Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

wewe kawnini unabashiri ubaya tu si iwepo kwanza ndio useme kama wamaharibu? kabla hata haijaanzishwa ulishabashiri wataharibu tutafika kweli?
 

Mkuu kuzaliwa kwa huyo mtoto wa nje haina maana sheria za kiislaam zisitumike ktk sheria zetu. Sheria ya Kiislaam ktk Urithi inafuata mapendekezo yako yaani Will, zaidi ya mfumo wa kizungu ambao unatambua zaidi mama, mtoto wa damu kuliko wa nje,.
Hivyo Mahita ikiwa amemwandikisha mwanaye huyo wa nje kuwa mrithi wa mali yake basi ndilo litakalo kuwa mbele ktk mahakama.. Wadai wengine na sababu zao nyinginezo hupimwa uzito wake na pia nafasi ya wahusika ktk mirathi hiyo. Hii haina maana sheria za kiislaam zinapingana kabisa na kuzaliwa kwa mtoto huyu, unaweza mrithisha mtu ambaye huna hata nasaba naye. Huo ndio Uislaam.
 
Tatizo nalo ona hapa juu ya suala hili si kuwa wakristo wanauchungu na nchi yao bali tatizo ni athari za umasikini ndo zinapelekea wawe hivyo. Kwani hamna hoja hata moja wametoa yenye mashiko zaidi ya kusema waislam hawana uwezo wakujenga hoja , nakuwakejeli, kuwadharau na mambo kama hayo, so utaona yote haya ni athari za umasikini zinazo mfanya kila mtu awe mbinafsi, jamani angalieni hoja ya Mboma mkuu wa majeshi mstaafu alivyolielezea jambo hili kibusara, hao ndo watu tunawataka, watu kutoka na hasira za njaa na kuanza kuiamrisha serikali isikubaliane na masuala yanayotolewa na wananchi kama wao,waislam hawjaiamrisha serikali iwe na mahakama ya kadhi ,ila inaimba serikali ilifanyie kazi.

Kinachoshangaza zaidi nipale wakiristo kuwa na ilani za vyama vyao nao kuzitumia kama ndo muongozo wa nchi, manake wanadai wataka serikali itekeleze, sasa tujue nao ni chama cha upinzani au chama cha dini? Jamani tuipende nchi yetu, tusijisahau sana manake tutaenda pabaya, Lora nkunda nae alikua anajifanya ni mwanadini , lakini akafanya aliyofanya na kusababisha mauji na dhiki kwa wanakongo, jamani tunajisau mnoo, wengine mnaingilia hata madaraka ya nchi.
 
Amwanga,
Hapa mkuu nakukatalia kwa sababu hata Masheikh na hao kina Mufti nao pia wanaingilia sana siasa. Sema labda wewe hujasoma hotuba zao, ni wao hawa huwaombea dua viongozi wa CCM wachaguliwe...Wengine hupiga bao na kutumia Kuran ktk uchafu wao ili mradi kiongozi fulani apite uchaguzi..elimu waliyopewa wanaitumia vibaya ktk maswala ya unafiki na husda.
Huwezi kulalamikia dini isipokuwa tuwalaumu viongozi wa dini hiizi wanapotumia vibaya madaraka walokabidhiwa..Sisi sote tuna makosa makubwa inapofikia maswala ya siasa.
 
Mimi nafikiri siyo umaskini ni aina fulani ya wivu mkapa anauita wivu wa kike....
 
Tumain,
Mkuu sibashir isipokuwa ndio hali halisi... Naelewa vizuri WATU na MAZINGIRA yetu ndio maana kila napotoa hoja zangu hutazama nje ya box hilo na kukubali reality!
 
Last edited:
Mkanara,
You are talking, nafikiri wote wanaofanya hivyo ni kwa sababu za athari za umasikini kwani wanakimbilia kutibu nja zao kwa kuwadanganya waumini. Halafu mbaya ni pale wanaponyimwa chakula pale wanapotega, hurudi kwa taswira nzu kwa waumini kuwakataa viongozi wa nchi, na kwa kua ss waumini tupo kwenye dimbwi la umasikini wanatuzoa na kutuendesha, but kizuri wa tz hawapendi kupigana, ingekua kongo, burundi, kenya saizi tungekua tunazungumza mengine, tuombe mungu tusifikie huko kutokana na ushawishi wa watu fulani.
 
 
sawa kaka, huwezi kuacha kuandika bila hasira jamaa wanaboa sana kwa hoja wanazotoa, nimekubali ushauri wako
suppose imekataliwa what next for Mufti?
 
 
Mimi nafikiri tunaende hatua kwa hatua, hayo itakuwaje huko mbele ukijadili kabla haijaanza ndio kusema isiwepo au unatoa solution gani?

Mkuu nimeandika ushauri mkubwa huklo nyuma labda kasome nada inayozungumzia serikali kukataa mahakama ya kadhi badala yake watachukua sheria za kiislaam zipate kukubalika na mahakama zetu..
Hii ni hatua nzuri zaidi kiasi kwamba unaweza kukata rufaa hadi high korti ambako pia watafuata vifungu vya sheria hiyo kuliko kutegemea uamuzi wa Mufti au watu ambao huyo Mufti atawapanga kwa sababu hatuwezi kupuuza mambo haya hasa inapofikia maswala ya dini. Kumbuka ni hawa hawa waliuza kiwanja cha shule kule Temeke halafu leo uwape ulaji mwingine itakuwa CCM ina the making!
 
Ukitaka kujua rangi zetu za kweli Watanzania basi ingiza maswala ya dini. Uko tunakokwenda hmmmm!!
 
Hivi Bakwata au Chombo chchote kinacho ongoza Waislamu, kama baraza la kuendeleza Kuran, wakichagua wanazuoni wao na kuendesha Mahakama hizo za Kiislamu, hususan katika kutoa maamuzi ya ndoa, mirathi nk itakuwa haitoshi? mpaka mahakama hiyo ianzishwe na serikali? ili mradi wahusika wakuu wa hizo kesi wakubaliane kwamba ikiwa ndoa yangu itaingia mgogoro au mirathi yangu basi hatua ya kwanza ni balukta au bakwata. kwa mafano mimi ni mkristo itakapo tokea ya kutokea ni aidha niende mahakama za serikali au niende kwa paroko wangu, hiyo ndio au ndio njia nilizo nazo. period, sina haja ya kugombana na mtu, wa kugomba nami ni nafsi yangu.
 
Wamezidi ahadi za ulongo, wakome. Hahaaaaaaaaaaa! Big up mufuti.
 
Viongozi wetu wana web site ya Uongo na kuna baadhi yao Ukipisha nao wananuka Uongo.
 
Kwanini isiwe wakristo kwenda kwa waislamu kwanza kabla ya kukurupuka na kujidai christians view is the natioanl view? (wanayofikiria kwamba watafanyia kazi watanzania wote...shame on them kwa leta unecessary tension!
My point is: Wakristu na Waislamu wa Tanzania ni wawe "responsible" kwa mambo yao. Mie sioni tatizo lolote ku-create communication dialogue in betwee. Wa-Umini wa dini hizi zote karibu weng ni ndugu; marafiki nk. Je dini ni bora kuliko undugu wetu hata kutufanya tuwe maadui wa kuapizana kiasi hiki? I frankly don't see any advantage of being a christian or a muslim if i will be creating such enemity.
 
Good point mkuu lakini kama hufahamu na unataka kufahamu kuwa sisi - NDIVYO TULIVYO, soma mada zinazohusiana na dini...true color (enemity) hujitokeza. Now it's up to you kama utakubali matokeo ama utajaribu kuondoa kiwingu..
 
waende wakatafute nchi ya kwao binafsi. waende kule mafia. huyu mufti wao mwenyewe anayetisha ukimwangalia, duh, Mungu na amwondoshee mbali. muda wake naye uko karibu. asipookoka na kumfuata Bwana Yesu, siku zake zinahesabiwa. watu wanaomba sana apotelee mbali na kadhi zake, akahukumiwe nazo huko kuzimu. ameshindwa kwa Jina la Yesu.
 
Haooo wamekuja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…