , wazazi wengi hukosa maarifa zaidi kutokana na kuishia ngazi za chini za elimu kama vile darasa la saba, kidato cha nne au kutokuwa na elimu kabsa.

5. Kukosa mshauri sahihi, katika maisha ya mwanadamu tunaishi kwa kutegemea. Hivyo, kuwa na mtu wa kukushauri unapokwama ni muhimu sana. Mwanafunzi hukosa mshauri sahihi mwenye maarifa juu ya masomo au fani husika iwe mzazi na hata mtu mwalingine. Kwa mfano mwanafunzi ana ndoto ya kuwa mhandisi, hivyo ili apate ushauri mzuri au mwongozo anapaswa kupata mtu sahihu mwenye uelewa wa hiyo fani.

6. Kushindwa kujua uhusiano wa masomo na fani zake kwa kina. Kutokana na kukariri mwanafunzi hujua baadhi ya miunganiko ya masomo kwa mfano PCB, PCM au HKL na kushindwa kuelewa kwa kina fani zipi zinafaa kwa mchepuo fulani.

Matokea yake kabla na baada ya kumaliza elimu.
1. Kushindwa kusoma mchepuo au fani aipendayo, kutokana na kukosa muelekeo sahihi baadhi ya wanafunzi hushindwa kusomea kitu wakitakacho. Hivyo, huishia kusoma kwa unyonge ili amalize au kuhitumu.

2. Kukosekana kwa wataalamu wenye uweledi juu ya kile walichosomea, uwajibikaji wa wataalamu huwa ni mdogo na ubunifu hutoweka kabisa. Hivyo, watatuzi wa changamoto huwa ni wachache.

3. Kuibuka kwa maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi baada ya kuhitimu ngazi fulani, baadhi ya maswali hayo ni kama vile kozi ipi ina soko ?, nikisoma mchepuo huu baadae naweza somea nini ?, Je, mchupuo huu naweza soma fani hii ?. Hapo ujue mwanafunzi hana muelekeo sahihi.

4. Kurudia kusoma upya, kuna baadhi yao huweza kurudia au kusoma fani aitakayo kwa kuanza ngazi ya chini kama vile diploma na hapa huwa kashapoteza mda mwingi sana hadi kuamka.

5. Kupatwa na matatizo ya kisaikolojia, kutokana na majuto pamoja na lawama huishia kupata msongo wa mawazo na magonjwa mengine. Dharau na kutengwa na jamii nayo huwa inachochea maradhi kwa mhusika.

6. Lawama kwa jamii na hata serikali, mwanafunzi au mhitimu huanza kulaumu juu ya fani au kozi zitolewazo kwa kudai mbona wanatoa kozi ambazo hawaajiri na kusahau suala la utafutaji wa maarifa.

Mapendekezo yangu kwa jamii pamoja na serioali.

1. Kuwepo na somo litakalowapa uelewa wa uhusiano wa michupuo na fani husika. Itawasaidia wanafunzi kutambu kwa kina ni masomo yapi ayatilie mkazo zaidi kuepusha taharuki wakati wa jujiunga kidato cha tano au chuo. Somo au mafunzo haya yanaweza kutolewa mwanzoni nwa muhula wa Kwanza akiwa kidato cha kwanza na kuhakikisha wameelewa hasa muongozo wa Nacte na TCU.

2. Kila mwanafunzi anapaswa apate mshauri sahihi. Mshauri huyo anaweza kuwa ni mwalimu au mfanyakazi (aliyehitimu fani husika) wa masomo husika, kwa kufanya hivyo wanafunzi ataandaliwa kusaikolojia juu ya masomo na fani azipendazo kipindi akiwa mwanafunzi .

3. Kuwapa mda wa kutosha wa kubadili michepuo au fani, hii itapunguza hofu na jazba kwa mhusika na kupata mda wa kutosha kufikiri na kuamua kipi achague kwa wakati huo. Pia ushauri muhimu unapaswa uwepo inaweza ikawa yupo sehemu sahihi ila hana uelewa wa kutosha.

4. Kushirikisha wazazi na walezi juu ya kile ukipendacho. Katika jamii zetu kuna baadhi ya familia kama baba au mama ni mwalimu basi mtoto atalazimishwa kusomea ualimu au Kama ni nesi napo ni hivyo hivyo. Hii nayo huishia pabaya kwani mtoto atasoma kwa kinyongo bila bidii yoyote.Chanzo cha matokeo mabovu ya uwajibikaji kazini hutokana na kufanya kazi asiyoipenda , furaha yake ni siku ya mshahara tu ila siku zingine mawazo yote ni kuwaza mda wa kutoka kazini.

Hitimisho.
Napenda kuwashuru jamii na serikali kwa kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa ijapokuwa changamoto hazikosekani lakini mafanikio yameonekana. Ukilinganisha idadi ya wasomi kwa sasa na zamani ni tofauti kwani tumeweza kupata wasomi wengi kuliko kipindi cha nyuma. Juhudi na ubunifu huanza kwa mtu mwenyewe kwa kufuata mkondo husika lakini vitu hivi hukosekana miongoni mwa wahitimu.
 
Upvote 99
Upo sahihi dada "pendo" uwezi kusema kwenye swala la kuelimika kwamba ulikuwa unapoteza muda hapana.

Nazani mtoa mada alikuwa anazungumzia swala zima la "ajira" baada ya elimu, lakini mbona mwanafunzi akifika level flani anapewa nafasi ya kuchagua cha kusomea.
hata kuchagua napo bado ni changamoto kubwa sana. Mwanafunzi huwa hana uelewa na michepuo yote ya advance, akilini mwake anajua zile za PCB, PCM, EGM, HKL n.k. Utakuta akifika kidato cha tatu huwa yupo dilemma Sababu ya kukosa mshauri au hata hana uelewa wa mgawanyiko wa hizo combination na kozi kwa wale wa diploma. Uzuri nimeweka na mifano halisi ya nyuzi zilizochapishwa jukwaa la elimu.
Asante kwa maoni tuendelee kulijadili.
 
Jamani tusipite kimya kimya bila kupingwa. Kama umependezwa na chapisho hili, naomba mchango wako wa :
1. Maoni
2. Kura (gusa kialama ^ mwishoni mwa chapisho
Mbona hiko kialama hakionekani,,hebu screen shot jinsi kinavyoonekana kwako tukione.
 
Mkuu nioneshe ni sehemu gani hapo kuna hako kaalama?
Screenshot_20220722-060851.jpg
 
Naona hicho kialama kipo kwenye new app ya Jf "labda" maana kwenye hii app ya zamani hakionekani.
 
UTANGULIZI.

Elimu ni mfumo wa mafunzo utolewao mashuleni na hata katika jamii zetu tunazoishi.Elimu ni moja ya nguzo kubwa sana iletayo mapinduzi makubwa kwa kuirahisishia jamii kupambana na changamoto za kila siku ambazo huchochea maendeleo chanya kwenye sekta mbalimbali iwe kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Mfumo wa elimu kwa Tanzania hutokewa kwa ngazi tofauti kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, mfumo huu humuandaa mwanafunzi kupata maarifa ili atimize ndoto zake na kuisaidia jamii.

Katika kipindi cha masomo wanafunzi hukutana na changamoto nyingi sana za kielimu iwe kiujumla au kwa mtu mmoja mmoja. Kila mwanafunzi huwa na ndoto yake amvayo hutamani kuifikia kama vile kuwa mwalimu, mwanasheria, daktari pamoja na mhabdisi. Hata hivyo kuna baadhi waliofanikiwa na wengine kutofanikiwa kwa sababu mbalimbali kama vile ada, miundombinu, kufeli au kusimamishwa shule. Hivyo, muelekeo wa elimu kwao huenda kinyume na matarajio yao ambayo huzaa majuto na lawama ndani ya nafsi yake na jamii inayomzunguka. Kwa wanafunzi waliifaulu kuendelea husona masomo iwe kwa bidii au la bila kuzingatia ni masomo yapi yatanifikisha ninapokwenda ili ayashike vilivyo kwa kuyaelewa zaidi.

Baadhi ya mifano halisi ni Kama ifuatavyo :

Chando : Jukwaa la elimu

Sababu ziletazo muelekeo hasi kwa wanafunzi.
1. Kuchaguliwa mchepuo au fani (diploma) asizozitarajia, kwa mfano mwanafunzi kuchaguliwa mchepuo wa sanaa badala ya sayansi au fani ya ufundi badala ya afya(kwa ngazi ya diploma).

2.Uelewa finyu juu ya michepuo na fani husika, hapa mwanafunzi hujua baadhi ya michupuo Kama vile PCB, PCN, EGM, HKL na CBG au kozi fulani kwa mfano ualimu, udaktari na sheria.

3.Kufuata mkumbo wa wanafunzi wenzake (marafiki), mwanafunzi hushindwa kuwa na maamuzi binafsi (madhubuti) kwa kuzingatia hitaji lake. Kwa mfano kuacha baadhi ya masomo kwa kufuta mkumbo.

4. Upeo mdogo wa wazazi, ndugu na hata marafiki kuhusu uhusu masomo na kozi au fani husika. Baadhi ya wazazi au walezi hukosa au huwa hawana maarifa juu ya kipi mwanafunzi akipe kipaumbele zaidi ili afanikiwe kutimiza ndoto zake na mwanafunzi afikie malengo yake. Hivyo , wazazi wengi hukosa maarifa zaidi kutokana na kuishia ngazi za chini za elimu kama vile darasa la saba, kidato cha nne au kutokuwa na elimu kabsa.

5. Kukosa mshauri sahihi, katika maisha ya mwanadamu tunaishi kwa kutegemea. Hivyo, kuwa na mtu wa kukushauri unapokwama ni muhimu sana. Mwanafunzi hukosa mshauri sahihi mwenye maarifa juu ya masomo au fani husika iwe mzazi na hata mtu mwalingine. Kwa mfano mwanafunzi ana ndoto ya kuwa mhandisi, hivyo ili apate ushauri mzuri au mwongozo anapaswa kupata mtu sahihu mwenye uelewa wa hiyo fani.

6. Kushindwa kujua uhusiano wa masomo na fani zake kwa kina. Kutokana na kukariri mwanafunzi hujua baadhi ya miunganiko ya masomo kwa mfano PCB, PCM au HKL na kushindwa kuelewa kwa kina fani zipi zinafaa kwa mchepuo fulani.

Matokea yake kabla na baada ya kumaliza elimu.
1. Kushindwa kusoma mchepuo au fani aipendayo, kutokana na kukosa muelekeo sahihi baadhi ya wanafunzi hushindwa kusomea kitu wakitakacho. Hivyo, huishia kusoma kwa unyonge ili amalize au kuhitumu.

2. Kukosekana kwa wataalamu wenye uweledi juu ya kile walichosomea, uwajibikaji wa wataalamu huwa ni mdogo na ubunifu hutoweka kabisa. Hivyo, watatuzi wa changamoto huwa ni wachache.

3. Kuibuka kwa maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi baada ya kuhitimu ngazi fulani, baadhi ya maswali hayo ni kama vile kozi ipi ina soko ?, nikisoma mchepuo huu baadae naweza somea nini ?, Je, mchupuo huu naweza soma fani hii ?. Hapo ujue mwanafunzi hana muelekeo sahihi.

4. Kurudia kusoma upya, kuna baadhi yao huweza kurudia au kusoma fani aitakayo kwa kuanza ngazi ya chini kama vile diploma na hapa huwa kashapoteza mda mwingi sana hadi kuamka.

5. Kupatwa na matatizo ya kisaikolojia, kutokana na majuto pamoja na lawama huishia kupata msongo wa mawazo na magonjwa mengine. Dharau na kutengwa na jamii nayo huwa inachochea maradhi kwa mhusika.

6. Lawama kwa jamii na hata serikali, mwanafunzi au mhitimu huanza kulaumu juu ya fani au kozi zitolewazo kwa kudai mbona wanatoa kozi ambazo hawaajiri na kusahau suala la utafutaji wa maarifa.

Mapendekezo yangu kwa jamii pamoja na serioali.

1. Kuwepo na somo litakalowapa uelewa wa uhusiano wa michupuo na fani husika. Itawasaidia wanafunzi kutambu kwa kina ni masomo yapi ayatilie mkazo zaidi kuepusha taharuki wakati wa jujiunga kidato cha tano au chuo. Somo au mafunzo haya yanaweza kutolewa mwanzoni nwa muhula wa Kwanza akiwa kidato cha kwanza na kuhakikisha wameelewa hasa muongozo wa Nacte na TCU.

2. Kila mwanafunzi anapaswa apate mshauri sahihi. Mshauri huyo anaweza kuwa ni mwalimu au mfanyakazi (aliyehitimu fani husika) wa masomo husika, kwa kufanya hivyo wanafunzi ataandaliwa kusaikolojia juu ya masomo na fani azipendazo kipindi akiwa mwanafunzi .

3. Kuwapa mda wa kutosha wa kubadili michepuo au fani, hii itapunguza hofu na jazba kwa mhusika na kupata mda wa kutosha kufikiri na kuamua kipi achague kwa wakati huo. Pia ushauri muhimu unapaswa uwepo inaweza ikawa yupo sehemu sahihi ila hana uelewa wa kutosha.

4. Kushirikisha wazazi na walezi juu ya kile ukipendacho. Katika jamii zetu kuna baadhi ya familia kama baba au mama ni mwalimu basi mtoto atalazimishwa kusomea ualimu au Kama ni nesi napo ni hivyo hivyo. Hii nayo huishia pabaya kwani mtoto atasoma kwa kinyongo bila bidii yoyote.Chanzo cha matokeo mabovu ya uwajibikaji kazini hutokana na kufanya kazi asiyoipenda , furaha yake ni siku ya mshahara tu ila siku zingine mawazo yote ni kuwaza mda wa kutoka kazini.

Hitimisho.
Napenda kuwashuru jamii na serikali kwa kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa ijapokuwa changamoto hazikosekani lakini mafanikio yameonekana. Ukilinganisha idadi ya wasomi kwa sasa na zamani ni tofauti kwani tumeweza kupata wasomi wengi kuliko kipindi cha nyuma. Juhudi na ubunifu huanza kwa mtu mwenyewe kwa kufuata mkondo husika lakini vitu hivi hukosekana miongoni mwa wahitimu.
uko sahihi mkuu
 
Kiini cha Tatizo kinaanzia kwenye mtaala mzima uliowekwa na serikali hauna uhalisia na maisha halisi.
Unakuta mtoto wa Darasa la 6 au kidato cha kwanza anabebeshwa mzigo wa madaftari hadi shingo inapinda.
Hii inachangia wanafunzi kukosa focus kwa maana inakuwa kama bahati nasibu masomo atakayobahatika kufaulu ndio ataendelea nayo mbeleni na sio kile akipendacho.
Kwa ujumla mfumo wetu wa Elimu si rafiki kwa mwanafunzi kwa mfano mwanafunzi amesoma vizuri kuanzia form 1 hadi mwaka wa mwisho form 4 na huko nyuma alikuwa anafaulu vizuri mitihani ya mihula lakini zikifika siku za mitihani ya Necta inamlazimisha kutafuta notes na vitabu nje ya vile alivyofundishwa na mwalimu wake ili kuubahatisha ufaulu kwa kukesha usiku kucha na bado anaweza asiambulie kitu kwa lugha ya kiuanafunzi tulikuwa tunaita"Kwenda OP,Kuingia chaka,Kumeza matango pori".
Hii inawapotezea mood wanafunzi na kufocus kuhusu ndoto zao
Kwa mfumo huu wa elimu inageuka ni vita ambapo nchi za wengine huko majuu kwenye mitihani kile alichokifundisha mwalimu ndicho hicho utakikuta kwenye mitihani.
Matokeo yake mtu anasoma hadi anamaliza form 6 hajijui atakuja kuwa nani kutokana na mfumo mbovu wa elimu.
Kwa maoni yangu hatuwezi kufika popote bila kubadilisha mfumo wa elimu.
 
shukrani Sana.
Ni kweli hili la masomo mengi ni tatizo, Kama mshika mbili moja humponyoka sipatii wale wanaosoma masomo zaidi ya kumi na mbili. Uhaba wa vifaa napo ni shida maana mwalimu analazimika kutumia kitabu chochote bado tena kwa mwanafunzi naye ni hivyo hivyo . Na ukifatilia kwa mfano somo hata la hesabu vitabu anavyotumia mwalimu ni tofauti na mwalimu wa shule nyingine. Haoa Mimi naona wanafunzi waandaliwe mapema kufikia sekondari waanze kuchimba maeneo yawapendayo.
 
Back
Top Bottom