Mufti aagiza madrasa zote nchini kufungwa, swala ya Ijumaa kuswaliwa tofauti

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir ameagiza madrasa zote nchini kufungwa kuanzia leo Jumatano Machi 18, ili kupunguza ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Akizungumza na Mtanzania leo Jumatano Machi 18, jijini Dar es Salaam Sheikh Zubeir amesema agizo hilo linapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo na kwamba taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Amesema kuhusu Swala ya Ijumaa na ile ya Jamaa zitaruhusiwa kwa sasa na huenda itabadilishwa kulingana na mazingira ya ugonjwa huo.

“Kuanzia sasa swala za Jamaa zinapaswa kuswaliwa kwa kuachiana nafasi na kuzingatia usafi ili kupunguza maambukizi,” amesema Sheikh Zubeir.

Amesema kwa maeneo ambayo yanawashukiwa wa ugonjwa huo na yamewekwa karantini hairuhusiwi kuendelea na swala hizo kwani hata vitabu vya dini vinaelekeza kuwa ni dhambi kumuambukiza ugonjwa mwenzio kwa makusudi,” amesema.

Amesema muislamu yeyote atakayepata na maradhi haya ni haramu kwake kuhudhuria swala za Ijumaa na Jamaa kama ambavyo ni haramu kwake kuchanganyika na wengine kwani kufanya hivyo ni kuisambaza na kueneza ugonjwa huo kwa wenzake.

Chanzo: Mtanzania
 
....atakayepata na maradhi haya ni haramu kwake kuhudhuria swala za Ijumaa na Jamaa .... mekumbuka ule uzi uloletwa humu ukisema dini ndo mbaguzi wa kwanzaa kabsaa kwenye jamii
 
huo muda wa kuhudhuria jamaa atapata wapi wakati atakuwa kortini
 
Amesema kutakuwa na sala siku ya ijumaa tuu na jamaa na pia akasisitiza kuwa muislamu yeyote atakaepata corona huyo atakuwa najisi hivyo hatoruhusiwa kushiriki ibadani.
 
No anakosea anapoanza kuita watu najisi, na akiupata yeye je aitwe nani?inakera sana hii tabia ya mtu unateuliwa kiongozi kisha unasahau kwamba kuwa kwako kiongozi hakukufanyi kwa namna yoyote kuwa tofauti na wale unaowaongoza.

Imenikumbusha yule shehe aliyesema Corona ni adhabu kwa Wachina kwa sababu walichoma kitabu naye Corona ikampata.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
.
Your browser is not able to display this video.
 
ahsante mufti kwa maelekezo mazuri, naamini yatazingatiwa na wahusika wote kwa usalama wa waumini.
tujiepushe ili sote tubaki salama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwani najisi ni nini?
 
Mufti akipata muite tu hakuna shida si amesema Hapo kwenye maelezo yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…