Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

hata nchi za kiislamu zina law school kwa nini basi wasitumie viongozi wa dini tuu

Mkuu hivi unaelewa nini kuhusu mahakama ya Kadhi?..unazumgumza vitu gani..
Kwani Waislaam Tanzania hawakusomea law.. Jaribu kwanza kuelewa tunazungumza kitu gani hapa..Kisha basi maswali yako yanauliza mambo ya ndoa na mirathi.... Haya wewe nambie hiyo law ulosomea inakufundisha nini kuhusu ndoa ikiwa mume ni Muislaam na mke ni Mkristu..Huko mlikosomea wanasemaje?
 
Last edited:
Mkuu kupayuka tena kunatoka wapi,hii lugha nadhani si ya kiugwana
hatupayuki tunajadiliana.Au wewe unaona ni kupayuka huko.
 
Mkuu kupayuka tena kunatoka wapi,hii lugha nadhani si ya kiugwana
hatupayuki tunajadiliana.Au wewe unaona ni kupayuka huko.
Wewe unaelewa vipi kuhusu neno hili kupayuka..Ulichoandika nadhani hukufikiria wala kusoma maandishi ya wengine.. hakuna mtu alosema CCM ni chombo cha Wakristu/Waislaam..kisha unawalaumu Waislaam.. maneno haya ni sawa kabisa na kupayuka!
 
..kabla hamjabishana zaidi naomba mpitie maoni ya kisheria kwenye link hapo chini kuhusu hoja ya mahakama ya kadhi.

..nawaomba wanachama mbonyeze hapa kupata maoni ya kitaalamu.
 
Wewe unaelewa vipi kuhusu neno hili kupayuka..Ulichoandika nadhani hukufikiria wala kusoma maandishi ya wengine.. hakuna mtu alosema CCM ni chombo cha Wakristu/Waislaam..kisha unawalaumu Waislaam.. maneno haya ni sawa kabisa na kupayuka!

Nadhani sasa nimekuelewa mkuu.
 
Jokakuu,
Mkuu nimeisoma lakini kama umeelewa utaona uzito wa hoja yao yote ni kuwepo kwa mahakama ya kadhi au niseme pawe na hakimu (Liwali) Muislaam. Hili ndio nalopinga mimi kwa sababu naelewa dhamira yao haswa sii ku settle matatizo ya Waislaam ila Ulaji mtupu. Kosa la serikali linatumika kama sababu ya ku raise issue nzima ya mapungufu ya sheria zetu..

Sheria ikisha andikwa mwanasheria yeyote anaweza kuisoma na kuitafsiri kulingana na matakwa ya dini..Soii lazima awe Muislaam kwani huyo Simba au huyo Rwambo wanaweza vipi kuwa wabora zaidi ya watu wengine ktk maamuzi ya hekima na busara hasa ktk maswala tata ya Ndoa na mirathi...
Pia tutashindwa ku deal na matatizo ambayo yako nje ya sheria za kidini kama vile watoto waliozaliwa nje ya ndoa. Ndio maana nikapendekeza zaidi serikali utumie vyombo vyake badala ya mahakama ya kadhi kwa sababu mwongozo wa dini haufuatwi hivyo kuwahukumu wahusika wakati sii waumini wa kweli isipokuwa kwa majina ni kuwaonea. Ila basi zipo sehemu muhimu ambazo zinatakiwa marekebisho ili kuondoa adha iliyopo sasa hivi ambapo sheria zetu haziutambui kabisa sheria za Kiislaam..

Hoja kubwa ya Uongozi wa Bakwata na hasa hao Maulamaa ni kutawa wao wapewe ulaji ndicho nachopinga isipokuwa sikubaliani na uhuru waliopewa Waislaam kisha wakanyinmwa haki ya kutumia sheria zao ktk settlement katika maswala hayo hayo.
Na ukisoma kwa mamikni mambo mengi yaliyozungumzwa hapa ni kama nilivyoelezea mimi pamoja na kwamba sina elimu ya sheria. Unapoona hakuna haki sii lazima uwe umesomea sheria..
 
Mkandara,

..kumbe tayari kuna mechanism/utaratibu ya kushughulikia haya masuala.

..utaratibu huo unaweza usiwe mzuri 100% lakini jambo la msingi ni kwamba upo.

..mimi nadhani it is OK to give a good fight, lakini in the end lazima ku-strike a MIDDLE GROUND.

..binafsi naona utaratibu uliopo uendelee kuboreshwa kwa msaada wa Wataalamu wa Sheria za Kiislamu.

..pia naungana na wewe 100% kwamba sheria zetu lazima ziwalinde watoto waliozaliwa nje ya ndoa, pamoja na kina mama waliozalishwa watoto lakini hawapewi matunzo.
 
Jokakuu,
Shukran sana!....
Umeona sasa baada ya malumbano mazito, at last tumefikia sehemu ya kati (Middle ground) na kama nilivyosema siku zote vitu vyote haviwezi kuwa in Black and White.. ni muhimu penye utatat tutazame gray areas ili kuweza kufikia muafaka lakini kama tutabakia na imani za CCM na Chadema na U CUF hatuwezi kujenga kitu bali kuongeza ufa zaidi la utengano..
Shukran tena kwa kunielewa!
 
Sheria zenu zikishawalinda watoto waliozaliwa nje ya ndoa hapo patakuwa hapaeleweki na ni kwenda kinyume na sheria ambazo waislamu wanatakiwa wazifuate ,ila nimewaelewa kuwa mmevaa ngozi ya kondoo,nimewasoma tokea mwanzo na kila siku zikienda mnazidi kutokeza rangi zenu.
Mahakama ya kadhi ni muhimu kwa kila aliekuwa Muislamu hao watakao pewa madaraka ikiwa wanatafuta ulaji kwa kila alie muislamu huwa hahusiki huko lawama zote watabeba wao siku ya siku.
 
..kabla hamjabishana zaidi naomba mpitie maoni ya kisheria kwenye link hapo chini kuhusu hoja ya mahakama ya kadhi.

..nawaomba wanachama mbonyeze hapa kupata maoni ya kitaalamu.

Asante JokaKuu - siyo tu nimeisoma, nimeiprint na nitaendelea kuitafakari. Hata hivyo jambo moja limenishtua kidogo, yaonekana dai la Mahakama ya Kadhi ni hatua tu ya mwanzo - makubwa zaidi yapo njiani kulingana na hii hitimisho:-


Ukianza kwa kupinga mamlaka yasiyoongozwa na taratibu za Kiislamu, maanake ni kuwa hauko tayari kuwa chini ya serikali isiyo ya Kiislamu. Naomba nisahihishwe.
 
mkandara
hii mahakama ya kadhi ni nzuri kama kila kitu kikiwa black and white, kesi zinahisha haraka au ata saingine watu wanaishia kurudiana kitu ambacho ni kizuri sana...
lakini kukishaanza kuwa na complication na tension baina ya mke na mume, mahakama ya serikali ndio mahali pekee

lazima ukubali dini zote (wakristu + waislamu) zinawakandamiza sana wanawake na ni vigumu sana wanawake kupata haki zao..

kuna kipindi kimoja cha sheria law britain nilikuwa nakiangaliaga zamani, uk kuna wapakistani wengi sana kwa hiyo wakawa wanatatua matatizo yao ya divorce kwa njia hii ya masheikh, watu wenye hela kidogo kesi zao nyingi zilikuwa zinaisha kwa ajili hamna cha kugawana kingi, lakini wale matajiri wake zao walikuwa wanahamisha hizo kesi na kuzipeleka mahakamani ili wakapate chao kisawasa, na ugomvi wa watoto pia ulikuwa unapelekwa mahakamani

je naomba kuuliza wanawake wataruhusiwa kuwa mahakimu wa kadhi????????
 
una bahati umezaliwa ndani ya ndoa
watoto waliozaliwa nje ya ndoa (mtoto wa haramu) wanatakiwa walindwe regardless of what quran says
tafadhali ukweli ni kwamba watoto wa nje ya ndoa wapo wengi na wa dini zote embu fikiria mzee mahita alivyozaa na house girl, je yule mtoto anakosa gani kwa nini asilindwe
 
Last edited:
Wakristo wa Tanzania wako katika makundi manne either a) wana wivu b) wana chuki c) wana -Uchungu na Kodi zetu d) au Ni christian conservative (fundemantalist) kwa jinsi wanavyo kataa kuwepo kwa mahakama ya kadhi? kwanini?
i. Hivi wakristo wa Tanzania ni wakristo sanaaaa kupita wakristo wa kenya au uganda ambako kuna mahakama hiyo kama siyo wivu, chuki, (choyo) uchungu (costs)? au imani kali!!!!
ii. Waislamu wana negoatiate na serikali (presumed to be secular) halafu in-between wakristo wana-counter attack wanaingilia majadiliano na kuanza blablah...why?
iii. Wataalamu serikalini walikuwa wanaendelea nayo vizuri hiyo issue mpaka tamko la maaskofu na baadhi ya maafidhina wa kikristo ndiyo the whole issue ikaharibika hivyo wakristo wa Tanzania kama siyo wivu!, Chuki na choyo what else can we say?
iii. Mbona waislamu hawana hizo roho mbaya kwa wakristo maana wakristo waki-negoatiate na serikali kama dili la (MoU) ambalo pesa za kodi zetu zote zinatumika kufinance shule, na dispensari za wakristo mbona waislamu wako cool tu? why when it comes to Muslims demand to goverment wakristo wanaingilia?? wivu, chuki. choyo au uchungu wa kodi zetu. naomba nifahamu??
 
Naona watu baada ya kuona thread zao zilisusiwa wanaandika yale yale kwenye thread zingine.
 
Naona watu baada ya kuona thread zao zilisusiwa wanaandika yale yale kwenye thread zingine.
Kwasababu kuna watu wanataka kusikia aina fulani ya habari nyingine zinazowa-touch hawataki kusikia!
 

Mkuu nadhani hukuisoma vizuri hitimisho hilo..

Kilichoandikwa ndicho nachozungumzia mimi kwamba mara nyingi ofisi ya Mufti inajishughulisha zaidi na mambo ya siasa, Ulaji, Unafiki na mengine kuliko maslahi ya Waislaam. Huko Zanzibar na Bara mambo mengi yanakiukwa na ofisi hizi jambo ambalo linawapa mashaka watu wengi kuhusiana na hatua nyingine wanayotaka kuchukua.
ndio maana nikasema ikiwa hawa viongozi wanashindwa kuongoza dini yao kwa mwongozo wa dini iweje wapewe zaidi mamlaka wakati wanaharibu na kukiuka mengi ya msingi..

Huyo Mwiba achacheni naye, wangu huyu maadam Muislaam najua fika mimi kiboko yake.. na kama atasoma maelezo hayo, basi bila shaka ataelewa vizuri utata wa mahakama ya kadhi kuwa mikononi mwa hawa wanaojiita Ulamaa..
Raha ya Uislaam tunaweza kabisa kuwachambua hata viongozi wetu kwani wao sii mitume wala waliobarikiwa..Ni binadamu kama sisi wenye kuweza kufanya mazuri na mabaya kama mtu mwingine yeyote. Walichonizidi ni elimu ya dini tu lakini matendo yetu naweza kuwa mbora kuliko wao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…