Mkuu haya maneno mekundu ndio mtazamo wa wengi wenu hapa na ndio sababu nikasema mtoke ktk hilo box.. Tunapolalamikia serikali au niseme CCM hatuna maana ni chombo cha Wakristu au Waislaam..Hakuna hata sehemu moja nimeihusisha dini ya Kikristu na CCM au serikali isipokuwa nimesema sheria nyingi zinazotumika ktk kesi za madai, huko Kortini (Primary Court), zinafuata sheria tulizopandikizwa na nchi za Magharibi ambazo kwa kiasi kikubwa zimefuata misingi ya Kikristu..
Je, ni vibaya Waislaam kuomba sheria zao zitumike pia? sidhani kama ni kosa kikatiba na hakuna mtu aliyesema sheria za zamani ziondolewe kwa sababu ni za Kikristu - hakuna. Na binafsi nina hakika ingekuwa ni kinyume yaani sheria za sasa hivi ni za kiislaam, basi Wakristu wasingekubali kabisa. Wangetaka sheria zote zibadilishwe na sii kuomba sheria zao zitumike pia ktk maswala ya ndoa na mirathi yao. Kwa hiyo ni vizuri kuangalia Waislaam wanataka kitu gani badala ya kuanza kpayuka ovyo bila kuelewa nini hasa kinachowazuia.
Sheria hizi zitakubalika tu ikiwa nchi yetu inafuata dini moja nayo ni ya Kikristu lakini maadam tumetoa uhuru kwa dini nyinginezo kama alivyosema Mwakanakijiji ktk swali lake la A na B iweje maamuzi ya maswala hayo yasifanywe kwa sheria za Kiislaam zilizowafungisha ndoa na kadhalika..Binafsi iwe mahakama ya kadhi au sio kinachonipa shida kuelewa ni uhuru waliopewa waislaam ktk maswala ya ndoa, mirathi na kadhalika wafuate mafundisho ya dini lakini inapofikia maamuzi ktk matatizo, hizo sheria za dini hazitambuliwi..Nina tatizo kuelewa hapa! na ndio muda wote nimekuwa nikizungumzia.
Binafsi sina malumbano ya kidini kuhusiana na maamuzi ya seriakali. Wapo wanaoamini kwamba kanisa Katoliki lina mkono ndani ktk maamuzi mengi ya serikali.. hao ni wao sii mimi, hivyo nihukumiwe kwa maandishi yangu..
Jokakuu,
Mkuu swala hili ni Ibada kwa Waislaam kutokana na sababu zile zile walizopewa kuabudu mwanzoni..Ibada haikomei pindi wanapooana tu ila huenda hadi kuachana, mirathi na hata kuingia kaburini.. Waislaam wanalipeleka swala hili Bungeni kwa sababu ndiko kwenye sheria kikatiba inayowapa ruksa kuendesha mambo yao ya dini kama walivyopewa wengine..
Hivyo maamuzi yote ya Sheikh au Ulamaa ktk maswala haya yanatakiwa kutambuliwa kisheria. Ikiwa MCA haitambui maamuzi ya nayotokana na islamic law unategemea naniu ataweza kukubali hukumu au settlement zilizofikiwa..
Sheria ni mwongozo mkuu wangu, leo hii tunalazimika Waislaam kuitambua Bakwata kama chombo cha Waislaam.. unataka wafanye nini kinyume kama sii kuitwa magaidi ambao wanahatarisha Usalama wa taifa. Unamkumbuka Sheikh Kassim Bin Jumaa alichokuwa akipinga ni uhalali wa Bakwata na akaanzisha chombo cha Waislaam kwa waislaam toka kwa Waislaam (Balukta), unajua yaliyomkuta!.. alitiwa Lupangoi akafanyiwa mambo mengi machafu hadi akatuondoka hivi hivi tu...Wengi walisherehjekea sana kukamatwa na hata kufa kwake..
Kwa hiyo, ikiwa Bunge litaweza kutambua sheria za kiislaam ktk maswala wanayoyataka iwe kwa kupitia vyombo vyetu vya sheria ni lazima MCA itawapa vifungu vya kutumia..Huo ndio mwongozo wa nchi, sheria yoyote ni lazima ikubalike Bungeni laa sivyo basi tutakuwa tunarudi nyuma katika sunia ya Wagagagigikoko!
Bunge letu wakiingiza baadhi ya sheria ambazo zinahusiana na ndoa, mirathi na mengineyo toka kwa waumini wake - binafsi, sidhani kama kuna haja ya kuwa na mahakama ya kadhi. Naamini kabisa kwamba kjazi inayotakiwa kufanywa na chombo hicho inaweza kabisa kutumika na kufanya kazi ktk mahakama zetu..Haijalishi kama Liwali ni mkristu au Muislaam, kwa sababu hadi leo tunahukumiwa na sheria au watu wenye imani za dini tofauti haina maana makosa mengi ktk hukumu hutokana na imani ya hakimu ktk dini.. Sheria ya Katiba ndiyo inamwongoza Liwali, Makimu au mtu yeyote ktk kutoa maamuzi..Alichojaribu kusema huyo Naibu Mufti ni kwamba 2+2 inaweza kuwa na jibu tofauyti ikiwa waumini ni dini tofauti, wakati uwezo wa kutoa hukumu hufuatana na elimu na sii imani ya mtu..