Mzee Mwanakijiji,
Mkuu pengine nianze kwa kusema samahani ikiwa nimekukwaza.. Kalini siku zote mimi huandika with Authority ktk swala nalolifahamu - hoja zenye Critics huzijibu kwa critics sikuanza mimi kuuliza hayo..
Nimetumia UWT kama mfano na ajabu wewe umerukia UWT kwa sababu tu unafahamu hicho ni chombo cha CCM.. kisha ukaendelea kusema, wewe ukiwa mwana CCM una haki ya kuuliza. Ajabu ktk swala la mahakama ya kadhi wewe sii mwanachama,(Muislaam) wala mhusika wa Bakwata kwa njia yoyote ile, lakini umerukia kuuliza matumizi yake wakati huna unanachama ktk chombo hiki wala Uislaam..Kwa nini usiwaachie wana CCM (Waislaam) kuuliza kama ulivyojibu hapo nyuma!
Na unaposema CCM ndio hugharamia UWT una maana gani?, hizo fedha wanazipata toka wapi ikiwa CCM haina miradi ya kukiendesha chama hicho bila nguvu ya Watanzania wote.. Mkuu vyama vyote nchini mkuu vinaendeshwa na sisi wananchi iwe CCM, Chadema, CUF na kadhaliika. Pamoja na hayo naikubali hoja yakoi kama ulivyoandika na kujaribu kukutaarifu zaidi. Na kama umesoma vizuri nimeorodhesha taasisi nyinginezo ambazo umeziruka ukachagua moja kukidhi hoja yako.. U still wrong mkuu wangu. Ndio maana nikakupa mfano wa Pinda na majibu yake huko Kigoma.. huu ndio mtazamo wako ktk swala hili.
Kifupi ni lazima ukubali kwanza kwamba unaandika ukiwa kabatini hivyo ni vigumu kwako kuweza kuona nje ya kabati hilo.. Maneno yako ni mazito sawa na viongozi wa CCM ambao malalamiko ya vyama vingine kama Chadema, CUF na TLP huyaona upuuzi mtupu na malalamiko ya watu waliochioka..Wanaweka dharau badala ya kuzingatia kwamba kikatiba, kuwepo kwa demokrasia ndiyo inawapa wao nafasi ya kuongoza..Sasa ubaya wako ni pale unaposhindwa kuelewa kwanza malalamiko ya Waislaam na chombo chao kama vile CCM na viongozi wake wanapofumba macho ktk maswala ya vyama vinginevyo, hata kama hakuna haki ama utaratibu mzuri.
Je, unafikiri malalamiko mengi ya vyama kama Chadema ni uzushi mtupu? Sii kweli vyombo vya Usalama, NEC na vyombo vya serikali husimama upande wa CCM ktk chaguzi za Kitaifa?..Na pengine mawaziri khutumia fedha na mali za serikali ktk kampeni za chama CCM..Kwa nini unaona hakuna haja ya CCM kuyatazama maswala haya au mapendekezo ya vyama vingine..NMi kwa sababu CCM wanafikiria kwamba wao ndio watawala milelel huu mfumo wa vyama vingi ni geresha tu kwa nchi za magharibi.. Hivyo wewe pia unaona uhuru kwa waislaam ni geresha tu nchi yetu ni ya Kikristu na itaendeshwa kikristu.. Restriction ziendelee kama kawaida, hawataki wajikate wakaunde serikali yao. Siji wapi huko! ndio maneno yenu toka tuanze mada zinazohusu Waislaam..
Mkuu umeuliza hapo juu maswali ya A na B, kisha ukatoa suluhu ya C bila kufahamu kwamba Magistrate Court Act ya nchi yetu ina restrict matumizi ya islamic law ktk mahakama zetu..Kisha unahoji kwa nini waislaam wasitumie sheria zao. Hapa unafikiri nitakujibu vipi kama sii kuwa open minded (kutoka ktk kabati la udini) ukaelewa hoja ya Waislaam.
Swala hili ni sawa na lile la Bakwata kama unakumbuka tuliwahi kujadili mwka jana.. nikasema Bakwata ni chombo kilichoanzishwa na serikali. yaani sisi wote kwa mjumuiko wetu tunahusishwa moja kwa moja na Bakwata ktk matumizi yake.. we ask for that (Muslims and Christians), sasa ikiwa kuna swali waulize serikali na sii Waislaam ambao wangependa sana kujiongoza wao wenyewe bila baraka za serikiali.
Wewe kama Mkatoliki unajua fika kwamba Pengo hachaguliwi wala kuteuliwa na serikali ama Rais na hata ukitazama dini nyingine zote isipokuwa Waislaam. serikali au niseme CCM, imeingiza mkono wake ndani ya dini hii kiasi kwamba hata Mufti ni pandikizi la chama. Huyu anapewa nguvu ya kuchagua na kufukuza kiongozi yeyote wa dini kama atajisikia kufanya hivyo.. Unakumbuka mara ya mwisho alipokuwa India alifukuza uongozi wote wa Bakwata na kuweka mpya bila vigezo vya kidini isipokuwa maamuzi yake yalitokana na hitilafu za uongozi wa chama Bakwata. Bakwata ni chama under CCM zaidi ya kuwa jumuiya ya Waislaam.
Hivyo haya malalamiko yao ni ktk kujikomba kwa serikali wakitaka wapewe ulaji mwingine wakati Waislaam wenyewe wanahoji uhalali wa chombo hicho Bakwata..Huyo Mufti ni kiongozi wa Bakwata sii wa Waislaam isipokuwa tunalazimika kumkubali kama vile Mugabe na Zimbabwe kwani ndiye anayetambulika.
Ni hayo tu mkuu wangu ikiwa utakuwa open minded ukaelewa matatizo ndani ya Uislaam nchini ni rahisi sana kuweza kuona point nayozungumzia lakini unapokuja na hoja zilizopigwa mhuri ni vigumu kwako kuweza kuelewa.
Toka naandika hapa hujanisikia nikiwa critic na dini ya Kikristu isipokuwa waumini wenye kutazama nje ya mafundisho ya dini yao..Haina maana sina tofauti zangu au kutokubaliana na Ukristu lakini siwezi kuingilia mfumo wa dini yako wala ku question mambo ya ndani ya dini yako kwani hizo sababu ndizo zilinifanya nisiwe Mkristu..
Na kutokuwa kwangu Mkristu haina maana najitenga na wakristu wote, mambo yao yote na siwezi kula nao sahani moja..Nikifikia hapo ni upofu na hakikka nitakuwa nimejifungia ktk kabati la Udini.
Mkandara
Mkuu ulianza vyema sasa naona mnatupeleka kwenye malumbano.
swala la siasa na dini zinaharibu mwanzo/msingi mzuri wa hoja ambazo ulikuwa umezianzisha. Kama kweli CCM ndo ina msimika mufti hilo litakuwa ni tatizo la waumini wenyewe maana ninaimani CCM siyo ya wakristo tu
na wala siyo ya waislamu tu.
tuzungumzie faida na hasara za mahakama hii ili kwa wale wasiokuwa na mwanga walione wawe na maamzi sahihi.
Maswala ya UWT ni ya kisiasa zaidi.