Shanily
JF-Expert Member
- Nov 4, 2024
- 856
- 1,662
Ndoa nyingi za sasa zinavunjika kwakua watu wanaoa au kuolewa na watu ambao hawaendani nao.
Mnaweza nyote mkawa na dini, tabia nzuri lakini ndoa ikafa kwakukosa muendano wa kimawazo.
Kuna wanaume wao ndo wanataka wawe dominate kwa 100% yaani huna Cha kumwambia, neno lake ndo katiba huyu akitaka adumu ndoani aoe yule mwanamke wa tumeskia na tumetii, Chochote hewala.
Shida inakuja kakuta bint ana tabia zake nzuri lakini ni 50/50, anapenda ushirikishwaji katika mambo, maoni yangu yaheshimiwe pia , hapo lazima watasumbuana na ikafikia talaka maana mke atahisi kaachwa nyuma, vinyongo vinaanza.
Au mwanamke anataka yeye ndo awe mwenye kauli ya mwisho, anaenda kuolewa na mtu anaetaka kuwa mwenye kauli ya mwisho pia, hapo kizaazaa kinaanza, halafu shida tunajipa moyo atabadilika. Tabia ni kama ngozi ya mwili vigumu kuibadili.
Kwahy katika vigezo vya mwenza umtakae muhimu pia kuongeza kigezo cha muendano wa kimawazo ili tupunguze hizi talaka za Kila siku katika zama hizi za teknolojia.