Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzania, Dkt, Abubakar Zuber Bin Ally, amesema kuwa hakuna ukweli katika taarifa zinazosambazwa kwenye Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii zinazoashiria kuwa Wakristo wanawatukana au kuwafanyia fujo Waislam.
Mufti Zuber ameeleza hayo leo wakati akizungumza kwenye Baraza la Eid el Fitri Kitaifa, linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), huku akiongeza kuwa Jamii hizi mbili zimekuwa zikiishi kwa Amani na Mshikamano kwa muda mrefu, na kusisitiza kuwa hakuna hata tukio la aina hiyo lililowahi kuthibitishwa kutokea Nchini.
Aidha, ameonya kuhusu matumizi mabaya ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI), akisema kuwa baadhi ya watu wanaitumia kuzalisha taarifa za uongo zenye lengo la kuchochea chuki na migogoro ya kidini, na kuwataka Waislam na Wakristo kuendelea kudumisha Amani, kutopotoshwa na taarifa hizo, na kuepuka kuchokozeka ili kulinda mshikamano uliopo katika jamii.