Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Kwanini isiwe wakristo kwenda kwa waislamu kwanza kabla ya kukurupuka na kujidai christians view is the natioanl view? (wanayofikiria kwamba watafanyia kazi watanzania wote...shame on them kwa leta unecessary tension!
 


nimezipenda sana hizi analysis by mukandara
big up Mkuu
hizi information zingekuwa published kwenye news zingefaa sana kuikumbusha jamii ili tuweze kuwa pamoja kwani huku mitaani tunalopoka tu bila kujua tunataka nini
 
Bado hujaona umuhimu wa binadamu wenzako kupewa haki zao za ibada shame on you! bado sijaona kiongozi TZ ambaye anaweza kuleta harmony among her people!
 
kwanza namshangaa mtu kama mwanakijiji,duh sikutegemea kama utaweza kuropoka mtu kama wewe...
halafu basi,jamani hii mahakama ya kadhi waislam hawataki iletwe bali wanataka irudishwe,hii ni hakki ya waislam kwani ilikuwepo hapo mwanzo na ikaondolewa watu wenye chuki zao binafsi,na mbona nchi nyingi tu tena zinaongozwa na wakristo nyengine wanazo mahakama ya kadhi,hii ni kwa sababu ktk nchi madhehebu yote ya dini yanayo hakki sawa,na serikali inatakiwa ihakikishe haiwaingilii kk ibada zao, waislam ktk nchi hii wana hakki,na wanatakiwa wasikilizwe sio wakisema kanisa tu ndo wasikilizwe kama juzi tu hapa tumeona ndani ya masaa 48 limetoka tamko kuhusu msamaha wa kodi na wakristo wakasikilizwa tena kwa kutoa kauli kali na za kuitisha dhidi ya serikali,je wao tu ndo wana hakki? NO,HAIWEZEKANI.. WAKATI UMEFIKA...

Msiulize masuala mengi,nendeni kaulizeni kenya,uganda,afika kusini,znz na kwengineko.. wote hao wana mahakama ya kadhi kwa kuwa wanatambua kuwa hiyo ni hakki ya waislam.. nashangaa hata hiyo OIC mbona ni nchi nyingi tu tena nyengine za kikristo wamo ktk jumuiya hiyo,MBONA WENZETU WANAISHI KWA KUHESHIMIANA? KWA NINI NYINYI HAPA TZ MTUNYANYASE? KWA NINI HAMTUHESHIMU?
 
Kwanini isiwe wakristo kwenda kwa waislamu kwanza kabla ya kukurupuka na kujidai christians view is the natioanl view? (wanayofikiria kwamba watafanyia kazi watanzania wote...shame on them kwa leta unecessary tension!

Waislamu wanayo haki kabisa ya kuwa na chombo chao cha dini yao katika kushughulikia masuala yao ili mradi tu hawamlazimishi mtu kukitumia kama ilivyo kwa kutowalazimisha watu kusali sala tano au kuacha pombe na kiti moto n.k.

Kinachokasirisha hapa ni hawa maaskofu kulivalia njuga suala lisilowahusu kuwa mahakama ya kadhi haifai, hii ni kama kusema kuwa "dini ya uislamu haifai". Kwa kuwa maoni ya maaskofu yameonekana kupewa uzito zaidi ya waislamu wenyewe katika kufikia uamuzi huu, basi hapa ndipo suala "christian view is the national view" linapoingia.

Waislamu waachwe wafanye ibada zao ambazo ni pamoja na kuwa na chombo chao cha kutenda haki ili mradi haiwahusu wakristo. CCM inajua kuwa itashinda kwa vyovyote hata kama waislamu hawataipigia kura ila wajue kuwa sasa nchi inaelekea pabaya, pale kundi moja la dini linapoona kuwa halitendewi haki kama kundi la dini ya pili. Kwa nini waislamu hawapingi ubalozi wa Vatican nchini?. Jibu ni simple hauwahusu sasa ninyi msio wailslam ni vipi yanawahusu ya waislamu?. Pilipili...
 

Mkuu ninatakaniamini kuwa hujaelewa msimamo wa makasisi na taasisi za Kikristo. Wanachokataa ni kadhi kuingizwa kwenye katiba ya nchi, siyo kuanzishwa kwa kadhi. Waislamu wanaweza kuanzisha mahakama hiyo bila kuulizwa na Wakristo au wasio na dini. Mkuu, kinachopingwa ni kadhi kuingizwa kwenye katiba ya nchi.
 

Tatizo hapa Mwanakijiji ni kuwa kila mpiga kura anapoenda kupiga kura huwa anakuwa na sababu yake ya kuchangua chama fulani au mgombea fulani. Kwa mfano, kama mimi ni mwalimu inawezekana nikapiga kura kwa kuangalia ni kiasi gani huyo mgombea ataboresha hali yangu kama mwalimu. Kama ni mkulima nitaangalia ni kiasi gani huyo mgombea atatatua matatizo yangu ya ukulima. Vivyohivyo, katika kupima mafanikio au kushindwa kwa mgombea niliyemchagua nitaangalia ni kwa kiasi gani amejibu yale matakwa yangu ambayo yalinifanye nimchague.

Ndiyo kusema kwamba kama waislamu (na hasa BAKWATA) waliichagua CCM mwaka 2005 kwa kuwa iliwaahidi kuanzisha mahakama ya kadhi, na kama wanaona wameshindwa kutekeleza hilo wana haki ya kuwapiga CCM huu mkwara. Ndiyo kusema sio lazima yale yanayowagusa watu wengine yawaguse BAKWATA. Kwa hivyo binafsi siwezi kuwalaumu wala kuwashangaa BAKWATA kama wataamua kuinyima kura CCM kwa sababu ya kusaliti au kushindwa kutekeleza ahadi waliotoa wao wenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote kuhusu kadhi mkuu. Hivi ndivyo wapiga kura wanavyotofautiana.

Msimamo huu wa BAKWATA, wakiutekeleza itatusaidia sana kuondokana na siasa za kinafiki za kuahidi mambo ambayo unajua huwezi kuyafanya, bali unafanya hivyo ili upate kura. Mimi nasema BAKWATA wakaze kamba hapa, watekeleze ahadi yao; wasije sasa na wao wakadanganya kama wao walivyodanganywa na CCM!
 
Inaonekana kuwa Waislam bado wanaongozwa na bayana ya wamazo. It is unethical to have two judicial conduits at the same time. Meaning islamic kadhi and GOV laws.

Islamic kadhi cannot be at par with GOV laws, since Tanzania is not an islamic nation. Islam can execute what ever is in Koran, but if it is contrary to the nation's laws, then, the laws of GOV of Tanzania will prevail and overwrite the islamic kadhi/sharia, that is the bottom line.
 
..katika masuala mazito na polarizing kama haya inabidi kutafuta MIDDLE GROUND.

..binafsi nadhani serikali imesikiliza kilio cha Waislamu, kwa kukubali kuziboresha sheria za mirathi na ndoa ili ziweze kukidhi mahitaji ya Waislamu.

..kuna wanaofananisha Mahakama ya Kadhi na Mahakama ya Biashara, lakini wanasahau kwamba wafanyabiashara hawakulazimisha Majaji wa mahakama hiyo lazima wawe ni wafanyabiashara.
 

Ni kweli kabisa kila kundi linapaswa kuwa na msimamo huo ikiwa halijatekelezewa matakwa yake. hii itatusaidia kupata viongozi bora na kuleta maendeleo.
Lakini je BAKWATA inaungwa mkono na asilimia ngapi ya waislamu? maana kama haiungwi mkono huo mkwara hauna maana. Maelezo ya Mkandara hapo juu yanaonyesha BAKWATA inatizamwa tofauti na waislamu walio wengi, sijui wenzangu mnalionaje hili? waislamu ni wamoja kiasi hicho?
 

Hoja zako ni nzuri isipokuwa unapoleta ad hominem. Lakini pamoja na uzuri wa hoja zako ni dhaifu vile vile.

a. Viongozi wa dini hawaongozi katika masuala ya dini tu. Dini kimsingi ni majumuisho ya mambo yote yanayohusiana na ibada, imani, na maisha ya muumini. Hivyo, dini siyo kwenda kanisani tu au msikitini au kusoma Qurani au Biblia bali ni kuishi kiimani kwa mafunzo ya dini hiyo.

Hivyo, dini hutufunza kuhusiana na majirani zetu, juu ya masuala ya fedha, biashara n.k Hivyo, ni vigumu sana kutenganisha maisha ya dini na maisha mwenye dini kwani vitu hivyo vimeshikana sana. Hivyo, kiongozi wa dini anaposhikilia suala la dini tu na akatofautisha hilo na maisha ya muumini basi haitendei dini haki.

Kiongozi wa dini anapoona au anapofahamu kuwa muumini wa kanisa au msikiti wake anaendesha danguro kwa mfano, je anasababu ya kujaribu kumshawishi au kumpa somo juu ya msimamowa kidini na jinsi gani mambo hayo ya danguro ni kinyume na dini? Au atakaa pembeni na kusema kile muumini anachofanya nje ya nyumba ya ibada hakikuhusiani na dini?

Ni kwa sababu hiyo viongozi wa dini huzungumzia mambo ya kutenda mema, haki, usawa, upendo, uaminifu n.k vitu ambavyo application yake ni zaidi ya suala la kumpendeza Mungu.

b. Kiongozi wa dini asiyekemea maovu katika jamii anapoteza umuhimu wake. Hili ndilo tatizo ambalo nimekuwa nalo kwa wachungaji na mapadre na mashehe wetu na nimeliandiika karibu mara tatu. Kwamba hawa viongozi wa dini wamejifunga na kulala kitanda kimoja na watawala kiasi kwamba imekuwa kwao vigumu kuukemea uovu ambao unafanywa na watawala hao au kwa majina ya watawala hao.

c. Mambo ya Watanzania yawaguse Watanzania wote. Kwenye suala la kadhi na masuala kadhaa yanayoibuliwa na baadhi ya Waislamu tatizo langu ni kuwa yamekuwa ni ya Waislamu na si ya Watanzania, na yale ya Watanzania wote hayagusi sana hadi pale yanapokuwa ya Waislamu. Hili nitalifafanua zaidi wiki ijayo kumjibu Mufti na Bakwata.

Kina Khalifa Khamisi na wenzake walianzisha chombo cha kugomboa au kudai mali wakfu za Waislamu ambazo inadaiwa zilichukuliwa au kuuzwa kinyemela. Wamefanya hivi vizuri na kuvutia waislamu wengi kukubaliana nao na kuwaunga mkono. Wamekuwa wakali sana mali za Waislamu zilipochukuliwa au kutumiwa vibaya na mfano mzuri ni suala lao na Yusuph Manji.

Na hata kwenye hili tunaona jinsi gani Mahakama ya Kadhi ni suala la Waislamu tu na kwa kweli linawaudhi baadhi yao hadi kuitisha kuisusia CCM. Lakini kwanini misimamo hii mikali ije kwenye masuala yanayohusu jamii moja tu ya Watanzania? Kwanini ukali huu usije na kuwa juu ya mali za Watanzania zinavyotumiwa vibaya? Kwanini, Wachungaji, Mashehe n.k hawajawahi kutoa kauli kali juu ya Meremeta, EPA, n.k ?

Ninafahamu sentiments za kidini. Hata hivyo muumini mzuri si yule anayetetea dini yake tu bali yule anayesimama dhidi ya wanyonge, anayesimama dhidi ya uvunjwaji wa haki za binadamu, anayesimama dhidi ya wizi wa mali ya umma n.k Yaani, ni yule anayekwenda zaidi na juu ya wito wake wa kidini.

d. Mahakama ya Kadhi
Binafsi tangu awali ninaunga mkono Waislamu kuwa na Mahakama yao ya Kadhi. Lakini ni wao wenyewe wanalifanya jambo hili kuwa gumu kweli. Upande mmoja wanataka serikali iunde lakini upande mwingine hawataki Wakristu wawe sehemu ya kuundwa huko. Huku ni kujipinga.

- CCM ina Wakristu, Waislamu na watu wa dini nyingine na wale wasio na dini. Je ni sehemu gani ya wana CCM ijadili na kupitisha suala la Kadhi?

- Serikali ina wakrisstu na waislamu kwenye watendaji wake. Je ni sehemu gani ya watumishi wa Serikali wajadili na kusimamia uundwaji wa Mahakama ya Kadhi? Je wakristu serikalini wakae pembeni na kuwaachia waislamu walioko serikalini kujadili, kusimamia n.k hiyo mahakama ya kadhi?

- Bungeni wapo Wakristu na Waislamu na wengine. Upande mmoja wanataka Bunge lipitishe mahakama ya kadhi, lakini upande mwingine wanasema itakuwaje Mkristu aamue juu ya suala la kadhi? Sasa, huko Bungeni mjadala huu ukija waachiwe kina Mudhihir na Msambya na kina Slaa na Mwakyembe wake nje?

e. Suluhisho langu bado ni lile lile.
Waislamu kwa vile sasa wameungana, wafanye kile Wakatoliki na Waanglikana wamekifanya kwa miaka mamia sasa, wajiundie mahakama zao nje ya mamlaka za serikali kwa vile wamesema ni sehemu ya ibada basi watekeleze ibada yao. Serikali haiwezi kuingilia ibada hiyo.
 
Ndiyo kusema kwamba kama waislamu (na hasa BAKWATA) waliichagua CCM mwaka 2005 kwa kuwa iliwaahidi kuanzisha mahakama ya kadhi, na kama wanaona wameshindwa kutekeleza hilo wana haki ya kuwapiga CCM huu mkwara.

Mwalimu, mojawapo ya mambo ambayo yamekubaliwa kuwa ni ukweli ni kama hilo. Sijui ni wangapi humu wameisoma Ilani ya CCM. Ilani ya CCM haikutoa ahadi ya kuanzisha mahakama ya kadhi. Na sijui kwanini CCM hawawaambii ukweli kile walichoahidi. Mkuu isome utashangaa imeahidi nini.
 
hii ni kwa sababu ktk nchi madhehebu yote ya dini yanayo hakki sawa,na serikali inatakiwa ihakikishe haiwaingilii kk ibada zao, waislam ktk nchi hii wana hakki,na wanatakiwa wasikilizwe


Sasa kama ni suala la ibada na kuwa ni sehemu ya ibada na ya kuwa serikali isiingilie ibada hiyo, kwa kuitaka serikali kuunda chombo cha ibada siyo kwamba serikali inaingilia ibada hiyo? au hiyo ni exception? Mbona Rais wa Zanzibar ndiye anamteua Kadhi Mkuu wa Zanzibar?

Msiulize masuala mengi,nendeni kaulizeni kenya,uganda,afika kusini,znz na kwengineko..

Mbona India kuna mahakama za Kadhi lakini haziko kwenye Katiba? Kwanini tusifuate mfano huo wa India? Mbona kuna nchi zenye Waislamu wengi na hazina mahakama za Kadhi?
 
watagawanyika tuu hivi, jamaa wanatafuta bei zao. serikali iwaweke lupango waache kelele.
Umewahi kusikia Uhuru wa kujieleza? umewahi kusikia utawala wa sheria? umewahi kusikia kitu kinaitwa haki za raia? uko dunia ipi wewe???
 
Mwanakijiji,

..suala hili la Ofisi ya Kadhi kuwa chini ya serikali liliwapa matatizo hata wenzetu wa Zanzibar.

..kulitokea mabishano ilipobainika kwamba Kadhi Mkuu ameteuliwa na Raisi wa ZNZ kwa ushauri wa Waziri Brig.Adam Mwakanjuki ambaye ni Mkristo.
 

Ndiyo maana suala la serikali isiingilie dini siyo hoja kwani tayari imeingilia na wanaiomba iingilie!
 
Hapa ni suala kubwa . kwamba Bakwata wanajua wanataka/kuomba nini na serikali haijui imekataa nini.Kwa jinsi ya uelewa wangu ni kwamba bakwata ilitaka serikali iwaanzishie mahakama ya kaadhi.Na serikali imesema NO.Kama sheria za mirathi ni ibada serikali haizuii ibada basi Bakwata ianzishe mahakama hizo nahakika serikali haitazuia. jambo ambalo bakwata hawawezi kutokana na kukithiri kwa ufusadi ndani ya bakwata kwa sababu hawana fedha za kuendesha.Kilichabakia ni kung'ang'ania serikali itoe fedha za kuanzisha mahakama hizo.Kwa kuwa serikali haina Dini haiwezi kuanzisha mfumo wa ibada kwa dini yeyote.Jibu la serikali lingekuwa serikali haina kizuizi kwa waislamu kuanzisha mahakama ya Kaadhi.Ila serikali haitahusika na kuziendesha au kuzigharimikia kwa sababu hiyo ni sehemu ya ibada.Lakini kauli ya serikali katika bunge inaonyesha ilitaka kuwapendeza wanaopinga mahakama ya kaadhi hata kama hawahusiki nayo.
 

umesema kitu ambacho kinaitwa "bottom line". Suala la kadhi ni suala la fedha. Nani afadhili na kugharimia mahakama hizo? Uongozi wa Waislamu wanasema serikali! lakini at the same time hawataki serikali kuingilia kati!? So hilo litawezekana vipi?
 
Nakubaliana na hoja dhidi ya mahakama ya kadhi kuanzishwa na serikali. Mufti ametimua vumbi, amejiaibisha mwenyewe na uislamu anaodai kuutetea. Zaidi sana tunaanza hata kuhoji upeo wake kitaaluma. Yeye ni kiongozi mkuu, sasa anashindwa nini kuanzisha mahakama ya kadhi chini ya gharama, usimamizi, na uendeshaji wa dini yake? Kwanini anaisubiri Dodoma imuamulie? Hajui kuwa dini zingine ikiwemo ukristu zimeanzisha mambo hayo miaka mingi iliyopita?! Mambo ya ibada ya dini yake anataka yabebwe na Bunge/serikali? LOL!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…