KERO Mufindi: Watumishi wapya wa kada ya Tabibu Daraja la II na Maafisa Afya hatujalipwa fedha zetu za kujikimu

KERO Mufindi: Watumishi wapya wa kada ya Tabibu Daraja la II na Maafisa Afya hatujalipwa fedha zetu za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tangu tuliporipoti kazini miezi sita iliyopita, sisi watumishi wapya wa kada ya Tabibu Daraja la II na Maafisa Afya hatujalipwa fedha zetu za kujikimu. Tunapofuatilia madai yetu, tunaelezwa kuwa fedha hizo hutolewa na TAMISEMI na bado hazijaingizwa hadi sasa.

Aidha, tuliitwa kusaini fomu za Vendors, lakini zaidi ya mwezi mmoja umepita bila kupata mrejesho wowote. Tumeelezwa kuwa tunaweza kulipwa Shilingi 600,000 zilizopo kwa sasa au kuendelea kusubiri fedha zetu zote kwa muda usiojulikana.

Soma: Halmashauri ya Mufindi tumeanza kulipwa fedha zetu za Kujikimu, japo tumelipa nusu

Tunaomba mamlaka husika iingilie kati kutatua changamoto hii, kwani tumekuwa tukihofia hata kupaza sauti kudai haki zetu.

Watumishi wenzetu walioajiriwa pamoja nasi katika halmashauri nyingine, kwa kiasi kikubwa, tayari wamelipwa fedha zao zote za kujikimu. Tunaamini kila mtumishi anastahili kulipwa stahiki zake kikamilifu na kwa wakati ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ari na ufanisi katika kulitumikia taifa.

Fedha za Kujikimu.png
 
Back
Top Bottom