Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katiba ya nchi ni kanuni ambazo jamii imejiwekea ili zifuatwe katika maisha yao ya kila siku. Kama suala ni kuingizwa kwenye katiba sioni ubaya ili mradi iwekwe wazi kuwa halazimishi mtu kwenye hilo. Mbona Hiyo BAKWATA Ilipoanzishwa wakati wa Nyerere maaskaofu hawakupinga?.
Halafu kama issue ni kuingizwa kwenye katiba, huoni kuwa kwa sheria hizohizo kuingizwa kwenye mahakama za kawaida zinakuwa tayari zimeingizwa kwenye katiba ( Sheria mama?). hoja yako bado imeelemea upande mmoja. Ndoa imefungishwa na Sheikh kwa sheria za dini yao ya kiislamu wewe hakimu Brown Christian unatumia sheria za dini isiyokuhusu kuhukumu wapi na wapi?. Huku ndiyo mwanzo wa kutafuta patashika. Kwa hili serikali imekosea inabidi watu waache idiology zao na kufanya kazi ya nchi sio maaskofu.
umesema kitu ambacho kinaitwa "bottom line". Suala la kadhi ni suala la fedha. Nani afadhili na kugharimia mahakama hizo? Uongozi wa Waislamu wanasema serikali! lakini at the same time hawataki serikali kuingilia kati!? So hilo litawezekana vipi?
Madrasa ni kaaazi kweli kweli.
Katiba ya nchi ni kanuni ambazo jamii imejiwekea ili zifuatwe katika maisha yao ya kila siku. Kama suala ni kuingizwa kwenye katiba sioni ubaya ili mradi iwekwe wazi kuwa halazimishi mtu kwenye hilo. Mbona Hiyo BAKWATA Ilipoanzishwa wakati wa Nyerere maaskaofu hawakupinga?.
Halafu kama issue ni kuingizwa kwenye katiba, huoni kuwa kwa sheria hizohizo kuingizwa kwenye mahakama za kawaida zinakuwa tayari zimeingizwa kwenye katiba ( Sheria mama?). hoja yako bado imeelemea upande mmoja. Ndoa imefungishwa na Sheikh kwa sheria za dini yao ya kiislamu wewe hakimu Brown Christian unatumia sheria za dini isiyokuhusu kuhukumu wapi na wapi?. Huku ndiyo mwanzo wa kutafuta patashika. Kwa hili serikali imekosea inabidi watu waache idiology zao na kufanya kazi ya nchi sio maaskofu.
Madrasa si kaazi bwana, nafikri developing countries kazi kwelikweli.... Kua mkweli haya ni matokeo ya be developing country , kwani asikudanganye mtu bwana hamna anae weza toa maamuzi yoyote juu ya nchi yake ikiwa kuna pressure za dunia ya kwanza.
Mwanakijiji,
Mkuu nitaendelea kukujibu kwa sababu bado kabisa majibu yako ni ndani ya kabati hilo ulojifungia... hutaki wala husikii sauti nje ya kabati hilo..
Mkuu binafsi sikubaliani na swala la mahakama ya kadhi kwa sababu za msingi ambazo hazihusiani kabisa na dini zetu.. Ni mahakama yenyewe ya kadhi nikitazama WATU na MAZINGIRA tunayoishi ndipo nakuja na hoja zangu..lakini wewe umeshikilia Udini tuuuu kiasi kwamba maswali yako ni ya kidini tupu... ukiwaona wao ni waislaam na wewe Mkristu.. mambo ya CCM na Chadema..kwa ufinyu huo ndio maana Pinda kajibu ujenzi wa barabara Kigoma umefanywa na chama chake - CCM..
Hivi nikuulize mambo ya wanawake mathaln UWT mbona huulizi nani alaipia gharama zake.
kwa nini usiwaambie wanawake wachukue dhamana ya matumizi ya chombo hicho badala ya taifa zima kulipa hali sisi sii wote wanawake..
Watoto Yatima, vilema, budget ya mikoa, wilaya kwa nini tunahusishwa sote wakati wengine haituhusu!.
.Haya ndio mawazo yako mkuu wangu unajaribu kutuvisha lakini huyo huyo Mwanakijiji inapofikia siasa huichambua CCM kama vile yeye sii mkristu anayepinga mambo mengine..
Mkuu, unapofikiria tu kuwa waislaam ni WAO, wale, na kadhalika tayari wewe umeshaweka utengano, yaani hao wana mabaya fulani ambayo wewe hutaki kuhusishwa, hivyo hoja yako haiwezi kujenga Umoja unataka kuutangaza hapa.bali kujitenga kama unavyojitenga na Ufisadi.
.Wewe unajua fika kwamba Magistrate Court Act yetu ina restrict matumizi ya Islamic law ktk maswala yote ya personal matters ya waislaam ambao Kikatiba wanaruhusiwa kufanya ibada hizo.
Sasa jiulize inakuwaje unamruhusu mtu kufanya ibada zake lakini inapofikia matatizo settlement ya dispute baina ya wahusika haifanyiki kufuata misingi ya dini..
Toka wakoloni Tanzania tulikuwa na mahakama za kadhi, toka Mreno, Mjarumani, Muingereza na hata baada ya Uhuru sheria nyingi za kiisilaam ziliendelea kutumika ktk legal framework..
Nitarudia kusema, kuwa mimi binafsi natazama nje ya box na nafanya hivyo sii kwa sababu ni Muislaam isipokuwa natazama wahusika na mustakabali wa nchi nzima kwa ujumla wake kwani binafsi sina mke zaidi ya mmoja, mirathi yangu ipo ktk will na kadhalika.
Binafsi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuweka vitu vyangu kulingana na mazingira ya hapa, nchi ambayo haitambui Uislaam zaidi ya dini ya Waarabu (Axis of evil)..kwangu poa vile vile lakini sii nyumbani ambaklo tunadai ati sisi ni nchi isiyokuwa na dini wakati tunatoa maamuzi mengi kufuata mfumo wa dini moja..
Kingine naelewa fika kwamba Tanzania ni Democratic secular State, imetoa ruksa kwetu sote yaani kila dini kuendesha shughuli zetu tofauti ktk maswala ndoa, Talaka, guardianship, Urithi na kadhalika lakini serikali hiyo hiyo inakataa (restrict)kutambua sheria za dini moja ktk maswala ambayo imeruhusu..Sasa jiulize kweli unawapa uhuru waislaam kuabudu au unawakaanga kwa mafuta yao wenyewe.
Hii ndio point ya hao Masheikh kutaka mahakama ya kadhi na kama utatumia sabnbabu zako mkuu unazidi kujenga hoja zao vizuri kwani unaonekana wewe ni Mdini..
Kinachotakiwa ni empirical and objective information.
Waarabu na wazungu tabia yao ya kulazimisha tushike dini zao ndiyo iliyotufikisha ha pa.
Ndiyo maana kwa hili nawapenda wahindi walikuja kuchukua pesa tu huku Afrika na siyo na imani zetu. Hivi na wahindi nao wangelazimisha imani zao naona nchi ingekuwa masikini zaidi duh! afadhali hawakufanya hivyo, yaani nchi isingekuwa na ng'ombe hata mmoja kwenye mabucha!!!!
Watu wanaweza kudhani ni utani, lakini sisi tulivyo? watu wangekuwa wanaandamana kupinga ulaji wa nyama ya Ng'ombe!!
Hebu angalia aibu hii, majitu mazima yanajiona bora kwa imani za kufikia!!!
Asilimi 60 ya Watanzania wana imani za dini zilizoletwa na Waarabu na Wazuungu kama unalichulikia jambo hili jepesi hebu siku moja jitose mskitini au kanisani uyatamke haya maneno unayo yaeleza hapa kwenye net huenda wakauelewa.
Ukisha ingia mskitini au kanisai sehemu yeyote ya Tanzania uambie "jamani eeh hivi ninyi mna akili kweli ninyi mijiti mizima mna jiona bora kwa imani za kifikia?"mie nahisi watakuelewa tu !
Bakwata hawana ubavu huo wanabwaka tu, wao wenyewe credibility yao ni questionable wasafishe nyumba yao kwanza.
Hawana jipya zaidi ya kutafuta njia ya kutokea na kuficha madudu yao. Ni ukweli usio na shaka uislam haupo kitaasisi kama ukristo na madhehebu yake catholics, Lutheran, Anglican nk. Bakwata ni kikundi cha wajanja wachache wasio na mandate yeyote kwa waislam ndio maana no body is taking them serious.
nimezipenda sana hizi analysis by mukandara
big up Mkuu
hizi information zingekuwa published kwenye news zingefaa sana kuikumbusha jamii ili tuweze kuwa pamoja kwani huku mitaani tunalopoka tu bila kujua tunataka nini