Sekenke,
Mkuu Mwanakijiji, hawa ni Viongozi wa dini na wanawakilisha waumini wa dini, hii ndiyo kazi yao kidini sii kuingilia Siasa ambazo hawana hata hzihusiani na dini wala hawana elimu nayo..Ikiwa Mapadre wenu wanaingilia Siasa hata ktk maswala yasiyohusiana na ibada zenu hiyo ni Ukristu wenu, usitake kuwavuta waislaam pia kuiga yanayopfanywa na Wakristu. Mufti akiingilia siasa hizi basi jua anazungumza kama raia mwninge na anaweza kuja hapa kijiweni kama Mkandara!
Hoja zako ni nzuri isipokuwa unapoleta ad hominem. Lakini pamoja na uzuri wa hoja zako ni dhaifu vile vile.
a. Viongozi wa dini hawaongozi katika masuala ya dini tu. Dini kimsingi ni majumuisho ya mambo yote yanayohusiana na ibada, imani, na maisha ya muumini. Hivyo, dini siyo kwenda kanisani tu au msikitini au kusoma Qurani au Biblia bali ni kuishi kiimani kwa mafunzo ya dini hiyo.
Hivyo, dini hutufunza kuhusiana na majirani zetu, juu ya masuala ya fedha, biashara n.k Hivyo, ni vigumu sana kutenganisha maisha ya dini na maisha mwenye dini kwani vitu hivyo vimeshikana sana. Hivyo, kiongozi wa dini anaposhikilia suala la dini tu na akatofautisha hilo na maisha ya muumini basi haitendei dini haki.
Kiongozi wa dini anapoona au anapofahamu kuwa muumini wa kanisa au msikiti wake anaendesha danguro kwa mfano, je anasababu ya kujaribu kumshawishi au kumpa somo juu ya msimamowa kidini na jinsi gani mambo hayo ya danguro ni kinyume na dini? Au atakaa pembeni na kusema kile muumini anachofanya nje ya nyumba ya ibada hakikuhusiani na dini?
Ni kwa sababu hiyo viongozi wa dini huzungumzia mambo ya kutenda mema, haki, usawa, upendo, uaminifu n.k vitu ambavyo application yake ni zaidi ya suala la kumpendeza Mungu.
b. Kiongozi wa dini asiyekemea maovu katika jamii anapoteza umuhimu wake. Hili ndilo tatizo ambalo nimekuwa nalo kwa wachungaji na mapadre na mashehe wetu na nimeliandiika karibu mara tatu. Kwamba hawa viongozi wa dini wamejifunga na kulala kitanda kimoja na watawala kiasi kwamba imekuwa kwao vigumu kuukemea uovu ambao unafanywa na watawala hao au kwa majina ya watawala hao.
c. Mambo ya Watanzania yawaguse Watanzania wote. Kwenye suala la kadhi na masuala kadhaa yanayoibuliwa na baadhi ya Waislamu tatizo langu ni kuwa yamekuwa ni ya Waislamu na si ya Watanzania, na yale ya Watanzania wote hayagusi sana hadi pale yanapokuwa ya Waislamu. Hili nitalifafanua zaidi wiki ijayo kumjibu Mufti na Bakwata.
Kina Khalifa Khamisi na wenzake walianzisha chombo cha kugomboa au kudai mali wakfu za Waislamu ambazo inadaiwa zilichukuliwa au kuuzwa kinyemela. Wamefanya hivi vizuri na kuvutia waislamu wengi kukubaliana nao na kuwaunga mkono. Wamekuwa wakali sana mali za Waislamu zilipochukuliwa au kutumiwa vibaya na mfano mzuri ni suala lao na Yusuph Manji.
Na hata kwenye hili tunaona jinsi gani Mahakama ya Kadhi ni suala la Waislamu tu na kwa kweli linawaudhi baadhi yao hadi kuitisha kuisusia CCM. Lakini kwanini misimamo hii mikali ije kwenye masuala yanayohusu jamii moja tu ya Watanzania? Kwanini ukali huu usije na kuwa juu ya mali za Watanzania zinavyotumiwa vibaya? Kwanini, Wachungaji, Mashehe n.k hawajawahi kutoa kauli kali juu ya Meremeta, EPA, n.k ?
Ninafahamu sentiments za kidini. Hata hivyo muumini mzuri si yule anayetetea dini yake tu bali yule anayesimama dhidi ya wanyonge, anayesimama dhidi ya uvunjwaji wa haki za binadamu, anayesimama dhidi ya wizi wa mali ya umma n.k Yaani, ni yule anayekwenda zaidi na juu ya wito wake wa kidini.
d. Mahakama ya Kadhi
Binafsi tangu awali ninaunga mkono Waislamu kuwa na Mahakama yao ya Kadhi. Lakini ni wao wenyewe wanalifanya jambo hili kuwa gumu kweli. Upande mmoja wanataka serikali iunde lakini upande mwingine hawataki Wakristu wawe sehemu ya kuundwa huko. Huku ni kujipinga.
- CCM ina Wakristu, Waislamu na watu wa dini nyingine na wale wasio na dini. Je ni sehemu gani ya wana CCM ijadili na kupitisha suala la Kadhi?
- Serikali ina wakrisstu na waislamu kwenye watendaji wake. Je ni sehemu gani ya watumishi wa Serikali wajadili na kusimamia uundwaji wa Mahakama ya Kadhi? Je wakristu serikalini wakae pembeni na kuwaachia waislamu walioko serikalini kujadili, kusimamia n.k hiyo mahakama ya kadhi?
- Bungeni wapo Wakristu na Waislamu na wengine. Upande mmoja wanataka Bunge lipitishe mahakama ya kadhi, lakini upande mwingine wanasema itakuwaje Mkristu aamue juu ya suala la kadhi? Sasa, huko Bungeni mjadala huu ukija waachiwe kina Mudhihir na Msambya na kina Slaa na Mwakyembe wake nje?
e. Suluhisho langu bado ni lile lile.
Waislamu kwa vile sasa wameungana, wafanye kile Wakatoliki na Waanglikana wamekifanya kwa miaka mamia sasa, wajiundie mahakama zao nje ya mamlaka za serikali kwa vile wamesema ni sehemu ya ibada basi watekeleze ibada yao. Serikali haiwezi kuingilia ibada hiyo.